Ni kweli, Ukilinganisha Tz na US, ni neema kwako kuwa US.. Sikupinga hilo, wala hali ya wakimbizi waishio nje ya Tz.
Lakini ukionesha kuwa huna lolote la kushukuru Tz, hiyo Inaitia ukakasi, licha ya kwamba sikulazimishi, ni hulka ya mtu binafsi.
Nilichopinga ni ulivyosema rekodi ya MTz huko USA sio nzuri, kujihusisha madawa ya kulevya n.k.
Huajiriwi au kupangisha kiholela huko US (wa Mexico kibao wanafanya hivyo) ndivyo utaratibu wao, wa Tz ilikuwa ni kuwadhibiti wakimbizi kutokufanya yote uliyoyaeleza. Ukiacha wakimbizi watoke kambini au wafanye biashara, wakati huna jinsi ya kuwafuatilia popote walipo, kwa yeyote mwenye akili timamu hawezi kufanya hivyo.
Kupewa social security card, green card na baadae pasi ya kusafiri ukiwa raia wa US, ni jinsi ya kukudhibiti kila ufanyalo. Tz hatukuwapa hayo kwa kuwa mlikuwa njiani kwenda popote kwenye neema. Mlivyofika Marekani, hamkuachiwa kwenda mitaani tu bila utambulisho wowote, mnadhibitiwa kwanza kwenye mifumo wao, halafu ndio unaruhusiwa kufanya shughuli zako.
Tz pia ndicho walichofanya, na nchi yoyote yenye serikali/ utawala ndivyo ifanyavyo.
Kila la Kheri katika maisha ya neema huko Marekani!
Sent using
Jamii Forums mobile app