SoC02 Wizara ya Maliasili na Utalii iliangalie hili katika kuchochea utalii wa ndani nchini

Stories of Change - 2022 Competition

politicians

Senior Member
Apr 8, 2018
154
124
Utangulizi: Awali ya yote napenda kutumia fursa hii kumpongeza "Mh: samia suluhu hassan, raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania" kwa kuonyesha upendo na mahaba makubwa kwenye sekta ya utalli nchini, kwa kuamua kwa dhati kucheza filamu ya "The Royal Tour" kwa lengo la kuhamasisha watalii waje kutembelea vivutio vyetu hapa nchini.

Kwa kweli ametuwakilisha vyema na ametuheshimisha kama taifa, kwa kupitia filamu hii vivutio vyetu vimeweza kujulikana zaidi duniani na kuvutia watalii wengi kuja nchini.

Pili napenda kuipongeza wizara ya malisali na utalii kwa kujitahidi kukuza sekta hii kwa kiwango kikubwa lakini pamoja na mafanikio hayo waliyonayo bado wanakazi kubwa sana ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wananchi ili uweze kuongeza mapato zaidi kwa serikali.

Mimi kama raia mzalendo na ushauri wangu naimani unaweza ukaleta uchochezi kwa watanzaniaia kupenda kutembelea vivutio vyetu nchini,ushauri wangu umejikita katika swala moja lakini litakalogusia mambo ma nne kama ifuatavyo.

wanyamapori: Asilimia kubwa ya Watanzania wengi wamezaliwa vijijini, hivyo basi wengi wao katika kukua kwao waliweza kuwaona wanyamapori mbalimbali kama vile simba, tembo, fisi, kiboko n.k na wengine wana waona mpaka sasa bila kutoa hata mia.

Kuna baadhi ya barabara ukipita ukiwa unasafiri utawaona wanyama mbalimbali wakikatiza barabarani na kuna baadhi ya mikoa pia wanyama hao huvamia makazi ya watu.

Hivyo basi ni vigumu kumshawishi Mtanzania wa kawaida kutembelea vivutio vya utalii nchini akawaone wanyama walewale aliowazoea kuwaona au anao waona mara kwa mara, utalii ni biashara hivyo panahitajika mkakati mpya wa kimasoko kuhamasisha watu kupenda kutalii kama wanavyopenda michezo kama mpira wa miguu n.k.

Bila kupoteza muda ngoja nijikite kwenye hoja yangu katika kuchochea utalii huu wa wanyama pori, kwa nini serikali isiangalie uwezekano wa kuleta wanyama wengine wageni kutoka nchi zingine iwe kwa kuwanunua, kuwakodisha au kufanya mabadlishano ya wanyama ya mda mfupi na badae kuwarudisha nchini kwao halafu wanakuwa wamewajengea sehemu fulani kama bustani ya wanyama.

Ili mradi mtu ukimtangazia aje atembelee aone wanyama na ukamtajia pia kutakuwepo na wanyama wageni kutoka nchi za nje waje waone nadhani hili inaweza ikaleta hamasa zaidi ya watu kuja.

Halafu kitu kingine wao mbona wanachukua wanyama wetu kutoka nchi za afrika kupeleka kwao kwani sisi tunashindwa nini kuchukua wa kwao kuwaleta kwetu?

Ili kutia hamasa tu kwa wananchi kupenda utalii, nadhani wataalamu wa sekta husika wanaweza wakaona nina mna gani hili wazo linaweza kutekeleza kama lita wafaa kimasoko,kwa mfano hebu tazama wanyama hapo chini hivi wakija tanzania watu si wanaweza kushawishika kuwaona.

white tiger.jpg

chui weupe(white tiger)wanapatikana
sana nchini india chanzo (Medium – Where good ideas find you.)

giant panda.JPG

anajulikana kama (giant panda)anapatikana sana maeneo ya nchini china,chanzo(Giant panda - Wikipedia).

Hawa ni baadhi tu ya wanyama wanaopatikana nchi mbalimbali,ila kuna wanyama wengi sana ambao.

wapo nchi za nje ila hapa tanzania hawapo tunaweza tukawaleta kwa lengo la kuhamasisha watu kupenda
kutalii.

Ndege: Kama nilivyoeleza hapo awali kwa upande wa wanyama pori hapo juu na ndege pia hoja yangu ni ile ile kwa mfano ndege kama hawa hapa wakiletwa tanzania watu watahamasika kwenda kuwaangalia.

keel-billed toucan.png

Anaitwa (keel -billed toucan)anapatikana huko latin america
chanzo cha picha( The Teal Mango | Anything But Traditional)

purple gallinule.png

Anaitwa (purple gallinule)anapatikana sana marekani,mexico na argetina,chanzo cha picha (The Teal Mango | Anything But Traditional)
mandarin duck.png

anaitwa (mandarin duck)anapatikana china na urusi,chanzo cha picha( The Teal Mango | Anything But Traditional)hawa ni baadhi tu ya ndege ambao hawapitikani hapa nchini ila wapo wengi tu,serikali ikiwaleta
na kuwahifadhi sehemu vizuri watu watahamasika kuja kuwaona tu,

Samaki:nchi yetu bahati nzuri imezungukwa na vyanzo vingi vya maji,binafsi sijajua mpango wa serikali kuhusu.

Utalii wa samaki,tumeshuhudia baadhi ya nchi wakifanya sana utalii wa samaki sio ule wa kuvua samaki tu, bali ni kujenga baadhi ya mabwawa karibu na ufukwe na watu kuja kutazama samaki.

dolphin fish.jpg


Anaitwa samaki(dolphin)anapatikana sana nchini pakistan, india kwa hapa nchini kwetu wanapatikana zanzibar ndio wanaonekana kirahisi lakini bara na uhakika watu wengi hawajawahi kuwaona,chanzo cha picha (dw.com)naamini katika bahari yetu kuna samaki wengi tu watanzania wengi hawajawai kuwaona, kama serikali itajenga mabwawa maalumu kwa ajili ya utalii wa samaki itakuwa vyema sana.


Maeneo ya makumbusho:tuna maeneo ya makumbusho ya makabila,biashara ya utumwa,mashujaa wetu kwa nini serikali isiangalie uwezekano wa kuweka makumbusho ya dini?,kwa sababu historia ya nchi yetu inahusisha pia dini hasa ukristo na uislamu,tunatambua kuwa serikali haina dini kwa mujibu wa katiba ya nchi lakini watu wake wana dini,watu wanatoka hapa nchini wanakwenda nchi za mbali huko izraeli na uarubuni kwenda kujifunza historia ya dini kwa kutalii ni vyema kukawa na makumbosho ya dini, mtu akitaka kujua historia ya dini yoyote iliyopo hapa nchini anakwenda hapo anaelezwa historia ya dini yoyote iliyopo hapa nchini kuanzia ilipoanzia mpaka kufika hapa nchini na serikali itaweza kupata mapato pia.

Hitimisho: Lengo langu la kupendekeza waletwe baadhi ya wanyama,ndege,samaki kutoka nje ya nchi sina maana kwamba wanyama, ndege, samaki wa hapa nchini sio wazuri kuzidi wa huko ulaya sio kweli, wanyama wote ni wazuri, ila lengo ni kutengeneza mazingira ya kuwashawishi watu kupenda utalii, watanzania wanatabia ya kuanza kupenda vya nje kwanza halafu badae wanakuja kupenda vya nyumbani, mifano ipo wazi walianza kupenda mpira,muziki wa nje lakini sasa wameanza kupenda vya ndani, sasa ukifika wakati ukiwambia njooni muone wanyama mbalimbali wa ulaya na asia lazima watakuja tu si wanapenda vya nje ya nchi.

Wakishaanza
kupenda utalii badae watapenda vivutio vyao vya ndani,moja kati ya sababu kubwa iliyonisukuma kuandika nakala hii ni kwa sababu sasa hivi dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali za magonjwa ya mlipuko kama vile "uviko 19", wote tulishudia sekta yetu ya utalii ili vyo yumba baada ya kuanza ugonjwa huo kwa mara ya kwanza.

Hivyo basi kuna umuhimu wa kuimarisha utalii wa ndani kuliko kutegemea utalii wa nje pekee kwa sababu hatujui kesho kutatokea ugonjwa gani tena ni muhimu kujiandaa wakati wote kulinda uchumi
wetu kwa maslahi ya vizazi vyetu vilivyopo na vijavyo kwa sababu uchumi ndio moyo wa taifa.
 
Back
Top Bottom