No choo no ndoa - India

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
Kwa waliosikiaa asbh BBC

waziri wa maendeleo ya jamii wa india ameshauri familia zenye watoto wa kike popote walipo ikitokea anaolewa ameshauri bwanaharusi kuhakikisha anajenga choo kwanza kwenye nyumba ya wakwe na hii ni kwa sababu nyumba nyingi azina vyoo na wengi hutegemea vyoo vya mitaani ambavyo ni vingi kuliko majumban...mh ameomba sana hilo kuzingatia ili kuweza kuboresha afya ya wa hindi popote pale walipo india so wazazi sio tu mnakubali kienyeji ngombe watengeneze choo aisee hii ingekuwa dar ,,mpaka raha
 
Duh! Hii mambo ya public toilet inanikumbusha mbali saaaana,Mnajikuta mmeunga foleni kama watu 8 hivina ukitoka kwenye foleni unaweka jiwe ili usipitwe.Kweli utoto raha jamani.
 
Kumbe muhindi wewe eeh?
Barbara cheee
Duh! Hii mambo ya public toilet inanikumbusha mbali saaaana,Mnajikuta mmeunga foleni kama watu 8 hivina ukitoka kwenye foleni unaweka jiwe ili usipitwe.Kweli utoto raha jamani.
 
Hapa bongo mtu akitaka kuoa wazazi wa binti wanaangalia zaidi kama mkwe wao ana maisha mazuri yatakayomfanya binti yao aende kuishi kwa amani na furaha, ikiwa ni pamoja kuwa na nyumba, kausafiri, biashara au kazi nzuri inayolipa n.k. Hii ni tofauti kwa wenzetu wahindi.

Katika hali inayoonyesha kwamba serikali imechoshwa na hali ya uchafu, imewataka wazazi wenye mabinti kuwekka sharti la kujengewa choo kabla ya binti yao kuolewa. Taarifa zaidi zinaeleza watu wengi wanamiliki simu za mkononi lakini wakati majumbani mwao hawana vyoo.

Taarifa hiyo inaendelea kusema kwamba katika sensa ya 2011 inaonyesha 75% ya wananchi bilioni 1.2 wa india wanamiliki simu za mkononi kati ya hao 50% tu ndio wenye vyoo na waliounganishwa katika mtandao wa maji taka ni 11%.

Hivyo kutokana na hali hii wazazi wametahadharishwa kuchunguza kwanza kama bwana arusi ana choo nyumbani kwake kabla hawajafikia uamuzi wa kumwoza binti yao.

Hayo ni ya India, hapa kwetu hali ikoje? Maana sio ajabu bwana arusi akiwa ukweni akageuka nyuma ya ukuta akauachia..................... Karibuni.
 
Back
Top Bottom