Niwaombe viongozi wa Tanzania wapunguze picha /selfie kwenye majanga; watofautishe furaha na kilio

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,105
Viongozi wa serikali waliokwenda Hanang hakuna kazi serious waliyokwenda kufanya; Jeshi limetekeleza wajibu wakuokoa Raia viongozi wametekeleza wajibu wakupigwa picha na vyombo vya habari.

Picha za viongozi zinazosambaa zimezima kabisa coverage ya uharibifu uliofanyika. Naamini wapo viongozi wameongozana na vyombo vya habari waweze kuonekana mitandaoni . Siyo sahihi, wanaohusika na maafa watambuliwe rasmi waweze kukabiliana na kadhia kama hii inapotokea.

Nchi haina kikosi maalum au timu ya wataalam wanaoweza kusimamia maafa Nchini. Kazi hii imekuwa ni ya kila mtu hivyo response inakuwa siyo madhubuti kwa sababu it no one responsibility.

Nani anayesimamia maafa Nchini? Mkurugenzi wa maafa yupo? Au tuna mfuko wa maafa? Let us restructure our system tuunde timu ambayo itakuwa na majibu wa kurespond kwenye majanga na maafa.

Haikuhitajika Mhe. Rais atangaze kuhusu makazi ya muda, ilipaswa wawepo watu wanaojua majukumu yao kabla , wakati na baada ya janga kutokea.

Mwisho, fedha zilizotumika kupeleka viongozi Katesh ni nyingi kuliko msaada wanaokwenda kutoa. Wamejilipa mabilioni kama per diems per sector. Kesho wapo watu watabaki bila makazi na tutaambiwa serikali haina fedha za kuwajengea nyumba manusura. Na atakayetamka maneno hayo atakuwa mmoja wa viongozi waliolipwa mamilioni kufika Katesh.

Familia za viongozi Tanzania zinaishia kwa dhulma kwa kutaka au kutokutaka.
 
Viongozi wa serikali waliokwenda Hanang hakuna kazi serious waliyokwenda kufanya; Jeshi limetekeleza wajibu wakuokoa Raia viongozi wametekeleza wajibu wakupigwa picha na vyombo vya habari...
Duh!!!.....inafikirisha sana.
 
Niliwahi kuandika kuwa tuwapime mawaziri wetu kwa ufanisi wa kuleta sera mpya dhidi ya matatizo ya nchi na sio hii tabia ya kuuza sura mitandaoni.

Nampongeza Ummy Mwalimu kwa kuwezesha kuleta sheria ya bima ya afya kwa wote...hiki ndio kipimo halisi cha waziri.
 
Viongozi wa serikali waliokwenda Hanang hakuna kazi serious waliyokwenda kufanya; Jeshi limetekeleza wajibu wakuokoa Raia viongozi wametekeleza wajibu wakupigwa picha na vyombo vya habari.
mbiwa serikali haina fedha za kuwajengea nyumba manusura. Na atakayetamka maneno hayo atakuwa mmoja wa viongozi waliolipwa mamilioni kufika Katesh.

Familia za viongozi Tanzania zinaishia kwa dhulma kwa kutaka au kutokutaka.
Wapo busy kutafuta umaarufu
 
Viongozi wa serikali waliokwenda Hanang hakuna kazi serious waliyokwenda kufanya; Jeshi limetekeleza wajibu wakuokoa Raia viongozi wametekeleza wajibu wakupigwa picha na vyombo vya habari.

Picha za viongozi zinazosambaa zimezima kabisa coverage ya uharibifu uliofanyika. Naamini wapo viongozi

Familia za viongozi Tanzania zinaishia kwa dhulma kwa kutaka au kutokutaka.
Inasikitisha kuwa mpaka sasa serikali ya ccm imeshindwa kutekeleza Sendai Framework for disaster risks reduction.

(What is the Sendai Framework for Disaster Risk Reduction?)
 
Back
Top Bottom