Mfikirishi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,339
- 13,643
sisi tunawashukuru Wajerumani kutuletea Lutheran church,machame yote ni walutheri,ingekuwa siyo wakoloni inawezekana kilimanjaro yote ile ingekuwa kama Tanga vibaghashia kila kona,Thank you Jesus
sisi tunawashukuru Wajerumani kutuletea Lutheran church,machame yote ni walutheri,ingekuwa siyo wakoloni inawezekana kilimanjaro yote ile ingekuwa kama Tanga vibaghashia kila kona,Thank you Jesus
Kwa hiyo shukrani zako za mwendea Yesu au mjerumani??sisi tunawashukuru Wajerumani kutuletea Lutheran church,machame yote ni walutheri,ingekuwa siyo wakoloni inawezekana kilimanjaro yote ile ingekuwa kama Tanga vibaghashia kila kona,Thank you Jesus
Na pamoja na yote haya kuna wafuasi wake wengi tu ambao kwao kila analosema Ndugu Prof. ni reflection ya Watanzania walio wengi!
Rais amesema ukweli!!!!!!!!!!!!! Wakoloni walituletea mambo mengi sana mazuri mfano, mashamba ya mikonge; Reli, Miundombinu ya maji, barabara nk. Pia walitutaka tufanye kazi kwa kutulazimisha........Yaani ni lazima ulime hekari tatu heka moja ya zao la biashara ya kwako, heka moja ya zao la biashara ya mkoloni na heka moja ya chakula ya kwako. Ni lazima kama minimu requirement.
Ukikutwa uko nyumbani kipindi cha kilimo ni lazima uwe na sababu za kutosha kwanini hukwenda shamba. Uwe na sababu kwa mfano u mgonjwa na cheti cha daktari uwe nacho. Huna unakula viboko!!!! Yaani walitulazimisha tufanye kazi kwa manufaa yetu na yao wao wenyewe.
Nini chanzo cha kudai mkoloni anatunyonya?
Ni Uvivu wetu......................!
Baada ya kuona tunalazimishwa utamaduni wa kuwa bize wakati wote na kwa kuwa sisi tumezoea kupiga domo muda mwingi na kukaa vibarazani kutwa nzima tukaona mkoloni kwa kutufanya tuwe bize anatunyanyasa.......Ule usiriaz wa mtawala anaostahili kuwa tukaona kero. (Siku hizi mtawala mzuri ni yule anayekwambia we kaa tu nitakuletea kila kitu; kuanzia mvua, mashamba, mazao, mashine ya kuvunia, ajira, vyandarua nk.)
Wanadai ujira aliokuwa anautoa mkoloni ulikuwa mdogo (ilikuwa minimum wage) lakini leo hii the so called minimum wage sijui hata kama inatosha. Ni heri kuwa fundi baiskeli utaziba pacha na kupata pesa nyingi kuliko mshara huo wa kima cha chini. Ndo wakaona anatunyonya! Wakaanzisha harakati za ukombozi.........
Lakini baada ya kupata uhuru hakuna hata barabara moja tuliyoianzisha zaidi ya zileziel alizozi "design" mkoloni. Reli hatuna mpya zaidi ya ile ya mkoloni (TAZARA labda) na hata hizo reli zimebakia historia tu.
Watu hawapendi kufanya kazi za mikono ama mitulinga. Wanataka kufanya kazi za kudanganya wenzao kisha wapate pesa. Ajira siku hizi inatafsriwa ni kuajiriwa ofisini na ukifika huko ni kupiga dili tu na wala si kufanya kazi.
Watawala wetu wanashindwa kutusimamia tupendekufanya kazi kwa sababu kuu mbili, kwanza wakisema hivyo watakuwa kama alivyofanya mkoloni hivyo kuogopa kuitwa na wao wakoloni, pili wanaogopa wakati wa uchaguzi watakosa kura maana watanzania tunapenda mtu anyesema nitajenga reli ama nitanunua ndege wakati hizo zilizopo hata ukarabati tu umeshindikana.
Maisha aliyokuwa akiishi mkoloni akiwa nchini kwetu akitutawala ndo yaleyale anayoishi hata kwake na maendeleo yake yamepaa.
Watakuja wanahistoria na wanasiasa waliopotoshwa na historia watasema mkoloni alikuwa mbaya maana alipora rasilmali zetu. Waulizeni ni rasilimali gani alizopora maana mkonge alipanda yeye na malighafi zingine. Muwaambie sasa hivi ndo tunaporwa rasilmali zetu maana hatuna hata mtambo mmoja uinaochimba madini kwa niaba ya serikali. Mitambo yote ni ya wageni na rasilmali zote zinazopatikana ni za kwao....Sisis twwambulia the so called ROYALTY ambayo haizidi asilimia tano. Uporaji mkubwa kushinda enzi za mkoloni .
Watakuja wataalamu wa gesi na mafuta watasema serikali inachimba gesi kupitia shirika la petroli Tanzania (TPDC) waambieni PSA (Production Sharing Agreements) zina kasoro. Gharama za uchimbaji gesi na mapato wanagawana kama ifuiatavyo TPDC 20% na Mwekezaji 80% lakini mwisho wa siku kodi anayechanga asilimia 20 ndo analipa kodi. Pia gharama za uchimbaji zinapelekwa mbele (costs are capitalized and losses are carrief foraard indefinetelly) Maana yake ni kwamba makampuni yakianza uzalishaji gharama zilizotumika kutafiti mpaka kuzalisha gesi ama mafuta zitatolewa kwenye mapato baada ya kuanza kuuza gesi. Mrundikano wa gharama hizo mpaka uishe ndo kampuni ya gesi ianze kulipa kodi. Sisi wataalamu wa fedha uchumi na uhasibu tumepiga hesabu itachukua miaka hamsini kwa kampuni ya gesi kuanza kulipa kodi. Hayo maendeleo ya gesi yatawanufaisha wawekezaji sisi tutanufaika labda na gharama za nishati kushuka na bei za bidhaa kushuka viwandani maana vitatumia gesi. Napo pia tujiandae maana gesi inaweza kufanyiwa biashara na wakubwa mpaka tutachanganyikiwa!!!!! Kila mkubwa ataingiza vikampuni vyake kwa kisingizio cha kutoa huduma ama mkataba wa kuhesabu gesi inayozalishwa........! .kisha akadai mamimilioni ya dola hatimaye yakasababisha bei za vitu kutoshuka maana inakuwa ni gharama kwa mwekezaji kuwalipa wakubwa gawio la mikataba ya "kuhesabu gesi iliyozalishwa......."
Angekuwapo mkoloni sasa hivi tungekuwa na barabara za ghorofa......
Faida za uhuru ni nyingi kubwa ni pale wananchi wanaweza kufanya jambo lolote bila kuchukuliwa hatua yoyote. Hayo ndo matunda ya uhuru.
Uhuru ulitokana na mawazo ya ku-"exercise practically the knowledge acquire in the class". kifupi uhuru ni theoretical ideas. Huwezi ukapata maendelo kwa kuchagua serikali kila baada ya miaka mitano na atakayekuja anakuja na mawazo yake binafsi na si sera ya taifa. Umaskini wa wananchi uwe ndo kigezo cha kuchagua Rais bora eti kwa matarajio ya kuja kuondosha umaskini wetu.......? hapana hiyo siyo sera na maendeleo kwa mtindo huo ni ndoto. Nawaambia hivi, kama kuna kijana kajiunga na mitandao ya kijamii akiwa na miaka ishirini nina hakika atafikisha umri wa kustaafu utumishi wa umma akiwa mchangiaji mzuri kwenye mitandao bila kuyaona haya maendeleo tunayoyataraji. Ni theoretical tu!!!!
Watanzania hawapendi viboko wakadai uhuru bila ya kujua madhara yake ambayo ni kuteswa na vyombo vya dola magerezani ama kulala na njaa kwa kutegemea mtu aliyeko madarakani akuletee chakula ama akupe kazi utakayoifanya ukipiga blabla tu kisha mshahara burungutu .
bila ukoloni tungekuwa ma bush man kama wa hazabe vile au masai hatuna dira,kila kitu kinatokea kwa sababu,elimu ya zamani ilikuwa jando tu na unyago sasa hivi mnapata elimu dunia.
Kikwete yuko sawa ila hakutakiwa kulopoka hivyo maana aibu
Tena licha ya Ikulu, Mjerumani kafanya kweli, reli ya kati mpaka leo.
Barabara karibu zote unazotumia leo ni zile zile za Mjerumani, sanasana tumezipanuwa na kuweka lami.
Nenda Tanga, moja katika miji ambayo imepangika vizuri na hiyo ni toka Mjerumani, si leo.
Ukweli ubaki kuwa ukweli. Natamani tungebaki kutawaliwa na Wajerumani hadi leo hii. Hatuwezi lolote.
kha,semaaa usiooogope semaaa.sisi tunawashukuru Wajerumani kutuletea Lutheran church,machame yote ni walutheri,ingekuwa siyo wakoloni inawezekana kilimanjaro yote ile ingekuwa kama Tanga vibaghashia kila kona,Thank you Jesus
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Profesa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa kututawala na kutuletea maendeleo wakati wa ukoloni.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ikulu jana, Rais Kikwete alimuambia Rais wa Ujerumani kwamba wakati wanatutawala walitufanyia mambo mengi sana mazuri ikiwemo kutujengea jengo la ikulu ambalo tunalitumia hadi sasa.
Sawa nyani Komiri, mimi ni Mtanzania hata bila mkoloni tungechomoza tuu. Tungeweza kuchelewa, lakini tungechomoza zaidi yatulivyo sasa ambapo ccm imetuingiza kwenye ukoloni mamboleo. kumbuka Mungu aliye hai hana upendeleo.
kwa mujibu wa historia walioleta dini ya kiislam hawakuacha maendeleo zaidi ya ulalamishi na ugaidi.hawa wengine kikwete kawapa heko
Tena ninatamani aingie nao mkataba wa kuimarisha idara za serikali kama polisi. Kwamba Jeshi la polisi liwe chini ya serikali ya ujerumani kwa miaka kadhaa ili warudishe hadhi kama walioyoicha.
Na wewe ulikuwa unafundisha hayo kwa mtaala gani?
Lakini huwa unakumbuka kuwafundisha wanafunzi wako how ccm is under developing Tanzania?
Kushuka kwa elimu ya Tanzania ni sababu ya Wajerumani pia?
Kukithiri kwa matendo ya rusha na ufisadi napo ni ajili ya wajerumani?
Huduma mbovu za jamii, ukiukwaji mkubwa wa katiba na haki za binadamu nazo ni za wakoloni?
Matumizi mabaya ya raslimali za taifa na lack of accountability nayo ni wajerumani?
Ndiyo maana kuna shida kubwa sana kaika kuinua elimu ya Tanzania. Kumbe hata wizara ya elimu inatkiwa ibinafisishwe!.
Ninatamani sana kikwete aongee naye juu ya kubinafsisha jeshi la polisi na wizara ya elimu ili wajerumani wazichukue.
Kama JK amesema hivyo basi mwacheni Mugabe aitwe Mugabe. Hiyo ni aibu kwetu sote na ndo maana tunahitaji Raisi mwenye macho ya tofauti kuwafundisha watanzania kuwa wanaweza na wajiamini waondokane na mtazamo wa kutembeza bakuli dunia nzima
Wakati fulani tuseme na ukweli, wajerumani walitukuta hatuna hata nguo, tunauzwa sokoni kama mbuzi, je hilo jengo la ikulu kajenga nani kama sio wajerumani, reli ya kati kajenga nani kama sio wajerumani.ukweli mazuri ya wajerumani kwa miaka 35 waliyokaa hayawezi kulinganishwa na ya kwetu.