Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

Mkuu mbona kuna watu kibao tu wamebadili dini kutoka uislamu na kuwa wakristo na hawajafanywa kitu wanaishi maisha yao kama kawaida au hujawahi kuona?
Labda Tanzania, ila kwa nchi nyingi ambazo ni Muslim majority kubadili Dini ni kosa la jinai ambalo adhabu yake huweza kuwa hata kifo
 
Atheist ni wakristo ambao wanapesa mingi ivyo kiburi cha pesa na sayansi ndio kinakuwa ivyo. Wakifirisika wanarudi kwenye dini
Mi habari za Dini nimeachana nazo nikiwa Sekondari na sikuwa na hela
 
Kama simu imetengenezwa haimaanishi aliyetengeneza alijitengeneza

Kama dunia na vinginevyo viliumbwa haimaanishi aliyeumba alijiumba au haitaji muumbaji

Ukisema muumbaji wa ulimwengu hana muumba unakua huna tofauti na anayekubali simu ina mtengenezaji ila ulimwengu hauna muumbaji
Kila kitu kina mwanzo wake ila kiakili lazima kiwepo kisicho na mwanzo ambacho ndio chanzo cha vitu vyote,bila ya hivyo basi kusingekuwa na chochote maana ili kipatikane kitu lazima kiwepo chanzo.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hapa uliambiwa ofsini leteni cheti cha ndoa ili uandike madai kuwa una mke baada ya kulipoti kazini,
Kuna masuala ya bima, likizo, posho mbalimbali na likizo pia mkuu, ukiwa kwenye ndoa (hasa mke) unakua na advantage kubwa kuliko ambaye hajaolewa
 
Kila kitu kina mwanzo wake ila kiakili lazima kiwepo kisicho na mwanzo
logical fallacy of special pleading

unatengeneza kanuni ambayo kimsingi ipo universal (kila kitu) kua lazima kiwe na chanzo. Kisha mungu awe ndio chanzo cha vingine halafu yeye asiwe na chanzo

In such an assertion, either God must have His own source or creator, or else the universal principle of everything having a source or creator must be set aside
ambacho ndio chanzo cha vitu vyote,bila ya hivyo basi kusingekuwa na chochote maana ili kipatikane kitu lazima kiwepo chanzo.
huu ni uwongo, nini chanzo cha mungu?
 
Wote tumezaliwa tukiwa atheist, dini tulikuja kuzifata baada ya kuja kuwa indoctrinated

Mtu kuwa atheist haimaanishi kabadili asili yake bali kairejea asili yake ambayo mwanzo aliikacha
Sasa mtoto mdogo wa kuzaliwa leo anawezaje kuwa na msimamo wa kwamba hakuna Mungu?
 
Nami naona hivyo, japo sipo upande wowote wa hizi dini kuu bado nina falsafa yangu, naamini katika upendo kwa watu wote na viumbe vyote
Binaadamu tunatofautiana na ndio maana kuna watu makatili wanauwa wenzao na kuna wanadhurumu wenzao,je hao watu utadeal nao vp kwa mujibu hiyo dini yako?
 
Tembelea channel ya Davistar Mata
Youtube uone mikasa ya watu hasa ya kichawi na jinsi walivyookolewa labda utaamini uwepo wa Mungu na Mungu ana nguvu kiasi gani.

Ukweli ni kwamba Mungu yupo na shetani yupo pia.Sisi wanadamu ndio uwanja wa mapambano baina ya hizi nguvu mbili. Mawazo uliyonayo kuwa hakuna dini(Mungu) si yako bali ni ufahamu wa kipepo ndo umekufunga. Usichukulie poa
Masimulizi yanaweza kutungwa tu mkuu, anyway mimi sio muumini wa Ukristo wala Uislam au dini nyingine kuu
Lakini Nina independent philosophy yangu nikiamini kuwa kila binadamu anapaswa kumpenda binadamu mwingine na viumbe wengine, wanaaonyesha upendo huo wanakuwa rewarded na 'Mamlaka nyigine iliyo Juu' ambayo unaweza kuita mungu or whatever
 
Nna kesi kama yako mkuu,
Ila naamini mungu yupo lkn siamini dhehebu lolote lile wala kitabu cha dini chochote hapa duniani...

Nna kesi kubwa sana na mke wangu ya kukataa kubatiza watoto, sijui tunaimalizaje naoana wakwe nao wanaleta habari zisizoeleweka.
Mi mtoto abatize tu ila Mimi aniache huru
 
Comments zako nyingi za kuhusu Islam's ni za kuukejeli why?

Maisha hayapo hivyo boss jifunze kuheshimu Imani za watu.
Tuanze na Huu uzi wapi nimekejeli?Usilete story za uzi ule na ule wa siku ile kwanini usingeniambia hukohuko?Tuanze hapa hapa
 
Sasa mtoto mdogo wa kuzaliwa leo anawezaje kuwa na msimamo wa kwamba hakuna Mungu?
atheism ni absence or lack of belief wakati theism ni kinyume chake, sasa huyo mtoto anawezaje kua na dini au imani ya uwepo wa mungu?
 
Back
Top Bottom