Nitaendelea kutokuwa na dini

Nitaendelea kutokuwa na dini

Sina hata cha ku comment maana umeongea fact tupu. Unajua watu ambao wameingia katika dini wanakuwa blind folded hata ufanye nini hawawezi kuuona ukweli na hivyo ndivyo mafunzo ya dini nyingi yanavyowatengeneza ili wasije wakastuka. Yaani utakapojidai kutaka kujua undani tu unaambia unakufuru na ndo inakuwa full stop yako. Hahaha dini bwana!
 

kitendo cha kuamini uwepo wa MUNGU kinaonyesha wazi kwamba Kumbe nawewe dini unayo labda hujui maana ya neno dini.

sasa tuambie hiyo imani yako wewe imeletwa na watu gani?
 
Kwa upande wa quran tukufu haijawahi kupitwa na wakati wala haihitaji marekebisho ndugu yangu.imezungumzia past,present and future na sayansi ya dunia unayoiona leo hii yote ilizungumzwa ndani ya quran.
 
Habari wana jamvi.
1.Dini zimetoka wapi?
Dini kubwa zinazodominate Tanzanian zimeletwa na wageni. Islam imetoka Asia na Christianity imetoka Europe. Lakini unadhani kabla ya wazungu na waarabu kuja tulikua sisi waafrika hatuna imani?

Inakuwaje unaiamini gari iliyotengenezwa Ulaya au Asia na kisha kuletwa Tanzania, Lakini usiamini dini iliyoletwa na hao hao?

Shida sio dini imeletwa toka wapi, maana hata Ukristo haukuanza Ulaya. Ulisambazwa toka Israel na kanisa la kwanza.

Kila familia, ukoo, taifa zinatofautiana katika kumtafuta Mungu. Wale wanaopata Nuru mapema wanasambaza kwenye giza. Waafrika tulichelewa kupokea si dini tu, bali hata maendeleo ambayo teknolojia yote tunazotumia zimesambazwa na hao walioleta hizo dini.

2. Dini zote hazitaki kupokea mabadiliko

Vitabu vikubwa vya dini ni Qur'an na biblia. Lakini maandishi yaliyo kwenye vitabu hivi na matakatifu na hatuwezi kubadilisha kwa namna yoyote.
Kama vitabu hivi viliandika zaidi ya miaka 1000 iliyopita basi vilikuwa valid kwa watu wa kipindi hiko na si kwa kizazi hiki.

JUA lipo tangu kuumbwa kwa dunia, je limeisha makali yake? Ndivyo hata sheria, na mamlaka na nguvu za Mungu zilivyo, hazibadiriki. Yeye ni Yule, Jana, na hata Milele. Sisi ni binadamu, tunasimamiwa na mamlaka za kiumbaji; sisi ni binadamu, Mungu habadiriki kulingana na matakwa yetu.

3. Dini ni mifumo mikubwa inayowanyonya ndugu zangu masikini walioamini.
Kama umefanikiwa kwenda katika vijiji vya hapa Tanzanian basi endapo utaona jenho zuri lolote lilioezekwa kwa bati na kujenga kwa tofali na kupakwa rangi vizuri ilihali majengo yote maeneo hayo ni tope na nyasi basi dhahiri jengo hilo litakuwa kanisa ama msikiti.

Usizungumzie utoaji wakati hujaamini Mungu. Lakini imani zote za uungu zinaamini katika sadaka. Hadi shetani anataka sadaka. Ikiwa hutaki kutoa sadaka, basi hutopokelewa kote.

Ukitoa sadaka usirudi nyuma kuangalia mchungaji au sheikh kavaa nini au kala nini!!! Huo sio utoaji.

Lakini utoaji kwa Mungu wa kweli ni mgumu sana. Naam, mtu anaweza akafanya lolote gumu kufanikisha kafara za kishetani, kwa kutimiza masharti yote atakayopewa. Mfano kununua mbuzi mweupe asiye na doa n.k. Lakini ni ngumu sana kutoa kilicho bora kwa Mungu. Tunatoa vitu dhaifu kwa Mungu. Bahati nzuri, sadaka kwa Mungu ni laini.
 
Kuamini au kutoamini uwepo wa Mungu ni uamuzi wako binafsi.Pia kumbuka matokeo yake ni yako binafsi.Lakini hofu yangu inakuja kwamba wewe unaamini hakuna Mungu kutokana na uelewa wako wewe mwenyewe bila kupata taarifa sahihi kutoka vyanzo sahihi.Sasa wewe hujui na inatoa hitimisho hakuna Mungu kwa huko kutokujua kwako,huoni kwambo unakuwa mwongo?Suala sio kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu bali ni kukosa taarifa za kuhusu Mungu
Mungu yupo kwamba unamkubali au humkubali.Naomba nijibu tu nn chanzo cha ulimwengu na vilivyomo?Halafu kuanzia hapo utaanza kujiuliza maswali ambayo yatakufanya uyafute majibu ya maswali yako badala ya kujijibu kutokujua kwako.Swala la watu kujenga nyumba za ibada nzuri na kuwa na makazi duni hilo haliusiani na uwepo wa Mungu au kutokuwepo bali mahusiano ya watu na Mungu kwa hiyo halina mantiki kwa hali duni za watu.Kingine Mungu ni SUPREME BEING anajua yote kwa hiyo hayo mabadiliko unayoyaona ukiyachunguza wala hayana chochote cha kufanya maandiko matakatifu kwani vyote vitabadilika ila Mungu anabaki kuwa yule yule.
Mh! Sizani kama umesoma vizuri mada yangu.
 
Umesema utaendelea kutokuwa na dini..na hiyo ndio imani yako coz unaamini hakuna Mungu na huamin dini yyote..
Sasa je,lengo lako hasa kuleta hii mada ni nni?
Kwa nni usikae kimya na imani yako...
Au huna confidence na unachokiamini sasa unataka labda tu ku prove wrong?....
Amini unachokiamin na usisumbue wengine..
hujasoma vizuri, kaandika Mungu yupo but dini ndo aniziona zimezidisha machenga chenga.
 
Umesema utaendelea kutokuwa na dini..na hiyo ndio imani yako coz unaamini hakuna Mungu na huamin dini yyote..
Sasa je,lengo lako hasa kuleta hii mada ni nni?
Kwa nni usikae kimya na imani yako...
Au huna confidence na unachokiamini sasa unataka labda tu ku prove wrong?....
Amini unachokiamin na usisumbue wengine..
nadhani anahitaji kuona ni wangapi walio upande wake ili kusudi ajiamini zaidi.....
 
Kwani umeleta mada hii ili ijibiwe, upongezwe kwa kutokua muumini wa Kiisllam, au Kristo, ama kutafuta wafuasi, ama kutujuza tu ama nini hasa lengo lako. Nimekuuliza hivi kutokana ulivyomjibu mchangiaji hapo juu, amekuuliza kulikua na haja ya kuleta hapa jamvini, si ungekaa nalo tu. Wewe badala kumweleza dhumuni lako, unamwambia hajajibu hoja yako hata moja, Yeye amekubaliana na hoja zako ila anachotakujua ni kwanini utuambie sisi. Labda mimi nikuulize kulingana na moja sababu zako, hii kuwa ilileetwa na wageni. Je nguo unazotumia hazikutwa na wageni, Magari, TV, Ndege, barabara za lami niiiishie hapo kwanza.
kuongezea hapo;;;,,,,SI wazungu wala waarabu walioanzisha dini nao walizipokea TU.
 
Kabla sijafika mbali na wewe hebu soma hapa maana ya allah halafu tuanze kuelimishana na sio kukashifiana
God Allah - Does It Mean God?
Does it Mean God?

The word "Allah" is the perfect description of the "One God" of monotheism for Jews, Christians and Muslims!

Is "Allah" only for Islam and Muslims?
[No! It is for All Three Abrahamic Faiths.]

"Allah" is the same word used by Christian Arabs and Jewish Arabs in their Bible, centuries before Islam came.

On page one [1] of Genesis in the Old Testament, we find the word "Allah" seventeen [17] times.

Every hotel and motel has a Bible. Next time you see one look in the introduction, you will find samples of the different languages they have translated. For Arabic they have translated the verse in the New Testament in Arabic from the famous verse in the Gospel John 3:16 -

"For God so loved the world..."
- and the word the translators used in Arabic for "God" is the very same word used by Muslims around the planet, "Allah."
Where Does the word "Allah" Come From?

"Allah" comes from the Arabic word "elah"a god' or something worshiped. - (Arabic) means '

This word (elah) can be made plural (gods), as in "aleha" and it can be male or female just as the word in English can be "goddess."

"Allah" comes from "elaha" but it brings more clarification and understanding.

Allah = Has no gender (not male and not female)
"He" is used only out of respect and dignity - not for gender
Allah = Always singular - Never plural
"We" is used only as the "Royal WE" just as in English for royalty
Allah = Means "The Only One to be Worshipped"

Mkuu link uliyoiweka ime dfn hv
 
NB: Huwezi kusema moja kwa moja dini yako n ndo sahh kulko nyingne kama hujasoma ya mwenzako. Kama MTU unataka kuwa ktk imani iliyo sahh isome kwanza dini yako then soma na dini za wengine kisha acha ukweli ufanye kazi.

Nawasilisha
 
Habari wana jamvi.
Kwanza kabisa naomba niwiwe radhi kwa nitakachozungumza hapa kama nitawakwaza baadhi ya watu, ashankum si matusi.
Pili napenda niweke wazi kuwa ninaheshimu imani ya kila mtu na mimi natumaini kila mtu ataheshimu imani na msimamo wangu.

Ninapatwa wakati mgumu sana pale ninapotaka kuzungumza kuhusu dini na mungu kwani mambo haya yanatazamwa kwa mtazamo tofauti endapo mtu atathubutu kusema hakuna mungu ama hakuna dini.
Mimi naamini mungu yupo(kama sitapata shaka ya kutokuwepo)

Lakini ninaamini pasi na shaka kwamba ideology ya dini ni propaganda na si kitu sahihi kukifuata.
Labda niweke sababu chache ambazo zimenifanya nisiamini kwa dini yeyote (Islam and Christianity to bespecific)

1.Dini zimetoka wapi?
Dini kubwa zinazodominate Tanzanian zimeletwa na wageni. Islam imetoka Asia na Christianity imetoka Europe. Lakini unadhani kabla ya wazungu na waarabu kuja tulikua sisi waafrika hatuna imani? Je hizo imani zetu zimeenda wapi? Wazungu na waarabu walizipiga vita imani zetu na kuziita primitive na wao wakaleta imani zao na dini zao "civilization" Hivi unadhani kati ya imani tulizokua nazo sisi na hizo walizoleta waarabu na wazungu zipi ni "primitive"

Ninaamini kwamba dini zilikuja na wageni kwa mission zao (ukoloni na biashara) na baada ya mishen hizo kwisha wametuachia ujinga waafrika wa kukomaa na dini wakati wao wameshaacha huo upuuzi zamani. Tujaribu kuona misa za makanisa ya ulaya zinavyokosa waumini na tulinganishe mafuriko ya waumini wa makanisa na misikiti yetu afrika.

2. Dini zote hazitaki kupokea mabadiliko

Vitabu vikubwa vya dini ni Qur'an na biblia. Lakini maandishi yaliyo kwenye vitabu hivi na matakatifu na hatuwezi kubadilisha kwa namna yoyote.
Kama vitabu hivi viliandika zaidi ya miaka 1000 iliyopita basi vilikuwa valid kwa watu wa kipindi hiko na si kwa kizazi hiki ambacho kina mabadiliko makubwa katika kila nyanja ya maisha. Na sawa nabkutunza funguo yako ya gari la zamani na kulazimisha iendeshe kila gari jipya utakalonunua.

3. Dini ni mifumo mikubwa inayowanyonya ndugu zangu masikini walioamini.
Kama umefanikiwa kwenda katika vijiji vya hapa Tanzanian basi endapo utaona jenho zuri lolote lilioezekwa kwa bati na kujenga kwa tofali na kupakwa rangi vizuri ilihali majengo yote maeneo hayo ni tope na nyasi basi dhahiri jengo hilo litakuwa kanisa ama msikiti. Ni upuuzi kuona tuna makanisa manne na miskiti minane katika kijiji chetu ilihali hatuna hata zahanati. Pesa za ujenzi wa kanisa tulichanga lakni kanisa halina hata msaada mkubwa kilunganisha na dhahanati.
Sitaki kuzungumzia mashekh, maaskofu , mapadri na maimamu ambayo wanaishi maisha ya kitakatifu na anasa ilihali mimi muumini wananikwangua mpaka jasho langu la mwisho eti namtolea bwana.

Nina mengi ya kuzungumza na ninaahidi nitatoa sababu nyingine tele zinzofanya nisiwe na dini pundi nitakapopata wasaa.
Nawasilisha
Soma Dini yenyewe kabla ya kuandika mawazo yako. Kwa mfano Uislaam unakubali challenges but with fact. sasa maelezo yako hayana nukuu hata moja ! ....... hivyo ni mtu unae ropoka ropoka tu
 
Alichosema mleta mada ni ukweli mtupu usio na hata chembe ya kejeli ,kwani ni nani anabisha kuwa haya madini ndiyo yanaharibu dunia kwa sasa,vita zimesambaa kila mahali,kisa imani.Ni bora kuishi kama wachina ambao wengi wao dini yako ni wewe na nafsi yako.
Dini haiharibu dunia hata kidogo mkuu...dhamira mbaya ya mtu ndio inayomfanya yeye kutenda uovu..
Adolf Hitler alikuwa haamini katika dini yyte ile na alichonja na kuuwa watu wengi sana..
Benito Musolin pia alichinja wakatoliko kule italia kwa sabab yeye alikuwa haamin katima dini yyte..je hao nao waliongozwa na dini gani kuuwa watu wengi kiasi hicho?..
Embu tujarib kufikir kwa mtazamo mpana tusijibu vitu kwa kukariri bila kuangalia ukweli umesimama wapi
 
Dini haiharibu dunia hata kidogo mkuu...dhamira mbaya ya mtu ndio inayomfanya yeye kutenda uovu..
Adolf Hitler alikuwa haamini katika dini yyte ile na alichonja na kuuwa watu wengi sana..
Benito Musolin pia alichinja wakatoliko kule italia kwa sabab yeye alikuwa haamin katima dini yyte..je hao nao waliongozwa na dini gani kuuwa watu wengi kiasi hicho?..
Embu tujarib kufikir kwa mtazamo mpana tusijibu vitu kwa kukariri bila kuangalia ukweli umesimama wapi


Umeshajaribu kukaa chini na kulinganisha machafuko ya dunia hii yanayosababishwa na dini na sababu nyingine kwa kutumia uzani wa ubongo wako??.... Je, utabaini kuwa dini sio sababu ya machafuko mengi hapa dunian???..... .

Kubali au kataa dini ndio chanzo cha machafuko mengi hususan kwenye contemporaly issue za ulimwengu wa sasa... Mifano yako ya Benito Musolin na Hitler sio Halisi katika uzi huu..... By then kwenye reign za Benito na Hitler ugaid haukuwa umeshamiri sana zile zilikuwa vita au mauaji ya kimbali kams rwanda... Mauaji ya kuteketeza jamii ya watu fulan(genocide)... Ila hii haimaanishi kuwA dini sio chanzo cha uhasama hapa dunian???


Kaa chini ujiulize kwanin machafuko yanayohusisha dini yanatokea kwenye nchi masikin za afrca na asia.... Mbona watu hawauan kwa dini ulaya au america!!!!

Mungu hana dini..
 
@ozzanne issakiwisa.mbna unataka kutuaminishi vya ulaya yote bomba .na USHOGA je nao unataka tuukubali kwa mikono miwili kw kua umetokea dini zilipotokea!!!???
 
Imani yako imekuponya!, Imani ni kuwa na Hakika ya mambo yatarajiwayo.......Unachokiamini ndiyo imani yako hiyo. kama huna dini basi ndio hivyo hakuna kuchapwa fimbo wala nini. Wengine huokoka baada ya kukumbwa na shida mbalimbali mfululizo, hatuigi bali kwa kuamua wenyewe. Hoja yako namba 3 inasumbua waumini wengi nchini, nadhani ni tatizo sugu kwa makanisa mengi!. Kanisa kama linaanza watu wanabebeshwa misalaba ya misumali sana lakini kanisa linapokua kubwa, waanzilishi huwa wanatupwa kule labda kama wanajiweza kifedha wao binafsi. Otherwise Yesu atusaidie sisi tulio upande wake!!!!!
 
Matatizo yako soma Summa Theologica. Kwa sababu posting yako ni kama ukurasa unetolewa katika Summa Theologica. Mapadre wanajiuliza,sisi mapadre tunaposema Mungu yupo,tuna uhakika gani?
 
Back
Top Bottom