Ni kweli kuwa watu wa DUCE wana hofu sana shule, muda mwingi hupenda kukaa vimbwetani hata kama hawana shughuli ya muhimu. Hasara wanayaoipata kwa kufanya hivyo ni kutopata uzoefu wa maisha ya jiji. Kwa wanaokaa hostel za ndani ndo hupata athari zaidi maana wao huishi kama vile ni form 7. Wamalizapo chuo hawana plan yoyote zaidi ya kurudi nyumbani kusubiria baraka za Mola ziwape mema. Pili watu wa DUCE ni wasomaji sana wa madaftari ya notes, hawana muda wa kutumia mtandao wala PC, nadhani ndo chuo ambacho kinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wasiojua kutumia kompyuta. Kwa mwaka mnaoanza kuna mazuri yaliyopo DUCE kama vile uungwana katika mavazi, uzingatiaji wa dini na uaminifu katika mahusiano, hizo ndo tunu za DUCE mzifuate mnufaike. Masomo zingatia sana hakikisha unapambana GPA yako iwe juu ya 3.5. Tembea mjini ujue k/koo, posta, mwenge, kurasini, k/ndoni. Husiana na marafiki nje ya wanafunzi ili uwe na picha nzuri ya maisha. KARIBUNI DUCE, KISIWA CHA USTAARABU.