Njia ya kuongea na mwanamke ipasavyo ili afunguke kukwambia kila kitu

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Ili mwanamke afunguke kwako lazima ajisikie amani na usalama kwako. Wanaume wengi huwa wanawapotezea wanawake zao kwenye kuongea, ndio mana wanawake wao pia huwapotezea kitandani. Sababu mwanamke anaona haujali hisia zake.

Njia hii ya kumfanya mwanamke aongee unaweza kuitumia kwa mama yako, mchumba wako au rafiki yako wa kike. Itakusaidia kujua kilichopo nyuma ya pazia.

Usipoongea na mwanamke ipasavyo atakupa shida na kufanya maisha kuwa magumu kuliko ungekua bachela. Sote tunajua maisha yanavokua magumu pale inapobidi uhangaike na mwanamke ambaye ana uchungu, hasira hasira kila muda na kukupa shida hata salamu.

Lakini mwanamke mwenye furaha anafanya maisha yanakua rahisi na ya furaha, pia unapata urahisi wa kuweka nguvu zako kwenye kazi yako.

Ili kumfanya mwanamke afunguke kwako inabidi ujue kuuliza maswali sahihi na uelewe vitu kwa upande wake.

Unapoongea na mwanamke anaweza kukujaribu kwa kukuambia “Kila kitu kipo sawa/tuachane na hayo tuongee mengine” au maneno yenye maana kwamba yupo sawa. Lakini ukikubiliana naye anakasirika zaidi sababu anaona kama haumjali. Hivyo basi, hata akikuambia hivyo usikubali kirahisi, endelea kumchimba mpaka akuambie kilichopo nyuma ya pazia.

Unaweza kuanza na maswali madogo tu, “Baby siku yako ilikuaje?” Kisha mwache aongee. Kisha mfanye aongee zaidi “Kweli baby? Mhh… wacha bhana… ningependa kusikia zaidi kuhusu… heh, kwaiyo ikawaje? Hii nimejifunza kwa mzee wangu anapoongea na mama, we kazi yako ni kusikiliza na kuuliza maswali.

Akishaongea mengi na unaona ubadilishe mbinu ya kumfanya aongee zaidi, we fanya kurudia alichokisema mfano, anakusema umemsahau, usitake kumshinda ila rudia kitu kilichomfanya ajisikie vibaya, “anha! Kama nimekuelewa vizuri baby umesema jana nlipolala sijakuambia usiku mwema ulijisikia vibaya, eti?

Ebu nambie zaidi ulivojisikia/ulitamani ufanyaje?” Kisha mwache aongee. We usichukulie kama anakusema bali chukulia anaongea kuhusu hisia zake. Unaweza kuona ni utoto/ni jambo la kushangaza lakini kwa mwanamke ni jambo kubwa. Ndo njia hii unaweza mchimba mwanamke kwa lolote na akakuambia zaidi.

Msikilize mpaka atakapomaliza kuelezea hisia zake utaona ana hali ya amani/furaha/tabasamu na anaweza akakuambia “asante kwa kunisikiliza/unanipa amani/saivi najisikia furaha/yani unajua kunifanya niongee,” au chochote chenye kumaanisha kama ivo. Ukifikia hapo ujue amejiachia kwako na atakuona wewe ndo mpenzi wake wa maisha.

Mara nyingi haizidi nusu saa kumsikiliza mwanamke ila inategemea kama huwa unamsikiliza vizuri au huwa unajaribu kushinda kila mazungumzo. Kama unamjali tenga muda kwa ajili yake.

Pia ukiona mwanamke wako hata umpandishe/umtomase vipi kitandani bado ni mkavu chini, basi anza kuongea naye, mfanye afunguke kwako na kukwambia kuna nini kinachondelea kihisia kinachomfanya asijiachie kwako kitandani, na uoneshe kujali hisia zake.

Zingatia;

Katika maelezo hapo juu hakuna sehemu inayosema unatakiwa umshinde mwanamke kwenye mazungumzo, au umtatulie tatizo lake kwa kumpa ushauri na pia utaona hamna mantiki ya kueleweka kumfanya mwanamke aongee, sababu wao wanatumia hisia zaidi sio kama sisi.

Wanawake wanatatua matatizo yao kwa kuongea, akiongea na wewe sio kwamba anaomba ushauri bali anataka umsikilize, hivyo USIMPE ushauri mpaka yeye mwenyewe aombe.

Pia usiwe serious sana au mkali, bali jiachie ona kama unamsikiliza mtoto wa kike unayemjali. Mchombeze pia.
 
Kiasili mwanamke kusikilizwa ni moja ya mahitaji ya msingi sana.

Lakini sio sawa kwa mwanaume kutaka kusikia mwanamke akuambie kila kitu, ila hii isimfanye mwanaume asumsikilize mwanamke.
 
You nailed it mkuu. Ni kweli wanawake wanahitaji kusikilizwa Sana (kujali) na wewe Kama mwanaume unapomsikiliza usiwe "Mr Fixer" yaani mzee wa kutatua Mambo, Ila jifunze Sana kuwa msikilizaji na kumuonyesha kwamba unaelewa jinsi anavyojisikia. Pia wanawake wanapenda kufanyiwa vitu bila kuomba kufanyiwa.

Mfano anaporudi kazini amechoka jitahidi kumsaidia Kaz mbalimbali, sio usubiri mpaka akuombe, pia unaweza kumsaidia kutengeneza vitu mbalimbali vilivyoharibika ndani, usisubiri akuombe, unaweza msaidia kutoa takataka nje kabla hajakuambia.

Kiufupi wanawake wanapooza hisia zao za huzuni, chuki, hasira kwa kuziongea na watu wa karibu. So anapokushirikisha jinsi anavyojisikia usizani kuwa anakushutumu wewe bali muonyeshe kuwa unajali hisia zake kwa kumkumbatia, kumkiss, kumletea zawadi na sio KUTOA USHAURI. Asante
 
Ili mwanamke afunguke kwako lazima ajisikie amani na usalama kwako. Wanaume wengi huwa wanawapotezea wanawake zao kwenye kuongea, ndio mana wanawake wao pia huwapotezea kitandani. Sababu mwanamke anaona haujali hisia zake.

nini kinachondelea kihisia kinachomfanya asijiachie kwako kitandani, na uoneshe kujali hisia zake.
Wanawake hawa hawa ila hamna formula moja
 
You nailed it mkuu. Ni kweli wanawake wanahitaji kusikilizwa Sana (kujali) na wewe Kama mwanaume unapomsikiliza usiwe "Mr Fixer" yaani mzee wa kutatua Mambo, Ila jifunze Sana kuwa msikilizaji na kumuonyesha kwamba unaelewa jinsi anavyojisikia. Pia wanawake wanapenda kufanyiwa vitu bila kuomba kufanyiwa.

Mfano anaporudi kazini amechoka jitahidi kumsaidia Kaz mbalimbali, sio usubiri mpaka akuombe, pia unaweza kumsaidia kutengeneza vitu mbalimbali vilivyoharibika ndani, usisubiri akuombe, unaweza msaidia kutoa takataka nje kabla hajakuambia.

Kiufupi wanawake wanapooza hisia zao za huzuni, chuki, hasira kwa kuziongea na watu wa karibu. So anapokushirikisha jinsi anavyojisikia usizani kuwa anakushutumu wewe bali muonyeshe kuwa unajali hisia zake kwa kumkumbatia, kumkiss, kumletea zawadi na sio KUTOA USHAURI. Asante
Umesema vizuri.
 
Back
Top Bottom