Njombe: Zaidi ya 30% ya Wakazi wa Vijijini wana Ugonjwa wa Usubi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1678179449192.png

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Dk. Isaya Mwasubila amesema Tafiti zimebaini Maambukizi makubwa katika maeneo 4 ambayo ni Itipula ina 30%, Igola 11.22%, Mji Mwema 5.68% na Mamongolo 4%.

Kutokana na hilo, Wizara ya Afya imeanza kampeni ya kutoa Dawa ili Kuwakinga Wananchi ambao hawajapata Ugnjwa na kutoa Tiba kwa walioathirika na Ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Usubi unapatikana kwenye maeneo yenye Vyanzo vya Maji yaendayo kasi ambapo kwa mujibu wa Takwimu za Mwaka 2022, Halmashauri 29 Nchini zilikuwa na Maambukizi huku 7.02% ya watu wakiwa hatarini kuambukizwa.

=================

ZAIDI ya asilimia 30 ya baadhi ya wananchi waishio maeneo ya vijijini wamegundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa usubi unaosababishwa na minyoo inayotoka kwenye nzi weusi wanaopatikana kwenye maporomoko ya mito.

Hayo ameyasema wakati wa uzinduzi wa kampeni ya unyeshwaji wa dawa kwa ajili ya kinga tiba dhidi ya ugonjwa wa usubi uliofanyika Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Kissa Kasongwa amesema kulingana na utafiti uliofanyika moja ya maeneo yalioathirika na ugonjwa wa usubi kwa zaidi ya kiwango cha kawaida ni Wilaya ya Njombe hasa katika Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Amesema kutokana na hali hiyo serikali kupitia wizara ya afya imeleta mpango wa kumeza dawa ambazo zitakwenda kuzuia na kutibu ugonjwa wa usubi.

"Ugonjwa huu una dalili mbalimbali kama ngozi kupauka, ngozi kutoka mabaka mabaka, Muwasho na ngozi kuchakaa kwenye macho lakini dawa hizi zinasaidia watu wenye upele, chawa na mapunye pia" amesema Kasongwa.

Amesema lipo tatizo kwa watanzania wanapoambiwa kitu wanadharau na kutaka kuona kwanza madhara lakini ugonjwa wa Usubi upo na umeathiri watu wengi.

Mratibu programu ya kudhibiti ugonjwa wa usubi kutoka Wizara ya Afya Dk. Clara Mwansesu amesema ugonjwa wa usubi unapatikana kwenye maeneo ya vyanzo vya maji ambayo yanayoenda kwa kasi ambapo baadhi ya vijiji vya Halmashauri ya Mji wa Njombe vimeonyesha kuwa viashiria vya ugonjwa huo.

"Wizara tulifanya utafiti mwaka jana tuligundua maambukizi yako juu ambapo baadhi ya vijiji kulikuwa na maambukizi zaidi ya asilimia 30 hivyo basi serikali kupitia Wizara ya Afya tumeamua kuanzisha umezeshaji wa dawa za kinga tiba katika halmashauri ya Mji wa Njombe ili kuweza kuwakinga wananchi walioathirika kupata tiba na wale ambao hawajapata madhara waweze kukingwa" amesema Dk. Mwansesu.

Amesema kwa awamu hii zoezi hilo linafanyika katika halmashauri 14 hapa nchini ingawa mara nyingi hufanya katika halmashauri 29 ambazo zimeathirika na ugonjwa huo.

Amesema kwa Mkoa wa Njombe ni Halmashauri ya Mji wa Njombe linafanyika zoezi hili, Morogoro linafanyika kwenye halmashauri tisa na halmashauri zingine tano kutoka Mkoa wa Tanga.

Katibu Tawala Wilaya ya Njombe Emmanuel George amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha wananchi hawaugui na wanakuwa salama ndiyo sababu iliyopelekea kuletwa kwa dawa tiba hizo.

"Kuna watu hapa Njombe wameshaugua lakini wengi hatukujua shida ni nini kumbe shida ilikuwa ni Usubi," amesema George.

Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe Dk. Isaya Mwasubila amesema tafiti zilizofanyika zilibaini masmbukizi makubwa katika maeneo manne ndani ya halmashauri ya mji wa Njombe ambayo ni Itipula asilimia 30, Igola asilimia 11.22, Mji Mwema asilimia 5.68 na Mamongolo asilimia 4.

"Kulingana na ukubwa wa tatizo tunatakiwa kunywa kinga tiba mara mbili kwa mwaka nyumba kwa nyumba kwa kutumia wagawa dawa ngazi ya jamii ili kuepuka ulemavu wa kudumu na umasikini"amesema Mwasubila.

NIPASHE
 
usubi huku kwetu ni vijidudu vidogo vidogo jamii ya sisimizi vinakutembea mwilini na wanang'ata hasa kipindi cha joto kali, usiombe wakawa kitandani
 
usubi huku kwetu ni vijidudu vidogo vidogo jamii ya sisimizi vinakutembea mwilini na wanang'ata hasa kipindi cha joto kali, usiombe wakawa kitandani
Huku nilipo Usubi ni Panga butu.

Angeweka jina la kitaalam.
 
Kichwa cha habari kinapotosha, sio 30% wa vijijini, ni 30% ya hicho kijiji cha itipula. Na ukifanya kwa wastani wa vijiji hivyo vilivyotajwa ni kama 10%, ila kwa vijiji vyote vya Njombe pengine havifiki hata 2%
 
Back
Top Bottom