Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,395
- 13,266
Sasa alisemaje? Kukanusha bila kutueleza alichokisema unatuacha gizanihuu ni upotoshaji mkubwa,,,,,,,,wengi tulisikiliza hotuba ya rais hakuyasema haya
Sasa alisemaje? Kukanusha bila kutueleza alichokisema unatuacha gizanihuu ni upotoshaji mkubwa,,,,,,,,wengi tulisikiliza hotuba ya rais hakuyasema haya
Wakati fulani tuseme na ukweli, wajerumani walitukuta hatuna hata nguo, tunauzwa sokoni kama mbuzi, je hilo jengo la ikulu kajenga nani kama sio wajerumani, reli ya kati kajenga nani kama sio wajerumani.ukweli mazuri ya wajerumani kwa miaka 35 waliyokaa hayawezi kulinganishwa na ya kwetu.
Mkuu waafrika tulikuwa na mila na Tamaduni zetu na kama sio wakoloni kututawala tusingelirudi nyuma kama tulivyo hivi sasa..
Kutawaliwa,kufanya watumwa imeirudisha sana Afrika chini ya jangwa la sahara...Kujengewa ikulu...kwani hiyo ikulu waliwajengea waafrika au walijijengea wenyewe kwa kuwatumia wafrika kama wafanyakazi
Kimawazo,kifikra tumerudi sana ,mawazo na fikra zetu bado tunafikiria kuwa watu weupe(wazungu) wako bora kuliko waafrika adhma hiyo imetengenezwa makusudi ili tuzidi kutawaliwa...na ndio maana raisi wetu na mtu kama wewe bado mna mawazo kama hayo "Slavery mentality" bado mnafikira "slave masters" bila wao tusingelifika Popote
Shikamoo! Unatumia kinywaji gani?
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Profesa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa kututawala na kutuletea maendeleo wakati wa ukoloni.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ikulu jana, Rais Kikwete alimuambia Rais wa Ujerumani kwamba wakati wanatutawala walitufanyia mambo mengi sana mazuri ikiwemo kutujengea jengo la ikulu ambalo tunalitumia hadi sasa.
Rais ameniumbua. Sijui nitaficha wapi uso wangu.
Tangu mwaka 2008 nimekuwa nikiwafundisha wanafunzi wangu Historia nikiwaaminisha kwamba wakoloni hawakuwa na nia njema. Nimekua nikiwaambia wanafunzi wangu kuwa wakoloni walikuwa wakitunyonya, kutukandamiza na kutudhalilisha sana.
Niliwaambia hata elimu waliyoitoa na miundombinu waliyojenga ilikuwa ya kuendeleza unyonyaji.
Niliwaambia wanafunzi wangu kuwa watu waliowapinga ukoloni na kuwapiga vita kama kina Mkwawa, Mangi Meli, Mtemi Isike na Chifu Kimweri ndio mashujaa wetu. Niliwasema vibaya sana wakoloni huku nikitumia vitabu vya kina Walter Rodney kama HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA katika kujenga hoja. Pia nilitumia sehemu ya nukuu za The Dar es salaam School of thought kuaminisha wanafunzi wangu kwamba wakoloni walikuwa watu makatili na wasiotufaa.
Leo rais kaniumbua. Kawaambia Watanzania kuwa Wakoloni walikuwa watu wema sana na waliotuletea maendeleo. Rais akafika mbali zaidi na kukiri bila Ujerumani kututawala tusingekuwa na Ikulu ya Dar es Salaam.
Sasa najiuliza kama wanafunzi wangu wamemsikiliza Rais Kikwete nitakoma maana nitaumbuka. Na kama wamemsikiliza Lazima watamuamini kwa sababu Rais wetu ni Profesa.!!
Kwa heshima ya Malisa Godlisten naomba kushirikisha hii simanzi!
Wakati fulani tuseme na ukweli, wajerumani walitukuta hatuna hata nguo, tunauzwa sokoni kama mbuzi, je hilo jengo la ikulu kajenga nani kama sio wajerumani, reli ya kati kajenga nani kama sio wajerumani.ukweli mazuri ya wajerumani kwa miaka 35 waliyokaa hayawezi kulinganishwa na ya kwetu.
nani kakudanganya? western media propaganda? nyerere na mandela walikuwa na wapinzani pia.
nani kakudanganya? western media propaganda? nyerere na mandela walikuwa na wapinzani pia.
Wewe mwenye akili tele lete kithibitisho kuwa wananchi wao wanaishi na raha na hawakimbii Afrika Kusini kwa dhiki na shida ya Maisha chini ya Mugabe.
Lete source yoyote kuonyesha mimi nimedanganya na nafuata western media sio ubongo wangu. sio unaleta maneno ya Kijiweni na viroba.
Pia, ulijuaje sijaishi Harare?
Mkuu nakupa dole gumba juu.Watu hawajielewi maana ya ukoloni eti!Gongo na msokoto mmoja wa bangi na hasusa embe kali 🙂
Mfano mmoja ambao wafrika chini ya jangwa la sahara tunashindwa hata kuendeleza hayo tulioachiwa na wakoloni,,sababu kubwa ya kushindwa kuvindeleza ni hatujiamini bado tuna mawazo kuwa bila ya "Master" mkoloni sisi wenyewe hatuwezi,mawazo kama hayo yametengenzwa na watawala hayakuja bure
Juzi juzi tu nimesikia mmoja wa mawaziri akisema kuwa Watanzania hawana uwezo wa kuwa na biashara ya kuwa na visima vya mafuta ambayo yamegunduliwa Tanzania,,,bado tuna mawazo kuwa wazungu ni bora kuliko sisi wenyewe hatuwezi
Kama watanzania hawana uwezo huo wa kuwa na visima vya mafuta kwanini serikali haiwawezeshi,,,nitakupa mfano wa nchi kama Vietnam serikali imewawezesha raia wake wawe milionea ili rasilimali za nchi zidhibitiwe na raia wenyewe,warabu wamefanya ndio hivyo hivyo...Watu waliokuwa hawawezi Duniani ni Waafrika wanaoishi chini ya jangwa la sahara na ndio maana nchi zilizoko chini ya jangwa la sahara ni maskini duniani...
Dini,ukoloni,utumwa hivi vitu tuliletewa na wageni na vitu hivi vilikuwa na madhumuni ya kuturejesha nyuma....havikuwa na madhumuni nyengine..
"Emancipate yourself from slavery mentality non but yourself can free your mind":-Bob Marley,,,,, mvuta bangi maarafu duniani 🙂
kauli ya akili na raha imeibukia wapi tena? tanzania kuna raha? watanzania hawakimbilii nchi za watu kila siku?
Mugabe ni simba wa Afrika.
Hujajibu bado. Talk is cheap. Au hujui maana ya kithibitisho?
Tuonyeshe Mugabe kama "simba wa Afrika" kafanya nini kusaidia Maisha ya wananchi. Onyesha sifa aliyostahili kupewa kwa mifano sio maneno ya kijiweni.
Unahitaji uthibitisho gani zaidi ya ulio dhahiri mbele za macho yako? Unataka kusema haujuwi kabisa ni kwa nini Magharibi wanamchukia na wanapandikiza mbegu za chuki kwa kuubaka uchumi wa Zimbabwe? Mnamchukia mtu kwa kusimamia haki na kweli? Mnamchukia mtu kwa kurejesha raslimali waliyopokonya mabwana zenu?
Inapofikia Rais wa nchi anaramba miguu ya wajerumani kwa kuusifia ukoloni haishangazi kwa mwananchi kama wewe kuwatetea wezi, fikra zako zimetekwa na kufifishwa na wakoloni.
Emancipate yourselves from mental slavery; None but ourselves can free our minds.
-Robert Nesta
Sio kila uongozi mbovu Afrika unalaumu nchi magharibi.
Na hiyo ardhi nyingi amewapa ndugu na rafiki zake. Soma juu jinsi uchumi ulivyoshuka. Kama angewapa wakulima wazawa wa kawaida ningemwelewa. Itakuwaje umsifie Dikteta aliyoifanya nchi Yake kutoka nchi tajiri inayojilisha na kusafirisha mazao ya kila aina mpaka kuwa masikini na kuomba msaada wa vyakula ? Kama unabisha, huu sio ukweli, basi thibitisha. Usilete hadithi za vijiweni. Sio kila tatizo ni kwa sababu ya nchi za magharibi. Kubali kuwa viongozi wa Kiafrika kama Mugabe wanaong'ang'ania uongozi tangu 1980 ndio tatizo kubwa la Maendeleo ya Mwafrika. Zimbabwe ya leo ipo wapi na ya 1980 ulikuwa wapi? Wewe ndio kipofu!
Wewe unajiitia hujui uchumi. Unamkabidhi ardhi Yake Mwafrika ghafla bila kumpa elimu ya juu ya kilimo, vifaa wala elimu ya kuuza nje mazao. Halafu unalalamika nchi magharibi ndio sababu ya kushuka uchumi.
Mwisho Ardhi ipo chini za mzawa lakini nchi haiwezi kujilisha na Wananchi kuteseka na njaa. Huku unawabana wapinzani wako. Hii ndio sifa anayoistahili kupewa?
Hujajibu swali. "Simba Wa Afrika" ameleta maendeleo gani Zimbabwe tangu aichukue 1980? Na kama imeendelea chini ya uongozi wake, tuletee ushahidi sio maneno ya vijiweni. Hapa sio kijiweni. Ni rahisi sana kusema kuliko kutenda.
Unajifanya haujuwi njaa ya Zimbabwe imeletwa na nani? Haujawahi kujiuliza kwa nini wakulima wa Ruvuma na Rukwa tu wanaotumia jembe la mkono wanazalisha mahindi ya kulisha nchi tatu na kusaza? Mugabe ameanza lini kung'ang'ania madaraka, miaka ya 2000? Haujiulizi ni kwa nini kuwa madarakani kwa muda mrefu Mugabe hakukuwa issue, hakukuwa kung'ang'ania madaraka mpaka alipoanza timuatimua kwa wavamizi mwaka 2002? Inamaana kabla ya hapo alikuwa shujaa, katimua wavamizi tu aondoke madarakani...loh! Wewe una hasira na Mugabe juu ya udikteta? Magharibi haina hasira juu ya Mugabe kwa sababu ya udikteta ndugu yangu rejea nyuma mzizi wa fitna ulikoanzia.
Unajitia haufaham weupe walipataje ardhi Zimbabwe? Sitaki kuamini kuwa hauijui Land Apportionment Act ya 1930. Hebu vuta picha leo hii hapa Tanzania waje Wakoloni watunyang'anye ardhi, yaani wavamizi ambao ni asilimia moja tu ya population wamiliki asilimia SABINI ya ardhi, halafu wenye nchi wahamishiwe shinyanga, singida, na dodoma kwenye ardhi isiyo rutuba na ukame!! Watu hawa walivumilia hayo, walivumilia mifugo yao kuibwa na kuuwawa. Lakini kumbuka uvumilivu una mwisho wake. Kumbuka Mugabe alikubali masharti ya uhuru, kununua ardhi kutoka kwa setlers ambao wataona kichefuchefu kuendelea kukaa Zimbabwe chini ya utawala mweusi (nikunyang'anye kitu kisha nikuuzie, geez!). Hauwezi kujua kilichotokea kwa sababu habari zako zote unaskiza BBC, lakini wacha nikwambie; London haikuishi ahadi yake ya kutoa "ruzuku" kwa serikali ya Zimbabwe, hivyo haikuwa na pesa za kutosha kununua ardhi kutoka kwa wezi wale na kuirejesha kwa wenye nayo, na pia wezi wale hawakuwa na nia ya kuuza kwa sababu walishahakikishiwa "ulinzi" kutoka London! Hivyo wenye ardhi yao walibaki kupiga miayo na kuwa vibaraka wa wakulima wavamizi.
Ilikuwaje mpaka hawa kondoo wa kiafrika wakageuka kuwa chui? Rejea ukame uliokumba Zimbabwe 1990-93, mjusi akawa amebanwa kwenye kona hana pa kutokea, wenye nchi wakamwambia Mugabe wanataka ardhi yao, ardhi halali ya babu zao, ardhi yenye rutba iliyotwaliwa na Mabeberu, wanaitaka mara moja bila masharti yoyote kwa sababu ni yao. Kuanzia hapo nadhani unaelewa kilichoendelea, kilichomgombanisha Mugabe na rafiki zake wakubwa wa London ni MAAMUZI MAGUMU, hizo unazobania pua wewe ni matokeo ya propaganda za Magharibi kwenye vijiwe vyao vya kahawa maarufu kwa vifupisho kama BBC, CNN nk.
Emancipate yourselves from mental slavery; None but ourselves can free our minds.
-Robert Nesta
You are thinking like our dear president and you are both very wrong. You just start to appreciate people who had used you and robed your humanity for token given. Utaanza kusifia waarabu kwa kuwapa watumwa walio wateka kwa kuwapa pilau na kuwavisha kanzu. It is absurd to say but the least.Wakati fulani tuseme na ukweli, wajerumani walitukuta hatuna hata nguo, tunauzwa sokoni kama mbuzi, je hilo jengo la ikulu kajenga nani kama sio wajerumani, reli ya kati kajenga nani kama sio wajerumani.ukweli mazuri ya wajerumani kwa miaka 35 waliyokaa hayawezi kulinganishwa na ya kwetu.
abeeeh.