Noti mpya hazina ubora?

Unashangaa nini wakati umesikia kuna mwingine aliagiza mashine zaidi za kuharibu noti. Na bado endeleeni kuichagua ccm ambayo ni wezi na wanashindwa kusimamia wezi kwani wakiwabana na wao watokosa hela. Hushangai majengo marefu yanaibuka kwenye miji mikubwa nchini na wenyewe hawajulikani vizuri.
 
Hivi JK tutamkumbuka kwa lipi jema? Mkulo na gavana walizisifia sana hizi matangazo kwenye tv zote, ze komedi na wakawasaidia kutangaza la kumbe ni kimeo kupita kiasi.
 
wanokubali hoja waseme ndiooooo na wanao wote kataa waseme sioooooooooo bunge letu bwana
 
Nchi ya madili bila kubadili uongozi huu(ccm) tusitegemee chochote wataendelea kufanya mambo below standard hadi nchi itacollapse.
 
Noti za Zamani ni bora zaidi ukilinganisha na za sasa, lakini licha ya Ubovu wa Noti za sasa, Watanzania tuwe na hulka za kutunza fedha yetu, wengine wanazikunja na hata kuzifinyanga kama tonge la Ugali. Tuwe wastaarabu.
 
yaaani haya manoti kila nikiyaona nasikia kichefuchefu kinachonikela zaidi ni pale tunapofanywa majuha kila tunapolalamikia juu ya ubora wa minoti hii utasikia yanakuja kutueleza hoo teknologia iliyotumika ni ya kisasa na ya juu kuna nini hapo just pieces of rubbish hivyo hakina mkulo hayaoni aibu kutetea mchemsho huo? kwanini msikiri mmechemka? acheni noti za zamani ziendelee na mkome kutetea minoti yenu mipya eboo!
 
Hivi JK tutamkumbuka kwa lipi jema? Mkulo na gavana walizisifia sana hizi matangazo kwenye tv zote, ze komedi na wakawasaidia kutangaza la kumbe ni kimeo kupita kiasi.

Alishasema kwamba wamkumbuke kwamba aliwatoa hapa akawapeleka pale basi
 
Mpya Ni za kichina.....pesa Za kichina......INJI ya kichina........INJI ishauzwa hii!! Bora noti za Mkapa zilikuaga za ukweli na ndo mpya.
 
Hizi noti hazina muda mrefu kwenye mzunguko lakini cha ajabu ni kwamba leo hii kuna noti mpya ambazo zimechoka kiasi kwamba unashidwa kuamini kama ni noti mpya....noti hizi zinachomoka sana ule mkanda wa mng'ao ...kwani point ya kubadili noti hizi ilikuwa nini kama zina mapungufu makubwa kuliko zilizokuwepo....nani alisimamia hii tenda zima ya utengenezaji wa noti mpya...anawajibikaje kama noti zikionesha mapungufu makubwa kiasi hichi kwa kipindi kifupi namna hii...///natoa hoja////

Kamuulize MKULO, si ni ndugu yako mnatoka naye Morogoro!
 
aliyedizaini hiz noti mpya cjui alikuwa mgonjwa kuhara,maana alikuwa yuko fasta ili acje kujharishia alikuwa anakmbilia choon kuhara hahahaaa bure kabisa!
 
GreatThinkers,
Noti gani hizi nimeweka mfukoni zinachuja na kutoa rangi?
Huwezi amini kale ka uzi kananyofoka na kuacha matundu noti ya sh. 500 ikiwa lainiiiiiiiiii kama inaogeshwa.
Hivi ni nani aliye idhinisha malipo hayo ya noti feki na kutuingiza ktk hasara????

Nina hakika Rais ajaye Lazima atazipiga chini mapema na tutamsahau very Soon Mku"lo" na Ndu"lu"
 
BOT sasa watatoa sarafu ya shilingi 500
 
Mi nlishasema... nchi gani nyingine inatumia noti aina mbili?
Kulikuwa na mantic gani kutengeneza noti mpya na kuziacha za zaman?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom