Ushauri wenu kwenye hili ndugu zangu

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,930
Mimi ni kijana nimemaliza chuo kikuu miaka kadhaa imepita sasa, Umri wangu ni miaka 31 (sina mke wala mtoto), baada ya kuangaika sana kutafuta ajira mpaka kufikia kukata tamaa atimaye Mungu wa mbinguni, muumba mbingu na nchi akaniona na kunipatia kisehemu kidogo cha kujishikiza (project flani hivi),

Tangu nianze kufanya kazi nina miaka 3 sasa, na kila pesa niliokuwa napata nilikuwa najitahidi kadri ya uwezo wangu ku-save kadri niwezavyo maana nilikuwa nikifikilia kipindi sina ajira nimepitia kwenye moto mkali sana wa mawazo na kukosa pesa ata ya kupeleka CV sehemu.

Kwa sasa bado nipo kwenye ajira hii (project) na hii project inaelekea kuisha ndani ya miezi minne kutoka ivi sasa, na nimejaribu kutuma sana CV kuomba sehemu mbalimbali ila sijapata mrejesho wowote tangu mwaka jana, na kwenye hii project mpaka sasa nime-bahatika ku-save jumla ya kiasi cha shillingi milion 40.

Sijawahi kufanya biashara popote pale katika maisha yangu, na katika kazi zangu izi katika hii kampuni zinabana sana muda wangu kufanya kazi zingine binafsi.

Natamani sana nipate kazi sehemu nyingine baada ya hii kuisha, ila ndio ivyo nimejaribu sana kutuma CV mpaka sasa sijapata ata interview moja ya kuitwa,

Natamani pia labda ningeanzisha biashara ila sijawai kufanya biashara yoyote,

Kuna muda nawaza basi ngoja nitumie hii pesa kujenga tu nyumba maana sina nyumba, (ila kiwanja ninacho tayari),

Kuna muda nawaza sijui niitumie hii pesa kununua nyumba badala ya kujenga.

Kuna muda nawaza nitafute chuo nje ya nchi (nchi za ulaya tu mf, norway au ujerumani) course yeyote ya mwaka mmoja, mfano: postgraduate diploma nisome, ila hapa nia na madhumuni yangu makuu ni kutafuta ajira yeyote halali nje ya nchi ili niweze ku-save ela nyingi zaidi kwaajili ya kufanya maendelea yangu uku nyumbani tanzania.

Nipo kwenye msongo wa mawazo sana, msaada wenu wa ushauri ndugu zangu wana JmaiiForum
 
Mimi cha kukushauri fanya vyote na iyo pesa ila usijaribu kujenga nyumba. Tumia pesa yako kuzalisha kuzalisha zaidi. Ikifika wakati utajenga.

Mwisho gawa pesa iyo mara 3. Then tumia 1 kati ya mgawanyiko wa 3 kufanyia biashara, mbili ya kilichobaki subiri kupima mwendo wa biashara yako uliyoanza kuifanya.

Hint. Popote utakapojitambulisha unataka kufanya jambo la pesa useme kiasi kichache zaidi mfano 10m ndio huko nayo. Bila hivyo mapema tuu tunakupiga
 
Nakushauri usitumie hiyo hela kufanya biashara yoyote kwasasa. Na hata ukiamua kuitumia usifanye kitu kingine chochote isipokuwa kujenga. Ila kwasasa wala usiitumie kujenga hadi utakapopata kazi ya uhakika. Kwanini nasema hivi?

Ukiitumia hiyo hela kwenye biashara unaweza kukwama moja kwa moja kimaisha na hakuna jambo baya kama hili!

Ni mbaya mno kwani utakosa hata hela ya kutuma application au kuishi na utakwama kabisa. Endelea kutuma maombi ya kazi na kumweka Mungu mbele. Hofu au stress isikufanye ufanye maamuzi mabaya, kwasasa usifanye kingine isipokuwa kufanya applications hata kama itakuchukua miaka 2 kupata kazi hiyo ni kawaida siku hizi.
 
Mimi cha kukushauri fanya vyote na iyo pesa ila usijaribu kujenga nyumba. Tumia pesa yako kuzalisha kuzalisha zaidi. Ikifika wakati utajenga.

Mwisho gawa pesa iyo mara 3. Then tumia 1 kati ya mgawanyiko wa 3 kufanyia biashara, mbili ya kilichobaki subiri kupima mwendo wa biashara yako uliyoanza kuifanya.

Hint. Popote utakapojitambulisha unataka kufanya jambo la pesa useme kiasi kichache zaidi mfano 10m ndio huko nayo. Bila hivyo mapema tuu tunakupiga
Usiguse hiyo hela hata kidogo tafuta kazi kwanza!
 
Mimi cha kukushauri fanya vyote na iyo pesa ila usijaribu kujenga nyumba. Tumia pesa yako kuzalisha kuzalisha zaidi. Ikifika wakati utajenga.

Mwisho gawa pesa iyo mara 3. Then tumia 1 kati ya mgawanyiko wa 3 kufanyia biashara, mbili ya kilichobaki subiri kupima mwendo wa biashara yako uliyoanza kuifanya.

Hint. Popote utakapojitambulisha unataka kufanya jambo la pesa useme kiasi kichache zaidi mfano 10m ndio huko nayo. Bila hivyo mapema tuu tunakupiga
Asante kwa ushauri wako, nimeupokea
 
Chukuwa milioni 20 weka sokoni

Biashara za mazao....
Au ingia china chukuwa mavitu peleka mashuleni kila mwezi unakusanya mkwanja ila uwe na kibali tu.
Asante kwa ushauri wako, nimeupokea
 
Mimi ni kijana nimemaliza chuo kikuu miaka kadhaa imepita sasa, Umri wangu ni miaka 31 (sina mke wala mtoto), baada ya kuangaika sana kutafuta ajira mpaka kufikia kukata tamaa atimaye Mungu wa mbinguni, muumba mbingu na nchi akaniona na kunipatia kisehemu kidogo cha kujishikiza (project flani hivi),
Achana na nyumba mkuu utapata stress tu coz nyumba standard itatafuna hela yote hiyo na wewe utakosa Cha kufanya badae utajolaumu tu... Ni Bora chukua 10M kufungua biashara hata kuuza nafaka ila komaa usikubali kushindwa then utapata mwelekeo ... Ujenzi unakula hela broo
 
Jenga nyumba hata ya 25m,utakusaidia pale pesa itakapoisha angalau utakua na mahala pa kulala. Hakuna kitu kibaya kama uwe huna kazi,huna pesa na hata pahala pa kulala iwe changamoto.

Hiyo 15m itakayobaki,fanya biashara ya 9m na 6m weka kama reserve,then ndipo utafute kazi nyingine ya kufanya.
Nasisitiza nyumba kwasababu ukiwa na kwako hata ukienda kazini na ukafudi na buku 5 hautokua na pressure sawa na yule ambae anafanya kazi huku akiwaza kodi,.nk
 
Biashara si kitu cha kuogopa, everything is risky, hata kukaa na hela nyingi hivo na huna kazi ni risky. Utaitumia tu. Fungua biashara, hiyo hela kama ni mtu wa mzunguko mkubwa wa hela hata kkoo unaweza fungua duka lako la nguo, ukajianzisha taratibu, mtaani eneo lenye mzunguko as well. Kujenga nyumba inawezekana pia. Ila lazma hiyo hela iingie kwenye mzunguko mpya, utulivu hela haipoteagi tu kama unafanya jambo zuri kwa njia nzuri.
 
Nunua haice endesha mwenyewe mpaka hapo utakapopata kazi.
Usonunue used bongo bora utumie 28 milioni uvute yard.
 
Mimi ni kijana nimemaliza chuo kikuu miaka kadhaa imepita sasa, Umri wangu ni miaka 31 (sina mke wala mtoto), baada ya kuangaika sana kutafuta ajira mpaka kufikia kukata tamaa atimaye Mungu wa mbinguni, muumba mbingu na nchi akaniona na kunipatia kisehemu kidogo cha kujishikiza (project flani hivi),
Fungua pharmacy hutajuta kabisa kuna sehemu wanakoepesha mpka dawa utakuwa unalipa kidogo kidogo
 
Upo mkoa gani?
Ukisha jibu hili swali ndipo itakua rahisi kukushauri kutokana na mkoa ama wilaya uliyopo.
Lakini pia kwaharaka nilicho kiona kwako wewe sio mfanya biashara kwasababu hadi hapo ulipo ungekua tayari umesha anza kupata walau wazo la biashara kadhaa (watu wa hivi wapo). Lakini pia hii haikufanyi usijifunze kufanya biashara sababu Mungu alimpa binadam maarifa ya kujifunza, lakini wasiwasi wangu ni kwamba kama hiyo pesa ndio akiba yako pekee... kwanini utake risk kujifunzia biashara?? (Ulipaswa ujifunze biashara wakati mshahara unaendelea kuingia).
Hivyo basi, kwanza nakushauri ujenge nyumba ndogo ya room moja, bebule, choo/bafu na jiko. Hii naamini ukiisimamia mwenyewe haitizidi 25 millions.
Baada ya hapo endelea kutafuta kazi huku ukiweka hata genge la matunda, nyanya, vitunguu, mboga hapo maeneo ya utakapo jenga nyumba yako.
Kaa kwenye kijiwe chako kipya ambacho walau utatumia sio zaidi ya 2 milions kukijenga kwa mabanzi pamoja na mtaji na kisha pesa iliyo baki fanya kuitunza bank.
Baada ya hapo endelea kutafuta kazi online wakati tayari unauhakika wa kipato kidogo cha kukuwezesha kujikimu kwa chakula na mambo madogo madogo.
Ukilifanya hili ninaamini utafanikiwa na kazi nyingine utaipata kwasababu hapo toka itakua nikama umepata experience
 
Biashara si kitu cha kuogopa, everything is risky, hata kukaa na hela nyingi hivo na huna kazi ni risky. Utaitumia tu. Fungua biashara, hiyo hela kama ni mtu wa mzunguko mkubwa wa hela hata kkoo unaweza fungua duka lako la nguo, ukajianzisha taratibu, mtaani eneo lenye mzunguko as well. Kujenga nyumba inawezekana pia. Ila lazma hiyo hela iingie kwenye mzunguko mpya, utulivu hela haipoteagi tu kama unafanya jambo zuri kwa njia nzuri.
shukrani sana ndugu yangu kwa ushauri wako, nimeupokea
 
Back
Top Bottom