SoC01 Nitafanya nini sasa na wakati sina mtaji? Sijui nianzie wapi, wala sijui pia nikakope kwa nani?...

Stories of Change - 2021 Competition

Ornate

Member
Jul 13, 2021
26
33
Haya ndiyo mengi yanayotawala katika vichwa vya watu wengi, kutokana na kila mtu anawaza kwa namna yake.

Tatizo la ajira limeifanya jamii itafute njia thabiti itakayoweza kuwakomboa watu katika janga hili la ukosefu wa ajira. Lakini swali la kujiuliza vipi litamalizika tatizo hili katika bara la Afrika hasa katika nchi yetu ya Tanzania?

Katika makala hii nitakufahamisha kwa undani namna ya kuweza kukuza mtaji ulionao ili kuweza kujiajiri na kuendeleza Yale uliyotamani kuyafanya kupitia nguvu ya mtaji wako.

Kwa ufasaha wake neno Mtaji ni utajiri au kiasi katika mfumo wa pesa au Mali nyingine inayomulikiwa na mtu au shirika na inapatikana kwa kusudi Fulani kama vile kuwekeza katika biashara au kuanzisha kampuni.

Katika taifa lolote ambalo huhitaji maendeleo, mtaji ni jambo la kwanza kulitazama ili kuweza kufikia Yale ambayo taifa limelenga kuyafikia, ikiwemo ujenzi wa Barabara, reli, vituo vya afya na maendeleo katika nyanja zote za maisha.

Taifa lolote huendelea kutokana na ulipaji wa kodi pia kwa wananchi, ambapo wananchi hao hao neno mtaji limekuwa ni kilio kwa wengi Aidha kwa wale walio katika ujasiriamali na hata kwa wale wenye ndoto za kuwa wajasiriamali. Kwa uchache zifuatazo ni njia madhubuti ambazo zinaweza zikaleta usanifu mkubwa wa kuongeza na kukuza mtaji kwa jamii na nchi kwa ujumla wake.

Thamini kile ulichonacho; Kama ambavyo mwandishi Enock Mareges " Kitu kikishindija a katika maisha yako kamwe usikate tamaa kwa sababu kushindwa ni mama wa mafanikio na kukata tamaa ni mama wa kushindwa" Ni ukweli ulio dhahiri wengi hudhani mtaji mdogo hauwezi kukufikisha popote, hii ni dhana na uongo tena isiyo na mashiko kwani mtaji mdogo ndio unaweza ukakufikisha mbali kwa namba ya juhudi na jitihada zako katika biashara yako.

Mwanaharakati wa bara la Afrika Nelson Mandela aliwahi kusema “Mara zote huwa hakionekani, lakini pale utakapofanya ndipo huonekana” .

Usemi huu unaonesha namna ambavyo Mtu akithamini kile kidogo chake alichonacho na akakifanyia kazi ndipo huja kuleta matokeo makubwa na faida kubwa na hatimaye mtaji wake kuongezeka.

Ukiangalia mfano huu unaweza ukaufananisha na namna ambavyo aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli aliyeweza kuthamini kile kidogo ambacho Tanzania tunacho kutokana na kodi za wa Tanzania na hatimaye kufanya mambo makubwa katika taifa letu la Tanzania.

Weka biashara kwa ushirikiano (ubia); Namna nyingine ya kuweza kukuza mtaji ni kujikita katika biashara za kushirikiana au Ubia kwa jina lingine. Hii unaweza ikaleta matokeo chanya kutokana na makubaliano ambayo mtajiwekea na hatimaye kila mmoja akaongeza mtaji wake.

Tatizo la watu wengi ambao hujikita katika biashara za namna hii huishia katika ugomvi,chuki na hata kujenga uhasama usio na msingi na hatimaye kupelekea kushindwa kuyafikia malengo husika.

Kama tukijenga ushirikiano mkubwa na nchi za kimataifa yaweza ikawa ni tija katika taifa letu kwanza kuongeza mtaji tulionao lakini pia maendeleo lukuki hasa katika sekta ya biashara ambayo itapelekea maendeleo ya viwanda katika nchi yetu.

Akiba;
Wengi Kwa kupitia azimio la Tabora lililosisitiza juu ya uwekaji wa akiba na ukuaji wa uchumi mwaka 2015 , ripoti yao ilieleza kuwa kwa miaka takribani kumi na tano toka mwaka 2000 hadi 2015 nchi ya Tanzania imekuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi ya wastani wa 7%kwa mwaka.

Hata hivyo kubainisha kuwa nchi zenye malengo ya kukua kwa asimia Saba kwa mwaka inabidi ziwe na uwekaji wa akiba wa 35% ya pato la taifa. (Pinto, 2014). Wengi hufeli katika kipengele hiki kwani wengi wao hudhani kuwa unapopata ni fursa ya kutumia vibaya kumbe kuweka Akiba ndio kianzio cha baadae.

Hata katika taifa tunapokuwa hatuna kiasi cha fedha katika hazina ya serikali na mapato yakiwa yamepungua inakuwa ni vigumu kwa nchi kuendelea kwa namna yoyote ile. Na ndio sababu Akiba ikawa ni njia pekee ya kukuza mtaji.

Kwa mfano mfanya biashara aliyeanza na biashara yake na mtaji wa shilingi laki tano , akafanya kazi kwa miezi mitatu akazalisha faida zaidi ya shilingi milioni tatu kisha akaamua kuweka Akiba benk shilingi milioni mbili.. Hapo atakuwa tayari ameshakuza mtaji wake na amejiwekea Akiba ingine endapo atahitaji kufanya kitu kingine.

Omba mkopo; wakati mwingine ukikwama kabisa kuonba mkopo ni sababu ya kukuza mtaji wako ijapokuwa suala la mkopo limegubikwa na changamoto kubwa ya riba kubwa na hatimaye wengi kuangukia kuwa masikini kushindwa kurejesha mikopo na Mali zao kutaifishwa.

Hapa umakini unahitajika sana kwa muombaji hasa kwa kuzingatia ni kiasi gani unachohitaji kukopa na kwa lengo la kufanyia biashara gani ambayo itakuingizia faida ili uweze kurejesha mkopo. Wengi hufeli kwani hukopa pesa nyingi na huanzisha biashara ambazo hazina faida na mwishowe hushindwa kurejesha fedha za mkopo na kupelekea kukosa mtaji kabisa.

Miongoni mwa mashirika yanayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali ni SACCOS na hata benki, lakini pia aliyekuwa Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Hayati John pombe Magufuli aliweza kutoa fedha za kitanzania shilingi milioni hamsini kwa kila kijiji ili kiwawezesha wajasiriamali wadogowadogo kupata mkopo bila riba,hii yote ilikuwa ni jitihada ya kukuza mtaji Tanzania

Uza vitu binafsi, angalia ni kitu gani cha thamani unachomiliki na kinaweza kikakupatia mtaji,watu wengi wanamiliki simu zijulikanazo kama smartphones ambazo bei yake si chini ya shilingi laki moja, uza na upate mtaji kwani biashara ikikua utanunua nyingine yeny thamani zaidi ya uliyokuwa nayo. Wakati mwingine lazima tutoe tulivyonavyo ili tupate vikubwa zaidi.

Tafuta ndugu na marafiki, washirikishe ndugu na marafiki wa kweli kuhusu unachotaka kufanya waombe wakisaidie kujazia kidogo ulichonacho na ukitumie kwa kukithamini na kukilinda ili kiendelee kukupa faida mbeleni hapo utaweza kukuza mtaji wako ulionao na kuufanya uwe mkubwa zaidi.

Waswahili huwa na msemo wao wa kusema mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio haambiwi sikio. Njia hizi zikitumiwa kiufasaha tatizo la mtaji kuwa mdogo litaepukika na matokeo yake tutakuza mtaji kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na hata kwa taifa letu kwa ujumla.

Alisikika aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli kuwa Tanzania ni nchi tajiri iliyobarikiwa maliasili nyingi na za kutosha ikiwemo madini. Hivyo kama zitatumika vizuri na kwa mpangilio mzuri tutaweza kuleta maendeleo makubwa wenyewe. Usikate tamaa kwa kidogo ulicho nacho sema siwezi kushindwa kila wakati unapohisi unashindwa.

Mbali na hayo wanachuo wengi baada ya kumaliza masomo yao wamekuwa wakijiuliza sana ni kwa namna gani wanaweza kujikwamua kiuchumi hali ya kuwa hawana pesa, so kweli,mtaji huo huo hata kama mdogo, ndio,unatosha kabisaaa.

Kuna biashara nyingi sana zinazoweza zikawa na mtaji mdogo lakini ukapata faida fanya hivi uza makava ya simu, haya yanaitaji mtaji mdogo sana lakini watu wengi huvutiwa nayo na kununua, haitoshi bado zipo tangaza biashara zako mtandaoni, unaweza kufungua akaunti Instagram ukaikuza na kutanganza biashara yako ndogo hii pia itasaidia kupunguza gharama kubwa ya kutangaza kweny vyombo vya habari, lakini pia,uza vitafunwa na oka keki, watanzania wengi huamka asubuhi sana kuelekea makazini hivyo watanunua tu!

Ebu fungua mgahawa, uza vyakula kwa usafi na weledi watu watapenda watakula tu, usijali kama haitoshi ebu fundisha mtandaoni kwenye mfano unaweza tumia amazoni kufundishia utapata ela. Wapo Vijana wengi Tanzania walioamua kujikita katika kuuza CDs na kuingiza nyimbo, ndio inalipa ina faida unaweza ukaweka faida yako na kukuza biashara pia, anzisha blogu pia kwa kuanzisha blogu mtandaoni utaweza kufika mbali watu wengi sasa hivi sana sana wasomi wameweza kuanzisha blogu ambazo wanatoa taarifa mbalimbali na kuandika makala mbali mbali hivyo ni fursa kwao kwan wanaingiza pesa sana, mfano mzuri Ni Millard Ayo ambaye kwa sasa amekuwa maarufu na amepata faida kubwa kupitia blogu zake hivyo usiwaze utapata wapi mtaji. Usihangaike tena kijana mtaji kidogo,akili nyingi, faida kubwa.

Watanzania wengi wamekuwa wakishindwa kuendeleza biashara kutokana na kukatika kwa mitaji, tafadhali epuka kuweka undugu kwenye biashara, hata kama ni ndugu mwache anununue ilhali tu ni biashara lakini pia uwe na muda wa kusimamia biashara zako mwenyewe kwani wakati mwingine tunaowaamini ndio wanaotuumiza hivyo pata muda wa kusimamia na kufuatilia biashara ulizonazo pia tumia faida kukuza mtaji mda mwingine punguza matumizi mabaya ya faida yako na uongezee kwenye mtaji wako. Pia usiharakie kupanua mtaji subiri biashara ichanganye na iwe ya faida nyingi hapo ndipo ukuze na utanue mtaji wako.

Wakina mama wengi pia wamekuwa wakishindwa kufanya biashara kisa hawana mtaji, hapana cheza michezo midogo midogo ya pesa na ujiingize kwenye vikundi mbalimbali vya akina Mama ikiwemo VICOBA pesa hiyo hiyo utakayoipata ndio itakuwa mtaji mkubwa wa biashara yako,usiogope kiutwa Mama ntilie au baba ntilie waswahili hunena mdogo mdogo ndio mwendo.
 
Back
Top Bottom