Njia rahisi ya kutengeneza fedha kwenye jamii yako

May 30, 2023
9
15

Ili uweze kuwa na pesa nyingi unatakiwa kuwatazama watu wanaokuzunguka kwa jicho la tatu, huku ukifikiri ni kwa namna gani watu hao watakavyokupa pesa zao.

Ili jambo liweze kutekelezeka hatimaye kuchukua pesa za watu hao wanaokuzunguka unatakiwa kuangalia na matatizo yanayowasonga watu hao kisha watafutie majibu ya changamoto hizo zinazowasonga.

Ukifanya hivyo ni watu lazima watakupa pesa tu, kila palipo na changamoto fulani ndipo sehemu ilipo na fedha, hivyo jifunze kutafuta suluhisho la matatizo ya watu ili kupata fedha zaidi.
 
Ukitaka kufanikiwa angalia wajinga wapo wapi, mfano wajinga wa soka, wajinga wa kubeti na wajinga wasiojali afya zao kwa kilevi.

Mjinga atakufata ulipo wewe na kukupatia hela yake kwa ujinga wake.
 
Back
Top Bottom