Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
10,434
Reaction score
17,203
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia.
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Mbona inasemekana kuwa mziki mzuri unapatikana kwenye 2 channel?
Mziki umekuwa sana, development imefanyika kubwa kwenye eneo la digital sound processing, usikariri sana mambo ya Hi Fi., kama umewahi kutumia avr ya 5-9 channel ukaja ukasikiliza mziki kwenye 2 channel utaona tofauti kubwa sana, especial kwenye live recorded music ambazo kwa sasa sisi wasikiliza gospel,regggae au kwa.mtu yeyote anayependa live music, kwenye 2 channel kuna vitu hutavipata kabisa, ila kama unasikiliza hii miziki ya kupika studio na FL studio au cubase huwezi ona
 
Mziki umekuwa sana, development imefanyika kubwa kwenye eneo la digital sound processing, usikariri sana mambo ya Hi Fi., kama umewahi kutumia avr ya 5-9 channel ukaja ukasikiliza mziki kwenye 2 channel utaona tofauti kubwa sana, especial kwenye live recorded music ambazo kwa sasa sisi wasikiliza gospel,regggae au kwa.mtu yeyote anayependa live music, kwenye 2 channel kuna vitu hutavipata kabisa, ila kama unasikiliza hii miziki ya kupika studio na FL studio au cubase huwezi ona
Upo sahihi na kupitia maelezo yako naweza kuhitimisha kuwa;
Hi-Fi stereo ni bora kwa purists wanaotaka sauti safi, ya asili, na ya moja kwa moja.
AVR na multi-channel ni bora kwa lve music, sinema, na immersive experiences hivyo
Aina ya muziki, mazingira ya kusikiliza, na ladha binafsi vinaamua zaidi kuliko teknolojia pekee.
 
Upo sahihi na kupitia maelezo yako naweza kuhitimisha kuwa;
Hi-Fi stereo ni bora kwa purists wanaotaka sauti safi, ya asili, na ya moja kwa moja.
AVR na multi-channel ni bora kwa lve music, sinema, na immersive experiences hivyo
Aina ya muziki, mazingira ya kusikiliza, na ladha binafsi vinaamua zaidi kuliko teknolojia pekee.
Kwenye avr kuna kitu kinaitwa pure direct, yaani mziki unaupata kama ulivyo, natura kabisa tofauti na Kwenye Hi Fi , kwenye hi fi kuna pre amp ambazo wakati mwingine zina vitu vya ziada ambapo bado mziki hauwi natural kabisa
 
Nilikuwa nimeacha kutumia kwa muda wa miezi 6 seapiano ( 1002) nimefika kuliwasha hali' connect bluetooth wala port ya flash haifanyi kazi. Shida itakuwa ni nini?
Mp3 inashida.
Mpe fundi yoyote akuchekie,au akuwekee nyingine

Je ile port ya flash ukichomeka usb inachaji simu?
 
Wharfedale Atlantic 400 front Na onkyo sorounds, sub natumiela infinity tss1200
Kwahiyo kwa sasa huna amplifier?, hizo front speakers zako unauza?.

Pia natafuta fundi mzuri, ambaye wanaweza nibadilishia surround foam/ile rubber ya speake inayoshika cone na frame. Nina speaker ya mid kwenye tower speakers imechanika/imekatika kutokana na uchakavu nadhani.
 
Back
Top Bottom