Changamoto Kuu 2 za Majengo ya Kupangisha hapa Tanzania

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Falsafa ya kujenga utajiri kupitia kipato endelevu ndiyo imeonekana kuwa ni falsafa ya kweli kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita. Falsafa hii inafaa zaidi kuitumia kujenga utajiri ukilinganisha na ile falsafa ya kutengeneza faida.

Zipo njia nyingi za kutengeneza kipato endelevu kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo. Njia ni kama ifuatavyo:

✓ Kumiliki majengo ya kupangisha.

✓ Kumiliki makontena au mabanda ya kupangisha.

✓ Kumiliki mashamba ya kukodisha.

✓ Njia zisizo za moja kwa moja za kutengeneza kipato endelevu zikiwemo uandishi wa vitabu, vipindi kwenye televisheni, utoaji wa ushauri kitaalamu na kadhalika.

Kati ya njia zote za kutengeneza kipato endelevu, kipato endelevu kutokana na majengo ya kupangua ndicho kinaweza kumfanya mwekezaji kuwa tajiri kwa uhakika ukilinganisha na njia zingine.

Lakini majengo ya kupangisha yamekuwa na changamoto kuu 2 katika mazingira yetu ya Tanzania. Changamoto hizi sio changamoto kuu kwenye njia zingine za kutengeneza kipato endelevu.

Changamoto hizi mbili sio changamoto kuu kwenye nchi zilijenga mifumo mizuri ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo ikilinganishwa na hapa kwetu Tanzania.

Changamoto Ya Kwanza.

Kukusanya mtaji fedha.

Hii ni changamoto kuu katika mazungumzo yetu ya Tanzania kwa sababu;

✓ Hakuna utolewaji toshelevu wa mikopo ya uwekezaji kwenye majengo ya kupangisha.

✓ Hakuna elimu na uthubutu wa kuchangiana mitaji fedha. Wengi tunachangiana kwenye tukio la ndoa, kipaimara, sikukuu kuzaliwa, mahari ya kumaliza elimu ya mifumo ya kimagharibi, n.k.

✓ Kukosa mfuko maalumu wezeshi kwa wanaonza kuwekeza kwenye ardhi na majengo.

✓ Kokosa umoja na kuaminiana miongoni mwa vijana ili wakusanye nguvu, mtaji na muda wao ili kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha.

Suluhisho Kuhusu Changamoto Ya Mtaji Fedha.

✓ Kuanzisha mfuko maalumu wa kuwawezesha wawekezaji wanaonza kuwekeza. Mfuko unaweza kuw

✓ Kufungua vikundi vya wawekezaji wanaonza kwa ajili ya kutumia njia za uwekezaji zinazo hitaji kiasi kidogo cha mtaji fedha ikiwemo kununua na kuuza viwanja, kumiliki mashamba ya kukodisha, kumiliki mabanda ya biashara kwa lengo la kukodisha, kutoa huduma za udalali, ukaguzi wa nyumba, n.k.

✓ Kuboresha mifumo ya mikopo ya majengo kutoka taasisi za kifedha.

✓ Kujenga tabia ya uwekaji wa akiba kwa ajili ya kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha.

Changamoto ya pili.

Jinsi ya kurudisha mtaji fedha uliowekezwa kwenye majengo ya kupangisha.

Majengo ya kupangisha huingiza jumla ya kipato endelevu sawa na bei ya kununulia au kujengea jengo husika kwa miaka mitano hadi saba. Kwa kipindi hiki, utaweza kununua nyumba ya pili ya kupangisha ikiwa kipato chote kitatumika kununua au kujengea nyumba ya pili ya kupangisha.

Miaka sita ni miaka mingi sana kumiliki nyumba ya pili toka umiliki wa nyumba ya kwanza. Hivyo ni lazima uweze kuwa njia za kukabiliana na changamoto hii.

Njia za kurudisha mtaji fedha kutumia nyumba yako ya kwanza ni kama ifuatavyo:

✓ Kutumia mbinu ya B-R-R-R-R ya majengo ya kupangisha (Buy, Renovate, Rent, Refinance, Repeat). Hii huhusisha hatua ya kununua nyumba, kukarabati, kukodisha, kuombea mkopo na kurudia hatua ya kwanza ili umiliki nyumba ya tatu.

✓ Kutumia mbinu mseto ya mtaji fedha kwa 100% na mbinu ya B-R-R-R-R kwa wakati mmoja. Hapa nusu ya idadi ya nyumba zako unatumia mbinu ya B-R-R-R-R na nusu ya idadi ya nyumba zako za kupangisha unatumia fedha zako kwa 100%.

✓ Kuwa na ajira au biashara ambayo itakuwa ni chanzo cha mtaji fedha kwa umiliki wa nyumba ya pili ya kukodisha.

✓ Kununua nyumba ya pili kwa kutumia mkopo kutoka benki bila kuweka dhamana nyumba yako ya kwanza. Hii ni ngumu kuifanikisha hasa kwa mazingira yetu ya Tanzania ambayo mambo bora ya umiliki wa ardhi bado yanasuasua.

✓ Kutumia kipato endelevu kwenye mbinu za kuingiza faida kwa haraka ikiwemo kununua na kuuza viwanja.

Kwa ufupi, hizo ndiyo changamoto ambazo unatakiwa kuwekeza nguvu, maarifa na taarifa ili uweze kupiga hatua kubwa kwenye uwekezaji huu.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

MUHIMU; Jiunge na kundi la whatsapp liitwalo TZ REAL ESTATE TEAM. Ukiwa hapa utapata masomo na mijadala kuhusu uwekezaji kwenye ardhi na majengo (real estate investment).

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom