NJAA YAJA: Dear Mr. President, On a Serious Note...

NJAA YAJA: Dear Mr. President, On a Serious Note...

It is coming....!!

Bei za vyakula zapanda tena (Majira)


*Mchele, maharage, sembe, mafuta 'hayashikiki'
* Gunia la mkaa sasa 30,000/-, ndizi nazo 'zapaa'


Na Eben-Ezery Mende

PAMOJA na kauli ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustapha Mkulo kuwa pato la Taifa limeongezeka na kuchangia kukua pato la wastani wa Mtanzania mmoja mmoja kati ya mwaka 1992 na mwaka huu, hali ya maisha ya Watanzania inazidi kuwa taabani kutokana na kupanda kila siku bei za bidhaa madukani hususani vyakula na kutishia kutimia ndoto za Maisha Bora kwa kila Mtanzania.

Mapema wiki hii, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, Bw. Mkulo alitoa takwimu zikionesha ukuaji mzuri wa pato la Taifa ambapo alisema mwaka 2007 pato hilo lilikuwa sh. trilioni 18 na mwaka huu linatarajiwa kufikia sh. trilioni 25.

Alisema kutokana na ukuaji huo, pato la Mtanzania mmoja mmoja nalo limeongezeka kutoka sh. 480,000 mwaka 1992 hadi sh. 545,455 mwaka 2007 na linatarajia kufikia sh. 631,300 mwaka huu.

Hata hivyo,Bw. Mkulo katika takwimu zake alishindwa kutoa takwimu zinazoonesha pengo lililopo sasa kati ya wenye nacho na wasionacho na kukiri kuwa serikali haijafanya utafiti unaoweza kutoa takwimu hizo.

Wakati Bw. Mkulo akitamba kukua kwa pato la Taifa sambamba na la Mtanzania mmoja mmoja, bei za vyakula madukani na katika masoko mbalimbali zimekuwa zikipanda siku hadi hali inayowafanya mamilioni ya Watanzania kukuza mkanda ambao sasa unakaribia 'kugusa mifupa.'

Jijini Dar es Salaam imeelezwa kuwa bei za vyakula zimepanda kwa zaidi ya asilimia 12 ikilinganisha na mwanzoni mwa mwaka huu.

Ongezeko hilo limeibua 'kilio' kwa wananchi wengi hususani wa kipato cha chini ambao sasa wameshuhudia kupanda mara dufu kwa bei za 'bidhaa wakombozi' kama chumvi na maharage ambazo kwa muda mrefu hawakuwahi kushuhudia ongezeko la bei zake.

Uchunguzi uliofanywa na Majira katika maduka mbalimbali jijini umebaini kuwa sukari ambayo mwanzoni mwa mwaka iliuzwa sh. 950 kwa kilo, sasa imefikia sh. 1,200 unga wa ngano umepanda kutoka sh. 750 kwa kilo na kufikia sh. 900. Sembe imepanda kutoka sh. 550 na kufikia sh. 700. Mafuta ya kupikia (Korie) ujazo wa lita 20 yamepanda kutoka sh.38,000 na kufikia sh. 44,000.

Mche wa sabuni ya kufulia ambao awali uliuzwa sh. 750 sasa umefikia sh. 1,000, kiberiti nacho kimepanda kutoka sh. 40 hadi sh. 50, mshumaa sasa unauzwa sh. 150 badala ya sh. 100, sabuni ya kufulia ya unga yenye ujazo wa gramu 50 awali iliuzwa sh. 150 sasa imefikia sh. 200.

Mkate wa gramu 500 mwanzoni mwa mwaka uliuzwa sh. 450 sasa unauzwa sh. 600, majani ya chai paketi ya gramu tatu awali iliuzwa sh. 10 sasa ni sh. 25, lita moja ya mafuta ya taa imepanda kutoka sh. 970 na kufikia sh. 1,300

Gunia la mkaa mwanzoni mwa mwaka lililouzwa sh. 19,000 sasa limefikia sh. 30,000. Nyama ya ng'ombe (steki) imepanda kutoka sh. 3,000 kwa kilo hadi sh. 4,000 na mchanganyiko kutoka sh. 2,500 hadi sh.3,000. Chumvi ya ujazo wa gramu 200 awali iliuzwa sh. 100 sasa imefikia sh. 150

Mchele wa Mbeya sasa umefikia sh. 1,500 kwa kilo huku maharage (soya) yakigota sh. 1,600. Awali katika masoko ya Dar es Salaam hususan Tandale soya iliuzwa sh. 1,000. Vyakula vingine mfano viazi mviringo vimepanda kutoka sh. 20,000 kwa gunia na kufikia sh. 30,000

Mkungu wa ndizi aina ya mshale awali uliuzwa sh. 6,300 sasa umefikia sh. 15,000, wakati malindi umepanda kutoka sh. 7,000 na kufikia sh. 13,000.

"Bei ya vyakula zilianza kupanda zaidi mwanzoni mwa mwaka huu hasa pale bei ya mafuta ilipopanda, "alisema Bw. Ally Uledy mmoja wa viongozi katika Soko la Tandale, jijini Dar es Salaam .

Akielezea upatikanaji wa vyakula hivyo mikoani, mmoja wa wafanya biashara wa mchele wa Mbeya sokoni hapo, Bw. Suleman Said, alisema kuna uhaba mkubwa wa chakula hicho kutokana na msimu wa mavuno unaoendelea.

"Mimi nafanya biashara ya mchele kwa miaka mitano sasa, upandaji bei wa mwaka huu umekuwa mkubwa sana kutokana na mambo mengi, kwanza ni kupanda kwa bei ya mafuta, ukame kwa baadhi ya mikoa na baadhi ya wakulima kukata tamaa kutokana na kupata hasara msimu wa mwaka jana," alisema.

Mbali na kupanda bei za vyakula, bidhaa zingine kama vifaa vya ujenzi nazo zimepanda bei mara dufu wakati saruji iliyokuwa ikiuzwa kati ya sh. 11,500 hadi 12,500 mwanzoni mwa mwaka sasa inauzwa kati ya sh.15,500 na sh. 16,500.

Wakati bei hizo zikipanda zipo taarifa za ongezeko la bei ya mafuta kwenye soko la dunia hali inayotishia kuzidi kupanda zaidi kwa bei za bidhaa zingine.

Takwimu zinaonesha kuwa pipa la mafuta ghafi sasa limefikia dola za Marekani 120 na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu linatarajiwa kufikia dola 200. Januari pipa liliuzwa kwa dola 60.
 
Serikali kichwa cha mwenda wazimu, kama serikali ya Tanzania haiwezi kuhedge swala la njaa wacha ifike then tuombe msaada kwa Waasia na Waamerica. Swala kubwa linalokwanza pale kwetu ni takwimu hai na mastatician wanajua kazi yao.

Haya mambo can always be predictable and serikali can hedge that risk. Lakini serikali ya Tanzania itaanguka kwenye the same mtego, sasa najiuliza kwa nini tuogope, we know inakuja. Let us wait.

Njaa ikija kina Rostam wanafaidi, njaa isipokuja pia wanafaidi. Kwao wao ni win win situation. Serikali ikiagiza chakula nje kwa kutumia mawakala, guess nani anaeshinda bid? Rostam na watu wake, then wanapata tax exemption na wakija wanauzia serikali at roof price.

What a damn government.
 
Heshima mbele wakuu, naona kidogo jamaa wameanza kujiuliza what is happening.... Lakini sio kwamba wameona tatizo bali wameweka maswali ya kufuatilia reason why bei zinapanda... Check the colored texts.... Nimekaribia ku faint pale kwenye BOLD and RED statement!!!!

Angalia hii article from Guardian la leo:

`Govt is grappling with skyrocketing food, fuel prices`

2008-05-14 10:09:45
By Lusekelo Philemon

The Government has declared that it is keen on curbing skyrocketing food and fuel prices, which are hitting the poor most, State House spokesperson said yesterday.


Speaking at a news conference in Dar es Salaam, State House communications director Salva Rweyemamu said increasing prices of basic items like food and energy were now a global concern.

``The government is trying to put all necessary control measures in place to mitigate the adverse spillover effects of this problem at domestic level,`` he said, adding that there had been an outcry across the world over food prices.

Latest economic review released by the Bank of Tanzania (BoT) says inflation rate reached 8.9 per cent last March.

It cites increases in consumer prices for items such as drinks, tobacco, fuel, electricity, water and transportation as the chief cause for rising inflation.

The State House official said that under the liberalised market system, the government had a very minimal role to play in the control of commodity prices.

He however urged farmers to produce more food crops, saying the move would help the country out of catastrophic food crisis situation.

``We should not allow excessive importation of food,� he said.

Home currency is particularly susceptible to drought, which prompts importation of food inflation, coupled by increased costs related to oil imports from abroad.

Tanzania has suffered intermittent droughts since 2004 when inflation rate was 4.4 percent, then increased to 5.4 percent in 2005, and later decreased to 4.3 percent in 2006. It re-emerged last year to reach 5.9 percent.
He said farmers also should develop a culture of preserving harvested food crops.

Analysts are also worried that current rising inflation is also contributed by low international flow of capital, which in turn has been occasioned by global credit crunch, especially the crisis related to collapse of US the sub-prime mortgage sector.

There are also concerns that foreign direct investment flows are equally on the wane, as the administration looks leaned only to serious foreign investors.

The obtaining inflation rate is the highest since early 2000s when it had settled at 4.4 percent, propped up by a strong local currency and influx of huge FDIs, especially in the mining sector.

It had by then been reduced from about 30 percent in the early 1980s through tight monetary policy and deliberate boosting of manufacturing and exports.
BoT has said it would consolidate these measures even further.

The government`s statement comes in the wake of the International Monetary Fund (IMF)`s warning that global inflation had re-emerged as a major threat to the world`s economy.

John Lipsky, the IMF deputy managing director said inflation concerns had re-surfaced after years of quiescence due to soaring energy and food prices. He said growth was slowing but headline inflation was accelerating.

The IMF warning came as crude oil prices hit a record increase of almost USD124, up by 99 per cent over last 12 months, as customers scrambled to take out insurance against prices rising above USD200 a barrel.

Lipsky said the forces pushing prices up appeared to be fundamental in nature and these were being amplified by lower interest rates and the US dollar�s decline.

He was optimistic that there would not be a repeat of the early 1970s when increasing energy prices ushered in a period of rising inflation expectations and accelerating inflation. However, he said this risk could not be discarded out of hand.

Lipsky said policy makers must respond aggressively to any signs of rising inflation expectations, lest the impressive gains in global stability in recent years be sacrificed.

On the other hand, experts say the IMF has warned that food prices will remain high for the foreseeable future.

SOURCE: Guardian
 
And from Tanzania Daima wanasema kwamba kuna njaaa, lakini angalia msisitizo ulipowekwa sio kwenye njaa, ni kwenye sababu za kiuchumi..... Duh, pamoja na kwamba wameanza kushituka kuwa kutakuwa na njaaa, still kama ilivyosemwa kwenye Guardian hapo juu sidhani kama ku control "Import of Food" kutasaidia chochote, nadhani control ya "Export of Food" ndio what we need at this time...

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.................

Article ya Daima ndio hii:

Serikali yatahadharisha kuhusu upungufu wa chakula

na Irene Mark

SERIKALI imeonya na kutahadharisha kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa upungufu wa chakula nchini, hivyo kuwataka wananchi kutumia chakula walichonacho kwa uangalifu.

Onyo hilo lilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Rweyemamu alionya kuwa upungufu wa chakula hivi sasa ni suala linaloikabili dunia lakini nchi maskini ndizo zilizoathirika sana, hivyo Watanzania wanatakiwa kuwa macho na hali hiyo.

“Watanzania nawashauri kutunza vema chakula walichonacho kutokana na hatari ya upungufu wake nchini,” alisema Rweyemamu na kuongeza kwamba hali hiyo inatokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Alibainisha kuwa bei ya mafuta ghafi duniani imepanda na kufikia dola za Marekani 124 kwa pipa, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 99 kwa mujibu wa takwimu za mwaka mmoja uliopita.

Hata hivyo, imebainishwa kuwa zipo sababu za msingi za kupanda kwa bei ya mafuta zinazochangiwa na viwango vya riba na udhaifu wa sarafu ya dola ya Marekani.

Alisema katika onyo hilo, watawala na wabunifu wa sera za kiuchumi duniani wametakiwa kuchukua hatua madhubuti na haraka za kupambana na dalili za mfumuko wa bei.

“Tishio la kuyumba kwa uchumi wa dunia linazidi kuongezeka… kwa hapa (Tanzania) maumivu tunayoyaona sasa yataongezeka.

“Unajua tunaposema kupanda kwa hali ngumu ya maisha kunatokana na ongezeko la bei ya mafuta, kwa wananchi wa hali ya chini tunayapata zaidi magumu hayo kwenye ununuzi wa chakula,” alisema Rweyemamu.

Wakati huohuo, alisema serikali imeteua watendaji wake 22 kuwa wsemaji wakuu wa wizara mbalimbali nchini na kufafanua kwamba, uteuzi huo utawapa mamkala ya kuingia kwenye vikao vya maamuzi ya wizara husika.

“Napenda kuwajulisha kwamba, serikali imewateua wasemaji wakuu wa wizara 22 kati ya 23 zilizopo. Watendaji hawa watakuwa na mamlaka kamili ya kuwahabarisha wananchi jambo juu ya wizara zao,” alisema na kuongeza kuwa wasemaji hao watashauriwa kuzungumza na waandishi wa habari kila baada ya muda fulani.

Rweyemamu alisema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa haijapeleka jina la msemaji wao, hivyo hakuna aliyeteuliwa kuwa msemaji wa wizara hiyo.

Courtesy: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/5/14/habari3.php
 
slowly we are getting there.. lakini still is not enough;

Matukio ya Burma na China, yataathiri sana chakula nyumbani na haitoshi kushauri watu watumie chakula vizuri (wasile??) Binafsi ningefurahi kusikia watuambie our SGR iko vipi, na wafungulie milango na kuondoa kodi ya vyakula muhimu; n.k
 
HERE WE GO! 1



Makubo Haruni, Rorya
Daily News; Wednesday,May 14, 2008 @00:05

WAKAZI wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, wanakabiliwa na upungufu wa chakula na kusababisha kukumbwa na njaa, hali iliyoilazimu serikali kuiagizia tani 100 za mahindi ili kukabiliana na hali hiyo.

Hayo yamebainika katika ziara ya siku mbili ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Crizant Rubunga iliyokuwa na lengo la kuweka mikakati ya kukabiliana na uhaba wa chakula wilayani humo.

Aliwaagiza watendaji wa Halmashauri kusimamia zoezi la kilimo kwa kila kaya kulima ekari mbili za mazao ya chakula na biashara. Katika majumuisho ya ziara yake, Rubunga aliiagiza Halmashauri ya Wilaya hiyo hususani watendaji na madiwani kuhakikisha kilimo kinawekewa kipaumbele na kuwa ajenda ya kudumu ili kuepuka njaa isiyo ya lazima kutokana na uzembe na uvivu kwa wakazi wake.

Alisema wananchi wa Rorya wana uwezo wa kufanya kazi, lakini imebainika kuwa hawajitumi kulima na kutunza chakula na kukaribisha njaa; kitendo ambacho aliagiza kila kata kuwapo daftari litakalokuwa na orodha ya wakulima na wasimamiwe na watakaokaidi kulima wachukuliwe hatua za kisheria.

Alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya, Jacob Kayange, kuhakikisha anawachukulia hatua za kinidhamu, ikiwamo kuwafukuza kazi watendaji wa kata na vijiji watakaobainika kuishi nje ya vituo vyao vya kazi na kushindwa kuwahudumia wananchi katika kutatua kero zao na kuhimiza maendeleo.

Aliwataka pia wananchi wa Rorya, hususani wanasiasa waache malumbano na mvutano wa wapi pawe makao makuu, badala yake waiachie serikali iamue kwa kuzingatia mapendekezo ya awali ili kutoa fursa ya kujengwa makao makuu ya wilaya hiyo na kuwapo urahisi wa kutoa huduma kwao.

Kayange alimwambia Katibu Tawala huyo kuwa kukosekana kwa makao makuu ya wilaya, watumishi wanafanya kazi katika mazingira magumu na wasiwasi mkubwa kutokana na kubanwa na kutishiwa kutimuliwa katika majengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ambako wamepewa siku 14 ili kuondoka katika ofisi na nyumba za kuishi watumishi.
 
Mkuu Mwanakajiji,

Inasikitisha kuona kwamba Tanzania haina tena "the big four".

Leo hii tusingekuwa na shida hizi.
 
HERE WE GO 2

Dodoma wakabiliwa na njaa

Dodoma yanyemelewa na njaa

na Rahel Chizoza, Dodoma


MKOA wa Dodoma upo hatarini kukumbwa na baa la njaa kutokana na maeneo mengi kushindwa kapata kiwango cha mavuno yaliyotarajiwa katika msimu huu wa kilimo.

Wananchi wa Kijiji cha Iyumbu, kilichopo wilayani Dodoma Mjini, walisema kuwa katika msimu huu wa mavuno, wamepata mavuno hafifu ambayo hayalingani na matarajio waliyokuwa wamejiwekea.

Wakiongea katika mkutano wa hadhara walipotembelewa na mbunge wa Dodoma Mjini, Ephraim Madeje (CCM), walisema kuwa kwa kawaida huwa wanavuna magunia sita mpaka manane katika shamba la ekari moja ya mtama, lakini katika msimu huu wanatarajia kuvuna wastani wa magunia mawili tu kwa kila ekari.

Walisema kutokana na hali hiyo wanaiomba serikali ikae ikijua kuwa kitafikia kipindi cha karibu na msimu wa kilimo ambapo watahitaji kupatiwa msaada wa chakula.

Walibainisha kuwa hali hiyo ya mavuno hafifu imesababishwa na mvua za masika kunyesha kwa kukatakata na hivyo baadhi ya mazao kukauka kabla hayajafikia hatua ya kukomaa.

“Unyeshaji wa mvua katika msimu huu haukuwa wa kuridhisha kutokana na kuwepo kwa vipindi virefu vya jua, ingawa wananchi wamejitahidi kulima kwa bidii, hali ya mavuno hairidhishi,” alisema mwenyekiti wa kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina la Yona Mlomo.

Alibainisha pia hata sasa bei za chakula hazijashuka kama ilivyo katika miaka mingine, ambapo katika msimu wa mavuno bei za mazao huwa ni nafuu na kuwawezesha kununua chakula kingi na kujiwekea akiba.

Akiongea na wananchi hao, Madeje alikiri kuwepo kwa hali ya mavuno hafifu inayoashiria njaa na kusema kuwa ametembelea maeneo mengi ya jimbo lake na kukuta wananchi wakiwa na matatizo katika mavuno.

Alisema kuwa mbali na kuwepo kwa mavuno hayo hafifu, wananchi nao wanapaswa kutunza chakula kidogo walichopata, ili kiweze kuwasaidia kwa muda mrefu kabla ya kuhitaji msaada kutoka serikalini.

Aliwataka wananchi hao kupunguza matumizi ya nafaka katika kupika pombe za kienyeji au kununua vitu kwa kubadilisha na nafaka kwani utaratibu huo umekuwa ukichangia kaya kukumbwa na upungufu wa chakula.
 
Nadhani mumesikia juu ya makampuni yanayotaka kulima mazao kwenye ardhi yetu kwa ajili ya baofuel sijui ni wangapi kati yenu mnalifahamu hilo? nchi ilishagawanywa kati ya makampuni hayo yanayohitaji hekta kwa hekta kwa ajili ya baofuel za kuendeshea magari ya ulaya na wakuu wetu wamepigwa changa la macho eti watapata soko ulaya! Rufiji,Kisarawe, Mbarali, Bagamoya Kagera Kigoma Mtwara, Lindi ni baadhi ya maeneo ambayo tayri yalishakuwa earmarked kwa ajili ya mashamba hayo, wanavijiji wengine kwa kurubuniwa kwa ahadi za ajira tayari washaridhia ardhi zao kuhawilishwa! Sasa sisi tungezalisha chakula cha kutosha si tungekuwa matajiri tena tunaidikteti nini tunataka kwakutumia silaha ya chakula! Serikali iliyolala matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona yaani kwa sera zao mbovu za kilimo tunaonekana tuna ardhi kubwa unategemea jembe la mkono lilime ekari ngapi?
 
maneno mazito hayo yaani tufe njaa kwa ajili ya kuja kuzalisha mafuta ya magari!
 
Kingine ninachokiona ni movement ya chakula toka maeneo yenye ziada kwenda maeneo yenye upungufu. Kama bei zitakuwa juu zaidi kwenye maeneo ya upungufu huenda baadhi ya wakulima wakauza hata mbegu na kusababisha njaa zaidi. Kama serikali haikuwa strict hata movement ya chakula kwenda nchi za jiani inaweza kutokea na kuharakisha nchi kukabiliwa na kuongezeka bei za chakula. Ni muhimu basi contingency plans zianze kufanyika kwani issue iko obvious na ni global!
 
unajua kitu kitakachotokea ni kuwa:

a. Hatujajiandaa kwa akiba ya chakula
b. matukio ya China na Burma yanazidisha upungufu wa chakula (kwani kingi kinapelekwa kwenye maeneo hayo ya majanga)
c. Nchi za Jirani kama Kongo, Zimbabwe, Malawi zinaanza kuwa na upungufu mkubwa (even Kenya) na Watanzania wa mipakani wanaanza kupungukiwa kwa chakula
d. Matokeo yake mikoa ya katikati (morogoro, Dodoma, tabora) inaanza kupata upungufu mkubwa wa chakula.
e. Serikali inatangaza kuomba misaada toka nje
f. Oops.. misaada inachelewa kwani nchi nyingi tayari zinahitaji.
g. Tunaanza kula Yanga tena
h. Watu watamlaumu Nyerere!
 
akiba ya chakula tanzania ipo tena kubwa sana, jamani hadi muambiwe kila kitu ?

chakula kipo, na kama hakipo, basi mnafaa kulaumiwa nyinyi mnaolalamika ! Hamtaki kwenda kwenye mashamba kazi kwenye intaneti 24/7, mara ya mwisho Mnyika alikataa kata kata ushauri wangu wa kwenda shambani instead akaenda kwa wamachinga.

Kila mmoja humu anaweza kulima hekari 20 kutokana na uwepo wako humu ( kuna baadhi wanalala humu humu) hao nadhani wanaweza kuzalisha zaidi ! kama akina mwafrika wa kike !
 
From BBC

Action is needed to prevent the current food crisis in Africa from becoming a disaster, the official heading a new UN food task force has warned.

Sir John Holmes told the BBC the solution to food shortages would be different for each country but there had to be a co-ordinated approach.

Escalating prices and shortages have sparked riots in more than half a dozen African states in recent months.

He said vulnerable children, pregnant woman and the old would be prioritised.

"We'll be trying to put together a comprehensive plan of action, but of course that needs to be translated into a local plan," he told the BBC's Network Africa programme.

The United Nations task force brings together the UN, the International Monetary Fund and the World Bank and other agencies.

Much of the focus appears to be on the need for some kind of "green revolution" among farmers - especially in Africa.

UN Secretary-General Ban Ki-moon recently said the world would need to find $1.7bn (£860m) to help them buy the seeds and fertilisers they needed.
 
akiba ya chakula tanzania ipo tena kubwa sana, jamani hadi muambiwe kila kitu ?

chakula kipo, na kama hakipo, basi mnafaa kulaumiwa nyinyi mnaolalamika ! Hamtaki kwenda kwenye mashamba kazi kwenye intaneti 24/7, mara ya mwisho Mnyika alikataa kata kata ushauri wangu wa kwenda shambani instead akaenda kwa wamachinga.

Kila mmoja humu anaweza kulima hekari 20 kutokana na uwepo wako humu ( kuna baadhi wanalala humu humu) hao nadhani wanaweza kuzalisha zaidi ! kama akina mwafrika wa kike !

Kada,

uchumi wa dunia unampa kila mtu sehemu yake, na kama Adam Smith alivyosema the most utility ya vitu inapatikana kama tukiwa na specialization.Sasa wewe unataka IT Guru mwenye Cisco credentials, six figure salary na utaalamu wa financial markets aliyeko Silicon Alley aende Tanzania kujiunga na kilimo wakati huyu anaweza kubaki huku mtandaoni akafinance watu walime wakati yeye anaangalia bei za mazao mtandaoni na kujua mazao gani yanalipa katika soko la dunia?

Argument ya kuwa ukiwa online huwezi kuzalisha ni weak, sema jingine.
 
Life getting tougher as food prices soar

2008-05-18 11:13:47
By Lucas Lukumbo

There are ominous signs that the country may face a serious food shortage in the remaining part of this year, if measures to curb a trend manifested by skyrocketing prices are not put in place, a survey by The Guardian on Sunday has revealed.

The warning was sounded over the week-end by the Tandale Market Grain Sellers Association and Investment (TAMAGRAI). Tandale is the biggest market in Dar es Salaam for food cereals from upcountry.

Its Secretary General, Abdul Kambaya, told this paper that while last year some 10 trucks carrying around 100 tons of maize were being registered at the market daily, the number has presently dropped to between one and four.

He said while the hiked food prices could be linked to rising transportation costs which is attributed to global rise in fuel prices, hoarding of staple crops like rice and maize by main buyers and growers was one of the main reasons.

``These big farmers and traders want to keep their stocks to sell them at relatively higher prices in months to come when there would be great scarcity of food,`` he says.

He said the little amount being brought into Dar es Salaam now was from peasants who must sell their food to get money for their daily needs.

He also said the threat of the impending hunger in the world was also the reason for big producers to stock their food crops.

``Some countries of the world were forcing their farmers not to sell to other countries. This means that the stock of food they are keeping would fetch higher prices as they will have no other competitors,`` he said.

The TAMAGRAI secretary also attributed the shortage of food to big crop farms being converted to other farming activities like the growing of jatropha plants which are widely advocated for in the world presently.

He gave an example of many of the Mbeya farms which used to cultivate rice were now growing the plant.

He particularly cited the privatized Mbarali farm which was once one of the country`s rice-baskets, but a chunk of it was now used to cultivate other crops including that of jatropha.

Jatropha is an oil bearing plant now being advocated in tropical countries for bio-fuel production. It is also grown around crop fields and gardens to keep out animals, act as a windbreak, and to reduce soil erosion by wind and water.

``When a farm is privatized there is no way you can force the owner to grow what he does not want to grow. We have lost great amounts of rice after the privatization of the Mbarali farm,`` he says.

The other reason for the scarcity of food is that Shinyanga which is a traditional supplier of rice to Dar es Salaam has found another outlet for its products to neighbouring Rwanda.

The new outlet was because there were better roads leading to Rwanda and Burundi than those going to Dar es Salaam.

Asked if the harvesting of raw maize for roasting has affected any production, the secretary said it has not, adding that the type of maize used for roasting in Dar es Salaam would not produce any quality maize flour and the type normally grown in Iringa and Mbeya are a high-breed.

Asked if the roasting of maize should be banned, he said that would �kill� many people in urban areas as it is an income generating activity in most urban areas.

``Maize roasting has employed many people in urban areas and stopping it would mean killing these people,`` he said.

Agriculture, Food Security and Cooperatives Deputy Minister David Mathayo admitted earlier last week while launching the East African Grain Council (EAGC) in Dar es Salaam that food prices are generally higher than would be expected at this period of time especially in major urban centres, affecting low income earners in both urban and rural areas.

According to a survey by this paper the price of maize flour has gone up to 800/- a kilogramme in some places up from 400/-.

Also the prices of rice has gone up to between 1500/- and 1800/- from the ordinary 800/- and 900/-. Soya bean prices are slightly down from the 1,200/- level reached last week.

One of the highest prices ever recorded in recent years is that of dried sardines from Kigoma.

They are sold at Kariakoo market at 9,000/- per kilo, up from 3,000/-. Those from Lake Victoria are sold at 1,800/- a kilo up from 1,000/-.
 
Heshima mbele wakuu... Leo nimeiona hii kwenye The Guardian (ya Tz)......

FAO chief cautions on food crisis

2008-05-22 10:45:25
By Correspondent Edwin Agola


The Director General of Food and Agriculture Organization (FAO), Dr. Jacques Diouf of Senegal winded his two day visit to Tanzania, urging the international community to immediately address the issue of food crisis by developing the capacity in seed production.

He said his organization had sounded an alarm to international community as early as 1996 due to the declining trend of food supplies as the world headed towards the current crisis.

He emphasized irrigation at village level as a short term measure to end the crisis.

``Our Agriculture should not depend on rains, which at times are unreliable,`` he said.

Diouf stressed the importance of producing fertilizer from within the African continent as opposed to importing the soil nourishment although Africa had the raw materials.

The FAO Director General said there was need to improve the infrastructure in rural areas so that poor farmers could access to farm inputs. ``Lack of adequate storage facilities should be addressed to reduce the problem of hunger,`` he said.

He added that his organization was mandated with preparing statistics and doing the projection of what might happen. ``If we are not careful, we may have the money to buy food without having the food to buy,`` he cautioned.

SOURCE: Guardian, 22/05/2008
www.ippmedia.com


Hebu angalia alivyoviweka wazi hapo....... Na kinachonimaliza ni ile conclusion yake mwisho kabisa..... Nadhani wengi bado tuanfikiri kwa vile vijisenti tulivyonavyo tutadunda na njaa kudhania watakaoathirika ni maskini... Haya maneno hayo kutoka kwa FAO wenyewe, wanalipwa kufuatilia/kuchunguza mambo kama haya.....

Swali ni, Je Tanzania tupio tayari kwa hili?? Wengi watasema kule kusini wamevuna sana mwaka huu.....what about?
1. Storage??
2. Soko bora la nje?
3. Madawa ya kuhifadhia mazao dhidi ya wadudu waharibifu

Need I say more??
 
Morani... we ngoja tu.. watawala wetu wanafikiria mambo ya Sulllivan Summit... kama chanzo kikuu cha chakula mwaka huu. Watu watakapoanza kufa kwa njaa nitaitwa nilikula njama au nilijua kitu ambacho mtu mwingine hakujua. Inaudhi kweli.
 
KAMA MTU MVIVU SERIKALI INAANZA KUAMKA!


Serikali yapiga marufuku uuzaji chakula nje ya nchi


2008-05-23 09:33:20
Na Raymond Kaminyoge (Nipashe)


Wizara ya Kilimo na Chakula, imepiga tena marufuku uuzaji wa mazao ya chakula nje ya nchi ili kukabiliana na upungufu wa chakula nchini.

Mara ya kwanza kupiga marufuku ilikuwa Januari mwaka huu na wafanyabiashara wakaruhusiwa kuingiza mazao kutoka nje ya nchi bila kutozwa kodi lakini ni tani chache zilizoingizwa.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Peniel Lyimo, alisema jana, jijini Dar es Salaam kuwa, serikali iliondoa kodi katika uagizaji wa mazao nje ya nchi ili kuhamasisha wafanyabiashara kuingiza tani 300,000 za mahindi zinazohitajika.

``Badala ya kupata kiasi hicho, ziliingizwa tani 8,070 tu za mahindi baada ya upatikanaji wa zao hilo katika soko la dunia kuwa mgumu huku bei zikiendea kupanda,`` alisema.

Alisema hali hiyo ilisababisha nchi nyingi zinazozalisha mazao ya chakula na kuuza nje, kusitisha uuzaji wa mazao yao na hivyo kufanya hali ya upungufu wa chakula duniani kuzidi kuwa mbaya.

Aidha, Bw. Lyimo alisema kupanda kwa bei ya vyakula kumechangiwa pia na kupanda kwa gharama za mafuta hali iliyoathiri gharama katika usafirishaji.

Aliongeza kuwa gharama pia za vyakula zimesababishwa na matumizi ya mahindi katika kutengenezea nishati ya mafuta.

Aliwataka wakulima kuhifadhi chakula cha kutosha familia zao kwa msimu wote kabla ya kuanza kuuza ziada.
 
Back
Top Bottom