Niwaambieni mapema tu nikija kuwa Rais wa Tanzania kwa Tiketi ya Mgombea Binafsi Daraja la 'Tanzanite' nitaamuru libomolewe haraka

Nimetafuta Mantiki ( Logic ) ya Ujenzi wa Daraja hilo mpaka sasa sijaipata sana sana naona 'Maluweluwe' tupu tu.

Nimejaribu Kuzungumza na Wakandarasi na Wahandisi Waandamizi wamesema hilo Daraja ni Kazi bure tu japo 99% walishiriki Kikamilifu katika Mchakato wake mzima mbele ya Hayati Mmoja wa Mwezi Machi na Marehemu mwingine wa Mwezi Juni.

Siku hizi huwa mnasema Sisi (akina GENTAMYCINE) Wapiga 'Kelele' Mitandaoni tukitoa 'Dukuduku' basi tutoe Suluhisho (njia mbadala).

Sasa nami GENTAMYCINE nasema nikibahatika kuwa Rais wa Tanzania kwa Tiketi ya Mgombea Binafsi hilo Daraja naamuru libomolewe kwani kuwepo Kwake hapo kwa mtazamo wangu (ambao naomba Uheshimiwe) ni 'Takataka' ndani ya Bahari.

Nitakachokifanya Mimi nikiwa Rais wa Tanzania ili Kuondoa Foleni Kubwa ya Watu wa Oysterbay, Masaki, Msasani, Kawe, Kunduchi mpaka Ununio na ikiwezekana hadi Bagamoyo kabisa ni Kuuza Madini baadhi na Ndege Mbili ambazo 'zinaduwaa' tu 24/7 pale JNIA kisha nanunua Meli za Mwendokasi kama Nne ambazo zitakuwa zinasafirisha Watu.

Akili Kubwa ambayo kidogo GENTAMYCINE ningeipongeza kwa wenye Dhamana ya Kikatiba ( japo sasa amelala Kimoja ) na Mwenzake (aliyelala nae Juzi kati hapa) ni kama ningesikia linajengwa Daraja refu la kutoka kati ya Bagamoyo hadi Zanzibar au Tanga hadi Zanzibar.

Kwa mtazamo wangu Maamuzi ya Ujenzi huu wa hili Daraja la 'Tanzanite' yalikuwa ni ya 'Kifisadi' zaidi pasipo Uhalisia na Matumizi ya Tija (Faida) kwa Watumiaji wengi na tafadhali Siku zingine tusirudie tena Kufanya Kosa kama hili kwani kwa wenye Akili timamu si tu wanatucheka bali Wanatudharau mno.

Na kabla sijasahau nikiwa Rais wa Tanzania kwa Tiketi ya Mgombea Binafsi GENTAMYCINE sitoishia tu Kuamuru 'Kubomolewa' kwa hilo Daraja la 'Tanzanite' bali pia nitaamuru upesi sana Mji Mkuu wa Tanzania ubadilishwe 'Kisheria' na Dar es Salaam ndiyo uwe Mji Mkuu na siyo huko Kijijini Mkoani Dodoma.

Ukiusoma Uzi huu na ukipandwa na Hasira nao tafadhali nakushauri tu tafuta Sumu ya Panya au ya Kunguni Unywe Ufe kabisa usiendelee Kukereka nami.

Ila nitapambana hadi Tanzania kuwe na Sheria ya Mgombea Binafsi wa Urais ambapo kwa Kipaji changu Kikubwa cha Ushawishi, Mvuto wa Kiuwasilishaji na nilivyobarikiwa na Mwenyezi Mungu 85% ya Watanzania wenye Akili Timamu (ukiachana tu na 15% wenye Uwendawazimu) watanipigia Kura.

Na hatimaye Tanzania itapata bahati nyingine ya Kuongozwa na Mzanaki kutoka Mkoani Mara (Musoma) ambapo najua baadae Watanzania wote mtaniomba niwe Rais wenu wa Milele (Kudumu) kutokana na Uongozi wangu Uliotukuka.
Wanaofikiri 'kimkakati na kiulinzi' wanakushangaa kwa kuliponda daraja hilo kwa hoja muflisi na za kisimbilisi.

Kiulinzi na usalama lazima kulihitajika kuwe na njia mbadala za kuunganisha jiji na vitongoji vyake, ili ikitokea, mathalani, daraja la selander 'likahujumiwa', kuwe na njia mbadala ya kuwezesha watu kusafiri kwenda na kutoka jijini kama kawaida.
 
Wanaofikiri 'kimkakati na kiulinzi' wanakushangaa kwa kuliponda daraja hilo kwa hoja muflisi na za kisimbilisi.

Kiulinzi na usalama lazima kulihitajika kuwe na njia mbadala za kuunganisha jiji na vitongoji vyake, ili ikitokea, mathalani, daraja la selander 'likahujumiwa', kuwe na njia mbadala ya kuwezesha watu kusafiri kwenda na kutoka jijini kama kawaida.
Madaraja hayajengwi kwa ulinzi tu, hoja hapa ni position yake pamoja na traffic conveyance efficaccy.
Soma post yangu no.13.
 
Back
Top Bottom