Nitakuwa salama na T-Shirt za Mbowe?

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,772
2,171
Tukio la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh Freeman Mbowe na kushitakiwa kwa kosa la ugaidi limevuta hisia
za watu wengi ndani na nje ya nchi.

Suala hili limegusa pia hisia zangu hasa nikitafakari kwamba amekamatwa masaa machache tu kabla kuhudhuria kongamano la katiba.

Kwa upande mwingine ni vizuri kwamba kesi hii itaanza kusikilizwa hivi karibuni ili kila upande utoe ushahidi wake utakaoiwezesha mahakama kutoa uamuzi wake.

Wakati haya yanaendelea, nimepanga kuchapisha T-shirt kama 15,000 zitakazokuwa na maneno "TUMWOMBEE FREEMAN MBOWE"
na kugawa bure T-shirt hizo kila wilaya katika ofisi za CHADEMA.

Je, nitakuwa salama na zoezi hili hasa ukizingatia kwamba wakati wa jaribio la mauaji yaTundu Lissu watu waliovaa T-shirt kuhusu TL walikamatwa na kuwekwa mahabusu!
 
Mimi nimechora kwenye magari ya Magereza halafu wewe unaogopa vitu vidogo vya T- Shirt?

20210809_.jpg
 
Lazima umfuate jela Mbowe. Achana na kitu ambacho hakikuongezei shibe katika maisha yako
 
Ungeandika kwenye magari ya PT
Hao magereza umewaonea tu.
 
Bila shaka utaenda kuunganishwa katika kesi tajwa kama mtuhumiwa na 2.😂
 
Tengeneza alaf uende makao makuu ya polisi umgaie IGP akipokea njoo unigaie na mimi
 
Fanya hivyo...chapisha T shirt hizo uone Kama utakamatwa au vipi
 
Acha kucheza na maisha ndugu yangu.

Pamoja na kupiga kelele za hapa na pale mitandaoni lakini tujue kwamba tuna familia zinatutegemea ktk mzunguko wa maisha, not a community to impress.

Usiige aina ya siasa za kiwehu kama Mdude aliyehenya siku 400 mahabusu alafu katoka anakuta familia yake imeparanganyika, biashara zake zimekufa.

Kaenda kwa Mbowe ampige tafu kaambiwa chamani mambo si mazuri hakuna ruzuku tena labda atafikiriwa kwenye tuposho akiwa anazurula mikoani kwenye makongamano ya katiba,,, bahati mbaya hata makongamano yameingia ruba.

Serikali ni dubwana la kuchunga sana, nenda kwa tahadhari sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom