Ni baadhi ya mabaki tu ndio yapo na hayapo kileleni kabisa mlima kilimanjaro una vilele viwili kibo na mawenzi kibo ndio kilele kirefu hivyo vilele vimetengana kidogo kutoka mawenzi hadi kibo kuna uwazi na tambarare flani hivi so hapo kwenye hiyo tambarare ndio kuna baadhi ya masalia ya ndege huwezi kuyaona kirahisi mimi niliyaona kwa juhudi binafsi kwakua hayapo njiani ili kuyaona unatembea umbali kidogo kutoka camp ili kuyafikia na kuhusu ndege kuvutwa sina uhakika kwakua nilishuudia ndege zikiruka karibu na kilele lakini siyo kila kipindi kuna vipindi maalumu wakati ambapo hali ya hewa inaruhusu hata hiyo ndege ilianguka kutokana kuchafuka kwa hali ya hewa