Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,746
- 40,899
Ndugu zangu, kuna uwezekano mkubwa kwamba itakapofika kiangazi mwaka huu, Taifa letu linaweza kujikuta kwenye upungufu mkubwa wa chakula ambao siyo tu unatishia maisha ya watu wetu bali pia unashusha hadhi na utu wa mwanadamu. Hakuna kitu kinachomdhalilisha mwanadamu na kuweza kumfanya awe mtu kama njaa.
Ni njaa ndiyo inayoweza kumfanya mtu aukane urithi wake wa kwanza kama alivyofanya Esau na ni njaa ambayo ilikuwa inatumika tangu enzi za kale kama silaha ya mwisho ya vita ambayo inalazimisha watu kusalimu amri.
Tanzania tutakabiliwa na njaa ambayo chanzo chake si ukame. Mara nyingi (kama siyo zote) njaa husababishwa na ukame na vita. Hata hivyo njaa ambayo naweza kuiangalia toka mbali na inayosogelea kama simba anyatiaye haitokani na mambo hayo bali makubwa mawili.
a. Kupanda kwa bei ya chakula duniani.
Habari za leo ni kuwa bei ya chakula duniani imepanda kwa haraka kuliko wakati wowote ule na hivyo kusababisha ugumu wa kupatikana kwa chakula. Yaliyotokea Haiti na Misri siku chache zilizopita ni dalili ya ubaya wa hali hiyo. Kwa wale walioko Dar au maeneo yenye masoko ya kudumu na kwenye mialo mbalimbali kanda ya ziwa wanaweza kutusaidia kutuambia kama kumeanza kutokea mabadiliko yanayoonekana ya bei ya chakula siku hizi chache zilizopita.
b. Mvua ya masika.
Hata hivyo naamini kwa upande wa Tanzania kitakachosababisha njaa sana ni hii mvua ambayo imeharibu mashamba na mazao ya watu kiasi kwamba baadhi ya maeneo ambayo kwa kawaida yana chakula cha kutosha yanaweza kujikuta yanahamia mwaka huu. Kama mpunga wa Kyela utakuwa umeathirika kama Dr. Mwakyembe alivyosema kwenye mahojiano yake nami kuna uwezekano kuwa Mwaka huu bei ya Mchele nayo itapanda na hivyo kufanya nafaka hiyo ianze kuwa adimu na kupatikana kwa wachache.
Maeneo ambayo mchele ndiyo chakula kikuu na pia zao la biashara watajikuta wanakabiliwa na upungufu wa fedha za kununulia hata vitu vingine na hivyo kusubiri chakula cha misaada.
Kwa vile tunajua haya yote na ziada; tufanye nini ili tujiandae na njaa ijayo?