Njia panda ya mapenzi

Njia panda ya mapenzi

Kwani ulimpa kitu gani mpaka amechanganyikiwa au ulimpeleka kwa mpalange
Habari za mchana wadau.
Ni hivi ni takriban miezi sita Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu,tunapendana Sana na tumespend Sana kipindi cha miez mitano iliyopita bila mkewe kujua.

Nikapata Safari mkoa flan,tukawa tunawasiliana kwenye simu almost every day and night.Sasa mhusika akawa hafuti zile simu na meseji tunazoandikiana.Akabadilika na tabia kwani kila usiku ilikuwa lazima tuzungumze hata hadi saa 8 za usiku.Mkewe akamchunguza simu yake akagundua Hilo, akachukua na namba yangu.

Sikumoja akanipigia simu usiku wa manane akanionya kuhusu kutoka na mumewe,akanambia ananipa taarifa kistaarabu ,nikamjibu nimemwelewa na nitaacha.Mchana akanipigia mumewe kunijulia hali,nikamweleza hali halisi ya mkewe kugundua penzi letu na mkwara alionipiga,nikamsihi aache kunipigia simu hasa usiku.Akanambia sawa.

Baada ya sikumbili wamekaa sehemu na mkewe usiku,akatoka pembeni kunipigia simu,mkewe akamwona,alivyorudi walipokuwa wameketi,mkewe akachukua simu ya mumewe kuangalia jamaa alikuwa anaongea na Nani,akakuta ni Mimi.Basi ukazuka ugomvi mkubwa Hadi kuvunjiana simu na mwanamke kuondoka nyumbani.

Asubuhi jamaa akanipigia simu kunielezea kisa kile,nikamshauri amfate mkewe ambembeleze arudi nyumbani.Kweli akafanya hivyo.Tatizo jamaa amegoma kutonipigia simu,anapiga hadi usiku.Wasiwasi wangu nakaribia kurudi toka Safari,halafu tunaishi majiran,je akinivamia?manake alishanionya nikamwelewa Ila tatizo mumewe kawa king'ang'anizi kwangu.
Wadau nifanyeje kwenye scenario hii?
 
Mimi hapa ndipo ninapopata kizunguzungu....Kiimani (Islamic) mume anaruhusiwa kuongeza mke wa pili mpaka hata wa nne...... Wakati akiwa kwenye hii process je huyo mwanamke wa nyongeza (wa pili, tatu au nne) huwa haihesabiki kama anakuwa na mahusiano na mume wa mtu? Au Kiislamu kuwa na mahusiano na mume wa mtu sio dhambi?
Mie sio muislam so sijui
 
Nimechukua hatua mumewe ndio king'ang'anizi.

Sasa hiyo ni hatua? Ungekata mawasiliano sio unaendeleza mawasiliano alaf unasema umechukua hatua. Huyo mwanaume nae bwege sana na hapo hajatiliwa limbwata anakuwa speed hivyo ana mke simu za usiku anazipendea nn au ndio anakuchunga?
 
Mimi hapa ndipo ninapopata kizunguzungu....Kiimani (Islamic) mume anaruhusiwa kuongeza mke wa pili mpaka hata wa nne...... Wakati akiwa kwenye hii process je huyo mwanamke wa nyongeza (wa pili, tatu au nne) huwa haihesabiki kama anakuwa na mahusiano na mume wa mtu? Au Kiislamu kuwa na mahusiano na mume wa mtu sio dhambi?
kimsingi ukianzisha uhusiano vichochoroni ni kinyume na utaratibu, unataka kuongeza mke fata taratibu Kama dini husika ilivyoagiza. Na taratibu ziko wazi kabisa
 
Ahsante Mkuu. Kwa hiyo taratibu ni kumwooa binti ambaye hamjawahi kuwa na mahusiano kabisa?
 
ndiyo hivyo mkuu. Ila kwa dunia ya sasa ni changamoto kweli
 
  • Thanks
Reactions: Mj1
Wewe cha msingi uhame mtaa tu kwa usalama wako au usubirie kulogwa 😂😂😂 kama hutaacha mchezo wa kumuibia mwenzio mume!!!
Halafu mbona vijana tulio single ni wengi mtaani, mnkwama wapi?
 
Habari za mchana wadau.
Ni hivi ni takriban miezi sita Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu,tunapendana Sana na tumespend Sana kipindi cha miez mitano iliyopita bila mkewe kujua.

Nikapata Safari mkoa flan,tukawa tunawasiliana kwenye simu almost every day and night.Sasa mhusika akawa hafuti zile simu na meseji tunazoandikiana.Akabadilika na tabia kwani kila usiku ilikuwa lazima tuzungumze hata hadi saa 8 za usiku.Mkewe akamchunguza simu yake akagundua Hilo, akachukua na namba yangu.

Sikumoja akanipigia simu usiku wa manane akanionya kuhusu kutoka na mumewe,akanambia ananipa taarifa kistaarabu ,nikamjibu nimemwelewa na nitaacha.Mchana akanipigia mumewe kunijulia hali,nikamweleza hali halisi ya mkewe kugundua penzi letu na mkwara alionipiga,nikamsihi aache kunipigia simu hasa usiku.Akanambia sawa.

Baada ya sikumbili wamekaa sehemu na mkewe usiku,akatoka pembeni kunipigia simu,mkewe akamwona,alivyorudi walipokuwa wameketi,mkewe akachukua simu ya mumewe kuangalia jamaa alikuwa anaongea na Nani,akakuta ni Mimi.Basi ukazuka ugomvi mkubwa Hadi kuvunjiana simu na mwanamke kuondoka nyumbani.

Asubuhi jamaa akanipigia simu kunielezea kisa kile,nikamshauri amfate mkewe ambembeleze arudi nyumbani.Kweli akafanya hivyo.Tatizo jamaa amegoma kutonipigia simu,anapiga hadi usiku.Wasiwasi wangu nakaribia kurudi toka Safari,halafu tunaishi majiran,je akinivamia?manake alishanionya nikamwelewa Ila tatizo mumewe kawa king'ang'anizi kwangu.
Wadau nifanyeje kwenye scenario hii?
Sasa mwambie akuhalalishe na akutambulishe kwa mkewe
 
Mimi ushauri wangu mng’ang’anie huyo mwanaume usikubali kupigwa mkwara kijinga hivo mume wa mtu mtamu
 
Naona mdau ameanza kushiboka na kabichi za mpito...
 
Back
Top Bottom