Makanjanja watawaibia sana babu zetu wauza mahindi kibaigwa ,korosho mtwara na wale wafugaji kwenye minada huko MaswaSi unajua wabongo lazima wajaribu kitu kipya, tena na hivi walivyokuwa wanajigamba kuwa hauwezi kutoa noti feki kwenye hizi mpya ngoja uje uone mziki wake
Lakini si tuliambiwa kuwa make-up ya notes mpya ni sawa na US $? Jamani, Tanzania! TAnzania nani alikuroga?
Makanjanja watawaibia sana babu zetu wauza mahindi kibaigwa ,korosho mtwara na wale wafugaji kwenye minada huko Maswa
Subirini tuibiwe tu! :disapointed:
Mkuu tumeisha pigwa changa la macho, hii ni kashfa nyingine imekuja. Kwani ni sababu gani za msingi zilizofanya wabadili noti za awali? Nahisi ulikuwa ni mradi wa kujipatia 10%Mkuu Nguli, nasikia zinachanika kirahisi sana pia; nini kifanyike sasa? Serikali izuie mzunguko wa noti hizi mapema?
Hivi hakuna testing kabla ya kupeleka kwenye mzunguko? Wanadhani watanzania ni vilaza kutoangalia ubora wa kitu walicholetewa na wamekilipia hela nyingi kufikia kinaingizwa sokoni?
Nani wanatakiwa kubebeshwa lawama hizi? BoT? Hazina? Serikali kuu?
Bongo tambarare!
Nadhani huo ulikuwa ni utabiri tu na wala si utafiti wa kisayansiWakuu nilieleza hii issue ya hizi noti kabla hata hazijaingia kwenye mzunguko kuwa ni kimeo, watu wakanishambulia hapa jukwaani sana na kusema sijui technolojia ya kisasa. Mmesahau kujaribu kuchana kidogo mwone nini kitatokea.
………………kashfa ya kuanguka kwa benki ya meridien biao haikukuwa kashfa pekee kwa dr rashid akiwa gavana wa benki kuu. Mwishoni mwa mwaka 1994, rais mwinyi alifanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri kwa kumteua jakaya kikwete kuwa waziri wa fedha, na kumuondoa kigoma malima (sasa marehemu). Mchakato mzima wa ufilisi wa meridien biao kwenda kwa benki nyingine ya kigeni – stanbic bank ulifanywa chini ya usimamizi wa kikwete na dr rashid na inasemekana haukuwa wa wazi kabisa. Kulitokea minon'gono kwamba milungula ilitembea.
Pili, wakati akiwa bado gavana wa benki kuu, dr rashid alishinikiza serikali kubadilisha kampuni ya uchapaji wa noti zetu kutoka kampuni ya zamani ya uingereza ya thomas de la rue na kuingia mkataba na kampuni ya giesecke & devrient ya ujerumani. Kampuni hiyo ya uingereza imefanya biashara na benki kuu ya tanzania kuanzia 1966 hadi 1996. Sababu za kubadilisha kampuni ya uchapaji wa sarafu hazikuwekwa sawa kwani wengi wanaona kuwa hii ya ujerumani inachapa noti zisizo na ubora kama ilivyokuwa zamani, zinachakaa haraka sana.
Mapungufu haya, pamoja na ripoti katika gazeti la the east african la agosti 13, 2001, kwamba mapema mwaka huo, 2001 benki kuu ililazimika kuziondoa katika mzunguko mamilioni ya noti za sh 1,000/- kutokana na kuchapishwa vibaya na mchapishaji huyo, bado dr rashid aliendelea kuishinikiza serikali kufanya biashara na kampuni hiyo ya ujerumani. Katika mwaka 1994 pekee, kampuni hiyo ilichapisha vibaya noti za tanzania mara nne. Hizi ni zile za viwango vya sh 500/-, 1,000/- na 10,000/-.
Aidha gazeti hilo liliripoti kwamba kampuni hiyo ya ujerumani pia ilikuwa imekataliwa kuchapisha noti za benki ya umoja wa ulaya (european central bank) baada ya kuchapa vibaya noti za euro za thamani ya mabilioni katika tenda iliyokuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 32.
Ilielezwa kuwa katika zabuni hiyo ya mwaka 2001, wakati kampuni ya thomas de la rue ilikubali kuchapisha noti zetu kwa thamani ya dola za kimarekani 33.02 milioni, kampuni hiyo ya ujerumani ilitaka ilipwe dola 49.15 milioni. Hata hivyo hatimaye wajerumani walishinda kunyakuwa zabuni hiyo.
chanzo mwanahalisi
Nasikia kwa mbali ngurumo ya dhoruba kubwa inayokuja. My instincts tell me kwamba hii itaifanya Dowans kuwa cha mtoto! Ngojeni tu!!!!!!!
Namimi nimesugua, rangi kwa kwenda mbele! Haya cha juu kulipia madeni ya helcopta za kampeni
Si unaona anazishangaa atakumbuka kuzisugua saa ngapi