Je Una Mtaji Wewe?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,497
5,533
Habari za Wakati huu;
Mwaka 2014 Nilikuwa katika harakati za kutaka kuanzisha shule ya biashara(Business School).NIlilenga iwe shule ya Biashara ambayo inapokea mwanafunzi yeyote,kwa kozi yoyote na ambayo ingatumia mfumo wa kujifunza ambo unazingatia zaidi matakwa na malengo ya mwanafunzi badala ya Kuwa na Mwongozo maalum.Ili kujiunga na shule hii Mwanafunzi alipaswa kufahamu hasa anataka kufanya nini na maisha yake na wataalamu wetu wa uandaaji wa Mitaala na Mafunzo wangemuundia kozi yake maalum kwa kuzingatia kozi na mafunzo ambayo tayari tunayo na kisha kwa yale ambayo hayapo tungeyatengeneza upya.

Binafsi niliamini kabisa kwamba hili ni wazo la kimapinduzi kulingana na uelewa wangu.SO nilianza kulifanyia kazi.Kwanza nilitembelea Taasisi zinazohusika na utoaji wa elimu ikiwmo ale UDBS na vyuo kama CBE na IFM.Nikazungumza na wanafunzi na baadhi ya wakufunzi ili kuona kama wazo langu linaweza kuwa validated.Kote huko Wazo langu walilipokea swala hilo Vizuri na Waliniacha na Swali Moja tu "JE UNA MTAJI WEWE?"
Nilitembelea pia mamlaka za usimamizi wa elimu kama Wizara ya ELimu,TCU,NACTE,VETA na hata baadhi ya Maofisa ELimu na wadau wengine kama NGOs na CSOs na kujadiliana nao kuhusu Jambo hili ili pia kupata validation yao.Huko nao walipokea wazo vizuri ili hawakuacha kuniuliza swali lile lile la "JE UNA MTAJI WEWE'
Katika kupekuwa zaidi nilitembelea taasisi za fedha na kujadiliana nao kuhusu uwezekano wa wao kuwekeza fedha katika Mradi huu hasa ujenzi wa miundo mbinu na nilifika hadi baadhi ya mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na wadau wengine wa biashara na elimu kama vile vyama vya wafanyabiashara na kodte huko wazo lilipokelewa vyema ila hawakucha kuniuliza "JE UNAO MTAJI WEWE"
Kama wewe umewahi kuwaza kuanzisha biashara au katika hatua za mwanzo za biashara umewahi kuuliza au kujiuliza iwapo "UNAO MTAJI"

Hili swali ni swali ambalo kwa nje linaonekana swali la kawaida sana ila ni moja katika ya maswali ambayo yanaua sana Mawazo mazuri na ni swali ambalo hupaswi kumuuliza mtu mwenye wazo wala hupaswi kujiuliza wewe mwenyewe kwa sababu ni aina ya swali ambalo linaua kabisa hamasa na msukumo wa ndani wa mtu ambaye anaweza kufanikiwa.

Ni zaidi ya miaka kumi sasa tangu nifanye jitihada za kutaka kutekeleza wazo hili ila kwa sababu bado najiuliza swali hili bado sijaanza utekelezaji wa wazo hili.Ninapoandika andiko hili natambua kabisa Kinachoua hamu ya kufanya hili jambo ni kwa sababu ya kujiuliza JE UNA MTAJI au kuulizwa na kila MTU ambaye nimejadiliana naye JE UNA MTAJI?Tena wengi wanaouliza swali hili huwa hawajua hata financial details za project na wala hawajui project inahitaji kiasi gani lakini watauliza tu ili waweza kuua wazo lako.Utajiuliza tu ili upate sababu ya kutokuchukua hatua.Ni kidonge cha SUMU ambacho kinalenga kuua mawazo mengi ya biashara.

Nimeleta Mjadala huu hapa ili hapo ulipo utafakari ni mara ngapi umeacha kufanya jambo zuri la biashara kwa sabbu ya kuulizwa swali hilo au kujiuliza wewe mwenyewe swali hilo?

Unaweza usiamni lakini kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita tangu niwe na wazo hilo,Nimefanikiwa sio zaidi ya mara moja kuwa na mtaji wa kuanza kutekeleza wazo hilo lakini sikutekeleza wala sikuliwaza.Naamni kabisa kwamba Kama shida kweli ilikuwa mtaji basi tayari tungekuwa business school kama nilivyoiota.

Je Wewe UNAO MTAJI?Je una wazo la Biashara ambalo umeacha kulitekeleza kwa sababu ya kujiuliza iwapo UNAO MTAJI?Je umeacha kufanya project yako kubwa baada ya kuulizwa JE UNAO mtaji.Kama jibu ni ndio basi hauko PEKEE wapo wengine sana.

Tufanyeje?Kwa leo tujadili JUU ya kauli hii na namna ambavyo iliathiri wazo lako.Jitahidi uweke wazo lako ambalo ulitamani kulifanya liwe biashara ila ukaliacha baada ya kuulizwa au kujiuliza iwapo uano mtaji Baada ya Kuliweka huenda wadau humu wakaliona na mkaungana na kupeana mtonyo ili kukata hii kasumba ya kuacha kufanya mambo makubwa kwa kusema au kuwaza au kuuliza JE UNAO MTAJI?

PS.Iwa po ungependa kujadili zaidi kuhusu mada hii na kuendelea kujifunza moja kwa moja tafadha tuwasiliane kwa email:masokotz@yahoo.com

Ninawatakieni SIKU NJEMA YENYE BARAKA
 
Sawa umeongea vizuri na umetia moyo vijana ila turudi pale pale hiyo shule ungeanzisha una mtaji? Au unasubiri umpe mtu wazo aweke hela zake siku akichukua useme kakuibia. Katika jambo la kujiuliza na lisikukatishe tamaa kwenye biashara ni mtaji yaani lazima uzingatie mtaji na ujue kwamba huo mtajinunaweza weka na ukaliwa na ukahitajika kutafta mtaji mwingine cha msingi ni kutokata tamaa uwezi sema mtu hajui gharama ya mradi alaf anauliza unamtaji ili ukate tamaa hio ni ngumu lazima ukimuambia mtu unaanzisha shule ya biashara atawaza kabla ya kiwa na wanafunzi lazima uajiri lazima uwe na majengo haya vyote hivyo ni mtaji unahitajika je unao?

Labda utoe somo la kitokata tamaa kama ww ulivyokata ila aliekuuliza unamtaji alikua na maana nzuri kwakua mpka leo miaka 9 imepita hujaweza kuanza ninkwasababu HUNA MTAJI. hayo mengine ni kujifariji
 
Sawa umeongea vizuri na umetia moyo vijana ila turudi pale pale hiyo shule ungeanzisha una mtaji? Au unasubiri umpe mtu wazo aweke hela zake siku akichukua useme kakuibia. Katika jambo la kujiuliza na lisikukatishe tamaa kwenye biashara ni mtaji yaani lazima uzingatie mtaji na ujue kwamba huo mtajinunaweza weka na ukaliwa na ukahitajika kutafta mtaji mwingine cha msingi ni kutokata tamaa uwezi sema mtu hajui gharama ya mradi alaf anauliza unamtaji ili ukate tamaa hio ni ngumu lazima ukimuambia mtu unaanzisha shule ya biashara atawaza kabla ya kiwa na wanafunzi lazima uajiri lazima uwe na majengo haya vyote hivyo ni mtaji unahitajika je unao?

Labda utoe somo la kitokata tamaa kama ww ulivyokata ila aliekuuliza unamtaji alikua na maana nzuri kwakua mpka leo miaka 9 imepita hujaweza kuanza ninkwasababu HUNA MTAJI. hayo mengine ni kujifariji
Mkuu,naelewa ni vigumu sana kuelewa ukali na nguvu ya hili swali katika kuua NDOTO na MAWAZO mazuri.Kwa kauli yako hapo umesema kabisa ,MTU anaweza kuweka PESA yake kwenye hio shule kisha BAADAYE ukaja ukasema kakuibia WAZO lako.So umeongeza DREAM killer nyingine ambayo nayo inafanya wale ambao wanayo mitaji wanapokutana na mawazo ya wasiokuwa na mitaji wanayapuuza.Kimsingi kujiuliza au kuuliza mtu "JE UNA MTAJI WEWE" ni kumnyeshwa SUMU ambayo inaweza kuua kabisa ndoto zake.So bado nasimamia Pale pale kwamba tuachane kabisa na hii kauli na aina hii ya maswali hasa kwa watua ambao wako na sound ideas na wanahitaji validation ya Ideas zao.TUSIWE CHANZA CHA WATU KUACHA KUFANYA JAMBO KWA SABABU YA MASWALI YA aina hii
 
Back
Top Bottom