First thing first. Mimi siyo mmoja wa wale Watanzania wanaomwabudu Nyerere kama Mungu au kila kitu asemacho ndio cha kweli. Alituongoza kibabe (bila demokrasia) na kuiacha nchi hoi bin taaban baada za zaidi ya miaka 20. Nadhani utakumbuka chakula cha ration. Mimi siwezi kutafuna maneno, Ujamaa kwa maneno ni mzuri sana lakini kwa vitendo uliua nchi.
Hajataka kugusa madini kwa sababu ni kinyume cha siasa yake na serikali Yake haikuwa na uwezo wa kifedha kwa kuwa Ujamaa uliuteketeza uzalishaji. Mfano mdogo ni ule wa ration ya chakula. Hata sabuni Nyerere alipewa MSAADA na Urusi. Najua kwa kuwa nilipewa kuuza na Ugawaji. Nani zaidi ya bepari anaweza kufanya biashara ya uchimbaji wa madini? Gharama zake na elimu yake ilikuwa kubwa wakati huo na ni kubwa wakati huu kuliko uwezo wa Watanzania na Serikali. Kaa na kujua uzalishaji WOTE wa nchi ni dola bilioni 40 tu mpaka sasa, sawasawa na uzalishaji wa mwaka jana wa Kampuni ya Huawei ya China. Na Tanzania ya Kikwete pamoja na wizi, ni Tajiri kuliko Tanzania ya Nyerere alipomkabidhi Mwinyi. Huu ndio ukweli kiuchumi. Tuweke hisia mbali na hali ya kiukweli ya nchi mbali.
Kuhusu Zimbabwe, Mugabe alitaka cookie points za kisiasa. Wakulima karibuni wote wa Kizungu wamepewa ardhi kubwa nchi jirani kwa kuwa viongozi wanaoona mbele wanajua kuwa hawa wazungu wana ujuzi wa Miaka mingi ya kilimo cha Kisasa na wana uwezo wa kifedha. Zimbabwe karudisha ardhi kwa mzawa na kushusha uchumi wake huku Waafrika wenzake Msumbiji, Zambia, na Afrika Kusini wamewakaribisha kulima kwao. Nani kapata faida hapo? Waafrika tukiacha siasa na porojo na kufikiri kielimu, tungefika mbali. Lakini wapi! Mugabe anapigiwa makofi huku nchi yake inadidimia kiuchumi na yeye kuganda pale pale tangu 1980. Quite an example to leave behind for future leaders!!
Siamini hata chembe kuwa Ujamaa wa Nyerere ungeweza kuitajirisha Tanzania. Alichukua miaka zaidi ya 20 na kutuweka na njaa kali.
The leadership failed in both nations and we shouldn't sugarcoat it anymore. It's time to accept their failures and move forward. Your implementation failure as the reason behind Ujamaa downfall is past expiry date, it doesn't hold water. Any reasonable person will admit that we are much better off economically now than in 1980 unless they are die-hard Nyerere apologists who will always find a way to praise his dictatorial leadership.