mkandumbwe
JF-Expert Member
- Aug 22, 2015
- 424
- 371
Habari wana jamvi.
Kwanza kabisa naomba niwiwe radhi kwa nitakachozungumza hapa kama nitawakwaza baadhi ya watu, ashankum si matusi.
Pili napenda niweke wazi kuwa ninaheshimu imani ya kila mtu na mimi natumaini kila mtu ataheshimu imani na msimamo wangu.
Ninapatwa wakati mgumu sana pale ninapotaka kuzungumza kuhusu dini na mungu kwani mambo haya yanatazamwa kwa mtazamo tofauti endapo mtu atathubutu kusema hakuna mungu ama hakuna dini.
Mimi naamini mungu yupo(kama sitapata shaka ya kutokuwepo)
Lakini ninaamini pasi na shaka kwamba ideology ya dini ni propaganda na si kitu sahihi kukifuata.
Labda niweke sababu chache ambazo zimenifanya nisiamini kwa dini yeyote (Islam and Christianity to bespecific)
1.Dini zimetoka wapi?
Dini kubwa zinazodominate Tanzanian zimeletwa na wageni. Islam imetoka Asia na Christianity imetoka Europe. Lakini unadhani kabla ya wazungu na waarabu kuja tulikua sisi waafrika hatuna imani? Je hizo imani zetu zimeenda wapi? Wazungu na waarabu walizipiga vita imani zetu na kuziita primitive na wao wakaleta imani zao na dini zao "civilization" Hivi unadhani kati ya imani tulizokua nazo sisi na hizo walizoleta waarabu na wazungu zipi ni "primitive"
Ninaamini kwamba dini zilikuja na wageni kwa mission zao (ukoloni na biashara) na baada ya mishen hizo kwisha wametuachia ujinga waafrika wa kukomaa na dini wakati wao wameshaacha huo upuuzi zamani. Tujaribu kuona misa za makanisa ya ulaya zinavyokosa waumini na tulinganishe mafuriko ya waumini wa makanisa na misikiti yetu afrika.
2. Dini zote hazitaki kupokea mabadiliko
Vitabu vikubwa vya dini ni Qur'an na biblia. Lakini maandishi yaliyo kwenye vitabu hivi na matakatifu na hatuwezi kubadilisha kwa namna yoyote.
Kama vitabu hivi viliandika zaidi ya miaka 1000 iliyopita basi vilikuwa valid kwa watu wa kipindi hiko na si kwa kizazi hiki ambacho kina mabadiliko makubwa katika kila nyanja ya maisha. Na sawa nabkutunza funguo yako ya gari la zamani na kulazimisha iendeshe kila gari jipya utakalonunua.
3. Dini ni mifumo mikubwa inayowanyonya ndugu zangu masikini walioamini.
Kama umefanikiwa kwenda katika vijiji vya hapa Tanzanian basi endapo utaona jenho zuri lolote lilioezekwa kwa bati na kujenga kwa tofali na kupakwa rangi vizuri ilihali majengo yote maeneo hayo ni tope na nyasi basi dhahiri jengo hilo litakuwa kanisa ama msikiti. Ni upuuzi kuona tuna makanisa manne na miskiti minane katika kijiji chetu ilihali hatuna hata zahanati. Pesa za ujenzi wa kanisa tulichanga lakni kanisa halina hata msaada mkubwa kilunganisha na dhahanati.
Sitaki kuzungumzia mashekh, maaskofu , mapadri na maimamu ambayo wanaishi maisha ya kitakatifu na anasa ilihali mimi muumini wananikwangua mpaka jasho langu la mwisho eti namtolea bwana.
Nina mengi ya kuzungumza na ninaahidi nitatoa sababu nyingine tele zinzofanya nisiwe na dini pundi nitakapopata wasaa.
Nawasilisha