gsu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2014
- 3,461
- 712
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Profesa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa kututawala na kutuletea maendeleo wakati wa ukoloni.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ikulu jana, Rais Kikwete alimuambia Rais wa Ujerumani kwamba wakati wanatutawala walitufanyia mambo mengi sana mazuri ikiwemo kutujengea jengo la ikulu ambalo tunalitumia hadi sasa.
Rais ameniumbua. Sijui nitaficha wapi uso wangu.
Tangu mwaka 2008 nimekuwa nikiwafundisha wanafunzi wangu Historia nikiwaaminisha kwamba wakoloni hawakuwa na nia njema. Nimekua nikiwaambia wanafunzi wangu kuwa wakoloni walikuwa wakitunyonya, kutukandamiza na kutudhalilisha sana.
Niliwaambia hata elimu waliyoitoa na miundombinu waliyojenga ilikuwa ya kuendeleza unyonyaji.
Niliwaambia wanafunzi wangu kuwa watu waliowapinga ukoloni na kuwapiga vita kama kina Mkwawa, Mangi Meli, Mtemi Isike na Chifu Kimweri ndio mashujaa wetu. Niliwasema vibaya sana wakoloni huku nikitumia vitabu vya kina Walter Rodney kama "HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA" katika kujenga hoja. Pia nilitumia sehemu ya nukuu za "The Dar es salaam School of thought" kuaminisha wanafunzi wangu kwamba wakoloni walikuwa watu makatili na wasiotufaa.
Leo rais kaniumbua. Kawaambia Watanzania kuwa Wakoloni walikuwa watu wema sana na waliotuletea maendeleo. Rais akafika mbali zaidi na kukiri bila Ujerumani kututawala tusingekuwa na Ikulu ya Dar es Salaam.
Sasa najiuliza kama wanafunzi wangu wamemsikiliza Rais Kikwete nitakoma maana nitaumbuka. Na kama wamemsikiliza Lazima watamuamini kwa sababu Rais wetu ni Profesa.!!
Kwa heshima ya Malisa Godlisten naomba kushirikisha hii simanzi!
Huyu ndiye kikwete ninayemjua.
[h=2]MAZURI ya Kikwete ambayo hayajawahi kufanywa na marais waliomtangulia HAYA HAPA[/h]
Katika kipindi cha Kikwete masuala yafuatayo lazima tumpe Credit kwani baadhi yamefanywa na JK wa mwanzo tu na hayakufanywa na Mwinyi wala Mkapa.
1. Ujenzi wa Sekondari za Kata ni maamuzi sahihi ingawa yana changamoto zake zinazoweza kutatuliwa na watakaomfuatia, lakini hapa JK ametumia madaraka yake vizuri
2. Ameendelea na uendelezaji wa Miradi ya Barabara, suala lililoanza kujitokea wakati wa awamu ya 3, JK ameendelea nalo suala hilo kwa kasi kubwa na kwa kipindi chote
3. Daraja Kigamboni, Malagarasi na Kilombero ni miongoni mwa mambo yatakayokumbukwa forever
4. Ongezeko la Taasisi za Elimu ya Juu limefanyika vizuri sana katika awamu ya Kikwete, mbali na UDOM lakini taasisi na vyuo vingi vimeimarishwa, kupandishwa hadhi na vyuo vingi binafsi vimeanziswa. Kwa sasa Taifa haliko tena na dhana ya UDII, Mzumbe na SUA. Aidha ari na moyo wa watanzania kulipia huduma za elimu umeongezeka.
5. Kumekuwa na ongezeko kubwa la ajira ukilinganisha na awamu mbili zilizomtangulia. Mkapa aliendesha Serikali nyembamba, suala ambalo ni zuri lakini lina changamoto zake kwa wale waliokuwepo wameliona hata akapewa sifa ya mzee wa "ukapa"
6. Mradi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara kwa lengo la kutatua kero ya Umeme ni hatua nzuri ambayo haijawahi kufanywa katika awamu ya 2 na ya Tatu (Vyanzo vya Nishati)
7. Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Chuma (Kule Liganga?) ambao maandalizi ya ujenzi wake yamekamilika ni hatua nzuri ili kuvutia au kuanzisha uwekezaji wa zana za Chuma pamoja na Viwanda vikubwa.
8. Hatua ya Kujenga Bandari mpya eneo la Bagamoyo yenye hadhi ya 4th Generation ni tukio litakalokumbukwa na vizazi Dahri vijavyo.
9. Hatua ya Utekelezaji wa mradi wa DRT ambao ulikuwepo miaka mingi pia ni miongoni mwa mazuri yaliyotendeka katika awamu ya JK
10. Zoezi la kutambua na kuwarudisha kwao wahamiaji haramu pia ni zoezi zuri ambalo bila shaka halijawahi kufanywa katika uongozi wa awamu nyinginezo kwa kiwango na utashi wa namna hiyo
11. Kitendo cha utekelezaji wa mradi wa vitambulisho vya Taifa ni credit kubwa kwa JK ambao hakuna sababu za wazi kwanini nchi imekaa miaka 50 pasipo na vitambulisho vya uraia kwa wakazi wake na raia wake
12. Ameendelea kuiweka Tanzania kwenye mahusiano mazuri kimataifa hususan SADC, UN na nyanja nyingine za Kitaifa. Ukiacha EAC ambayo sababu za kuzorota kwake ziko wazi, lakini maeneo mengine ame-play well.
picha; maendeleo ya ujenzi wa daraja la kigamboni eneo la kurasini jijini dsm. ujenzi ulikuwa asilimia 47 mwezi july