Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

Wakuu habari,

Mimi ni siamini kuhusu masuala ya dini, ila naamini binadamu tunapaswa kuishi kwa upendo kati yetu na tuwapende pia viumbe wengine, naamini hii ndio 'perfect' na 'universal dini'.

Matatizo kama vita, njaa, mauaji, talaka, pengo kati ya matajiri na masikini n.k vyote hivi tungevipunguza kwa kiasi kikubwa kama tungezingatia hii 'universal dini' zaidi kuliko nyingine

Mke wangu ni mtu wa Dini sana, ametokea familia ya walokole.

Amekuwa akinisumbua kuhusu kwenda kanisani kila mara, nimekuwa nikimpa visingizio vya hapa na pale ili nisiende naye kanisani, ila naona visingizio vimeisha.

Sasa nimechoka kelele za kuhusu kanisani, nafikiria nimchane kuwa siamini masuala yake ya kanisani na sitaki usumbufu tena.

Nitakuwa harsh sana au kuna mbadala wa kuyamaliza?
[emoji23][emoji23]japo nimegoogle kujua maana ya huo msamiati,,,naona kabisa hujui unachokiongea ndg yng.
 
Kwahyo mtoto aliyezaliwa leo anaamini uwepo wa Mungu?.
Kuwa atheist sio lazima uwe na msimamo Hakuna Mungu hata kutoamini uwepo wake either kwa kutokujua pia ni Atheism.
Chukulia mtoto azaliwe na akulie porini na wanyama..Je dini yake itakuwa ipi?Uislam au Atheism?
Mtoto mdogo aliyezaliwa leo hatuwezi kusema anamuamini Mungu au anamkana Mungu kwa sababu hana uelewa wa kupambanua lolote na wala haelewi chochote katika hayo.

Kwa kujibu hilo swali lako, ni kwamba imani ya uislamu humtambua mtoto yeyote yule anapozaliwa tu ni muislamu kwa maana ndio asili mpaka atakapo kuja kuamini tofauti na imani ya kiislamu.
 
Atheism sio kupinga Hakuna Mungu tu ni ile kutokuwa na imani ya uwepo wa Mungu.
Lack of beleif in God not the Beleif that there is No God.

Sasa kwa mujibu huo,mtoto mdogo ambaye analack beleif in God ni atheist.

Kuhusu uislam kwani Muislam ni nani?
 
Wakuu habari,

Mimi ni siamini kuhusu masuala ya dini, ila naamini binadamu tunapaswa kuishi kwa upendo kati yetu na tuwapende pia viumbe wengine, naamini hii ndio 'perfect' na 'universal dini'.

Matatizo kama vita, njaa, mauaji, talaka, pengo kati ya matajiri na masikini n.k vyote hivi tungevipunguza kwa kiasi kikubwa kama tungezingatia hii 'universal dini' zaidi kuliko nyingine

Mke wangu ni mtu wa Dini sana, ametokea familia ya walokole.

Amekuwa akinisumbua kuhusu kwenda kanisani kila mara, nimekuwa nikimpa visingizio vya hapa na pale ili nisiende naye kanisani, ila naona visingizio vimeisha.

Sasa nimechoka kelele za kuhusu kanisani, nafikiria nimchane kuwa siamini masuala yake ya kanisani na sitaki usumbufu tena.

Nitakuwa harsh sana au kuna mbadala wa kuyamaliza?
Challenge dini yake taratibu na siyo kumwambia msimamo wako , kwani ukishamwabia we ni atheist utaanza kuubiliwa kwa nia ya kutaka kukurudisha kwenye dini.

Watu wa dini huwa bado hawana uwezo wa kuona mtazamo wako.

fanya taratibu ujielezee mtazamo wako, muulize maswali tata kuhusu mtazamo wake wa dini.

tumia falsafa na science kumuonesha ukweli.

Mi huwa sisemi ni atheist kwa fundamentalist, ila taratibu nawachallenge kwenye maswala ya dini mpaka wananielewa na wengine kujiunga nami.
 
Na huyo muumbaji aliumbwa na nani...?
Nionyeshe kwanza haja ya muumba na yeye kuwa ameumbwa ? Yaani ulazima wa muumba kuwa na yeyw kaumbwa. Nini namaanisha hapa, ni kiwa nikikwambia Mola ameumbwa kuna mawili, ambayo kwayo pia hayawezekani :
1. Utauliza na yeye aliye muumba na yeye kaumbwa na nani ? Hapa kutakuwa na jambo ambalo halithibitishiki na halipo lile watu wa hesabu husema "Infinity Series".

2. Nitakuuliza kwanini Muumbaji unaulizia kaumbwa na nani ? Na huyo aliyemuumba ni nani ?

Kisha hiyo chain, uniambie ukomo wake ni wapi ? Na je kisicho mpaka kipo ukiacha Mola muumba ?
 
Atheism sio kupinga Hakuna Mungu tu ni ile kutokuwa na imani ya uwepo wa Mungu.
Lack of beleif in God not the Beleif that there is No God.

Sasa kwa mujibu huo,mtoto mdogo ambaye analack beleif in God ni atheist.

Kuhusu uislam kwani Muislam ni nani?
Atheism inatokana na kutambua kwa kutokuwa na ushahidi wa ki-science wa kuwepo kwa mungu.

basically, hakuna ushahidi wa ki-historia, biologia, physicia, wala chemia kuhusu uwepo wa mungu.

hivyo, mpaka mtu atakapotoa ushahidi tosha, atheist tutaendelea na mtazamo wetu.

kama mtu akidai itu bira ushahidi, basi waweza kuping dai lake bila ushahidi
 
atheism ni absence or lack of belief wakati theism ni kinyume chake, sasa huyo mtoto anawezaje kua na dini au imani ya uwepo wa mungu?
Hatuwezi kusema mtoto mdogo anaamini au haamini kwa sababu bado hana utambuzi wa lolote kati hayo mambo,hakuna chochote anachoamini au haamini/kukana.
 
Unaweza ukaamini kitu ambacho hukijui?
 
Atheism inatokana na kutambua kwa kutokuwa na ushahidi wa ki-science wa kuwepo kwa mungu.

basically, hakuna ushahidi wa ki-historia, biologia, physicia, wala chemia kuhusu uwepo wa mungu.

hivyo, mpaka mtu atakapotoa ushahidi tosha, atheist tutaendelea na mtazamo wetu.

kama mtu akidai itu bira ushahidi, basi waweza kuping dai lake bila ushahidi
Unafikiri ni kipi kinaweza kuwa ni ushahidi wa uwepo wa Mungu? Kwa sababu kwa navyoelewa mimi hauwezi kutaka ushahidi wa jambo hali ya kuwa hina hata idea huo ushahidi wa hilo jambo unafananaje.
 
Hao wote wana matatizo ya akili, kama wanakubali simu imetengenezwa na kuwa hivi ilivyo, vipi Dunia na vinginevyo visiwe na muumbaji ? Hizi akili wanazitumia vibaya sana, ila bishara mbaya kwao.
una ushahidi gani dunia imetengenezwa na muumbaji?

Ushahidi wa geography na astrophysics unaonesha jinsi dunia ilvyo jengeka kutokana na gravitational pull miaka 4.5 billion years pamoja na jua
kabla ujaanza kubisha kuhusu hili, jua kwamba Science hii ndio inayoendesha satellite na technology zote tunazotumia kubishana hili swala.

kiuwepesi, jinsi maji, mawe, hewa zilivyoweza kuwepo duniani imejurikana mda mrefu sana; sema tu wengi hatusomi vitabu
 
Unafikiri ni kipi kinaweza kuwa ni ushahidi wa uwepo wa Mungu? Kwa sababu kwa navyoelewa mimi hauwezi kutaka ushahidi wa jambo hali ya kuwa hina hata idea huo ushahidi wa hilo jambo unafananaje.
kama hakuna shida ya ushahidi, basi mi ninaweza kusema kwamba mungu hayupo ua mungu ni mchaga na nikawa sahihi

kwani una ushahidi gani mi sipo sahihi?

bila kuwepo na kipimo chochote inafanya kila kinachosewa kuwa sahihi
 
Nionyeshe kwanza haja ya muumba na yeye kuwa ameumbwa ? Yaani ulazima wa muumba kuwa na yeyw kaumbwa. Nini namaanisha hapa, ni kiwa nikikwambia Mola ameumbwa kuna mawili, ambayo kwayo pia hayawezekani :
1. Utauliza na yeye aliye muumba na yeye kaumbwa na nani ? Hapa kutakuwa na jambo ambalo halithibitishiki na halipo lile watu wa hesabu husema "Infinity Series".

2. Nitakuuliza kwanini Muumbaji unaulizia kaumbwa na nani ? Na huyo aliyemuumba ni nani ?

Kisha hiyo chain, uniambie ukomo wake ni wapi ? Na je kisicho mpaka kipo ukiacha Mola muumba ?
dah, waonee huruma
haya mambo ya philosophy si mepesi kwa watanzania..dah.. 😂
 
Atheism sio kupinga Hakuna Mungu tu ni ile kutokuwa na imani ya uwepo wa Mungu.
Lack of beleif in God not the Beleif that there is No God.

Sasa kwa mujibu huo,mtoto mdogo ambaye analack beleif in God ni atheist.

Kuhusu uislam kwani Muislam ni nani?
Kama ni hivyo basi itabidi kuwe na tofauti kati kutokuwa na imani na kuchagua kutokuamini/kupinga,yani kama mtoto anapozaliwa anakuwa hana imani ya Mungu na ni kwa sababu hana uelewa ila baadaye anapokuwa anakuja kuelewa habari za kuwepo Mungu,mpaka hapo atachagua kuamini au kutokuamini/kukana. Sasa sidhani kama itakuwa sawa kwa mtoto asieelewa kuwekwa kundi moja na anaelewa ila kachagua kutokuamini.
 
una ushahidi gani dunia imetengenezwa na muumbaji?

Ushahidi wa geography na astrophysics unaonesha jinsi dunia ilvyo jengeka kutokana na gravitational pull miaka 4.5 billion years pamoja na jua
kabla ujaanza kubisha kuhusu hili, jua kwamba Science hii ndio inayoendesha satellite na technology zote tunazotumia kubishana hili swala.

kiuwepesi, jinsi maji, mawe, hewa zilivyoweza kuwepo duniani imejurikana mda mrefu sana; sema tu wengi hatusomi vitabu
Ndugu msomi naomba niku ulize swali moja, kwa mujibu wa maelezo yako ni kwamba ilianza dunia ndio wakaja viumbe si ndio?
 
Hatuwezi kusema mtoto mdogo anaamini au haamini kwa sababu bado hana utambuzi wa lolote kati hayo mambo,hakuna chochote anachoamini au haamini/kukana.
Kama hana utambuzi utasema ana imani ya uwepo wa mungu?

Imani ya uwepo wa mungu ni mpaka ufundishwe lakini ukosefu wa imani haufundishwi

Atheism ni lack of beliefs so mtoto hana utambuzi hivyo ana lack of belief
 
Kama ni hivyo basi itabidi kuwe na tofauti kati kutokuwa na imani na kuchagua kutokuamini/kupinga,yani kama mtoto anapozaliwa anakuwa hana imani ya Mungu na ni kwa sababu hana uelewa ila baadaye anapokuwa anakuja kuelewa habari za kuwepo Mungu,mpaka hapo atachagua kuamini au kutokuamini/kukana. Sasa sidhani kama itakuwa sawa kwa mtoto asieelewa kuwekwa kundi moja na anaelewa ila kachagua kutokuamini.
Atheist wote hawana imani na uwepo wa Mungu hilo ndo main kundi..
Ndani yake sasa kuna wanaopinga uwepo wake
Kuna ambao hawaelewi/Hawajawahi kusikia habari za Mungu na
Kuna ambao hawaamini yupo lakini pia hawapingi uwepo wake yani simply they dont care awepo asiwepo kwao ni insignificant..
 
Back
Top Bottom