Njombe: Wananchi washauriwa kutumia baridi kama Utalii wa ndani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Kiongozi mmoja sijamkata jina na cheo huko Njombe ameongea (nimemuona kwenye taarifa ya habari ITV) akiwashauri wananchi kutumia baridi kama kivutio cha utalii wa ndani.

Baridi linaloendelea limetajwa kuathiri afya za watu na mazao. Nimonia kwa watu na ukungu kwa mazao ni kati ya magonjwa yaliyotajwa
 
Wakazi wa mkoa wa Njombe wamesema hawajawahi kuishuhudia baridi kali kama hii ya mwaka huu

Wakazi wa mkoa huo wamepunguza muda wa kufanya kazi wakihofia kupatwa na Maradhi

Naye Mkuu wa Mkoa huo mh Kindamba amesema Baridi hiyo ni fursa kwa mkoa huo kutangaza Utalii wa ndani na kuwaalika watu kufanya Utalii wa Baridi ili kuongeza mapato ya Serikali

Chanzo: ITV habari
 
Sijawahi kufika Njombe ila Kuna kipindi nilienda arusha, sasa usiku ukafika nikalala palepale stendi maana mfuko ulikuwa umekaa kushoto.
Nilijifariji kwa kudhani hali ya hewa ni kama nitokapo.
Sikujua lolote.
Aise siku ile nilipigwa na baridi kidogo nife.
Ilibidi tu niwe mpole na niombe nguo ya kuvaa kwa juu maana kidogo nifie pale pale stendi.
 
Hivi hawa viongozi wanajielewa kweli? Kuna utalii wa baridi yani kabisa nitoke dar nikapigwe na baridi kwa kisingizio cha utalii? ... wazungu wenyewe kipindi cha baridi wana kuja badhi ya nchi za afrika kukwepa baridi ...kama taifa tuna safari ndefu sana
 
Pole sana kaka.
 
Hata hapa Mbalamaziwa kwa kweli hali ni tete
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…