Noti mpya hazina ubora?

Walivyo zizindua kwa mbwembwe nilidhani wanafanya kitu cha maana kumbe danganya toto kweli TZ tunasafari ndefu. Hao BOT wanatufanya sisi ni wajinga kama wao ipo siku watanzania watakapo amua kuiondoa CCM madarakani watajua ipi mbichi au ipi mbivu.
 
Wakuu nilieleza hii issue ya hizi noti kabla hata hazijaingia kwenye mzunguko kuwa ni kimeo, watu wakanishambulia hapa jukwaani sana na kusema sijui technolojia ya kisasa. Mmesahau kujaribu kuchana kidogo mwone nini kitatokea.

Mkuu Nguli Jabali,

Hatukushambulia juu ya ubora wa rangi za noti, tulijadili suala la ATMs; kwanini noti mpya zisipite kwenye macshine hizo mpaka zifanyiwe marekebisho na tukabaini kuwa kuna kamchezo pale maana kama zimechapwa na watu makini na wanasema ziko katika size ya US dollars kwanini basi zikatae kupita kwenye ATMs....
 
mmh hii issue imeniacha mdogo wazi! Halijaisha la Dowans, limekuja lingine. Nafikiri JK anahitaji maombi ili aweze kuvuka hivi vikwazo la sivyo 2015 hatofika!
 
Haki ya nani,hii nchi iko kazi.Ufisadi kila kona..Rais Kikwete kila siku unaingizwa mkenge.Umejiongezea historia ya kuwa Rais aliyedanganywa mara nyingi kuliko marais wote hapa Tanzania. Unadanganywa mpaka kwenye noti..Hii ni aibu nyingine ya taifa.
 
Yani haiitaji mtu awe ameelimika kujua hili,hata kwenye markets vs offices watu wanasema the same thing!.oh!Tanzania.
 
Kama rais ni msanii na wasaidizi aliowachagua wanamsaidia kuendeleza usanii kwa ari mpya..nguvu mpya na kasi zaidi mnategemea nini zaidi ya muendelezo wa usanii kutoka mmoja kwenda mwingine!?Kwenye usanii ndipo tulipopiga hatua!

Tatizo ni kwamba kile chuo cha sanaa kiko Bagamoyo!!! Kazi kweli kweli!!!
 
MH!, Mi ja na nilitafuta kweli chanzo cha rangi nyekundu kwenye shati langu sikupata... mpaka nikagombana na mama watoto wangu kwamba hakulifua vizuri...Sasa nakumbuka kwamba niliweke noti ya sh.10,000 kwenye mfuko halafu manyunyu ya mvua yakanilowesha kidogo. Jamani, hivi Wa- Tanzania tumelaaniwa? Mbona kila kitu hakiendi?
 
Huu ni ukatuni kwa mhusika.
How dare you produce Currencies of that Nature?
How many hands does a currency pass in a day? This is the simplest question the concerned could have asked/axed Himself!!
Do you mean the currencies are brought into circulation After just an Eye looking Prove/Test?
This is really Tanzania!!!
 
Alafu zinachoka haraka sana, juzi nilishika noti mpya ya alfu tano yani nikama imekua kwenye mzunguko kwa mwaka mmoja, kumbe hata mwezi hazina
 
Mkuu Nguli, nasikia zinachanika kirahisi sana pia; nini kifanyike sasa? Serikali izuie mzunguko wa noti hizi mapema?

Hivi hakuna testing kabla ya kupeleka kwenye mzunguko? Wanadhani watanzania ni vilaza kutoangalia ubora wa kitu walicholetewa na wamekilipia hela nyingi kufikia kinaingizwa sokoni?

Nani wanatakiwa kubebeshwa lawama hizi? BoT? Hazina? Serikali kuu?

Bongo tambarare!

Serikali kuu na BOT ndio wanaoingia tender na mchapaji wa fedha hizi. naamini kabisa hizi fedha mpya kama zisipositishwa kwenye mzunguko basi after 3 years lazma tubadili tena haya makaratasi. Au serikali iwe inachapisha noti mpya kila after 3 months ku replace hizo mbovu

Nadhani huo ulikuwa ni utabiri tu na wala si utafiti wa kisayansi

Nitake radhi hunijui wala hujui kazi yangu ni nn sasa utaniitaje mtabiri?
 
Wandugu,

Tumepigwa tena kwa style tofauti.... Tumepiga kelele wee kwenye issue ya Dowans tumesahau kuziba mianya mingine... Watu wanarudisha gharama zao za uchaguzi.. Ndio zimeshachapishwa, makontena kwa makontena na waliochapishwa wameshalipwa.

Baadaye utasikia itabidi zirudiwe, unajua nini hapo " invoice nyingine''.... Mkianza kuhangaika na issue ya noti mpya, watu wanauza Dowans, kampuni nyingine wanalipwa wanasepa.... Yaani jamaa wamejipanga kila mahali hatuna pa kutokea...

Tatizo lipo moja tuu hakuna kuwajibishana kwa sheria.... Tungeweza kumuazima Kagame kwa muda tungeona yatakayotokea....

Mungu ibariki Tanzania
 
Tumeingizwa town!!!!!!
Yaani baada ya miezi sita noti zote zitakua nyeupe, hatutajua ipi ni ipi.
Kaaaazi kweli kweli, kila siku jipya TZ yetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom