Huyo aliyemfungia amwachie jamani
Hizi episode zinachinjwa na kuwa fupi, kama madamme mmoja tuliekuwa tukimuita madamme mchinjo kwenye wali maharage enzi hizo shulenSehemu ya 37.
Ndani ya mtandao huo wa Instagram katika kipindi asichokitarajia alikutana na mvulana aliyejulikana kwa jina la Fredick na kama utani alijikuta akianzisha urafiki na mwanaume huyo na baadae urafiki huo uliweza kuibua penzi kati yao.
Aliendelea na masomo yake ya chuo huku penzi hilo jipya likionekana kumbadilisha kwa kiasi fulani, hakuonekana kuwa mtu wa kuumizwa tena na mapenzi, moyo wake tayari ulikuwa umepata tumaini lingine, alimpenda sana Fedrick kwake mwanaume huyo alimuona kuwa sawa na malaika ambaye alikuja kipindi asichokitarajia. ****
Richard hakuwa tayari kuona Monalisa anaendelea kuubeba ujauzito, alichoamua kukifanya ni kumshauri autoe ujauzio huo lakini hilo lilikuwa ni jambo gumu mno kuweza kufanyika, Monalisa hakuwa tayari kufanya kitendo hicho.
Alizidi kuchanganyikiwa baada ya kusikia kuwa Evelyne alikuwa ameshampata mwanaume mwingine, hakutaka kuamini ilibidi atafute nafasi ya kuzungumza na msichana huyo ambaye moyo wake ulikuwa bado unampenda sana.
“Naomba uniache na maisha yangu,” alisema Evelyne.
“Siwezi kufanya hivyo hata mara moja nakupenda Evelyne,” alisema Richard.
“Upendo wako hauna faida tena kwangu.”
“Kwanini unasema hivyo kwanini unauumiza moyo wangu?”
“Siamini kama kweli ninauumiza moyo wako ila jaribu kuchunguza sababu ya maumivu yako.”
“Evelyne nataka urudi kuwa wangu.”
“Kwasasa haitawezekana kwasababu moyo wangu anaumiliki mwanaume mwingine.”
“Yupi.”
“Fredrick.”
“Hapana Evelyne, Hapana.”
“Huo ndiyo ukweli.”
“Nakupenda Evelyne.”
“Nilikupenda Richard,” alisema Evelyne kisha akaondoka eneo hilo.
*
*
Je, nini kitaendelea?
Usikose sehemu ijayo.
Monalisa king'ang'anizi kama rubaSehemu ya 36.
“Nina ujauzito wako.”
Yalikuwa ni mazungumzo mafupi yaliyofanyika ndani ya chumba cha kifahari cha hoteli hiyo, Richard hakutaka kuamini aliposikia kuwa Monalisa alikuwa amebeba ujauzito wake, ilikuwa ni taarifa ya ghafla! ambayo ilimshtua sana, moyo wake haukumpenda hata kidogo msichana huyo na kwa wakati huo alikuwa tayari ameshaubeba ujauzito wake, hilo lilizidi kumchanganya.
“Umebebaje ujauzito lakini?” aliuliza Richard kwa ghadhabu.
“Kwani ukiingia unaingiaje inamaana umesahau jinsi ulivyokuwa umelala na mimi?” alijibu Monalisa.
Richard alishikwa na kigugumizi mara baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa msichana huyo, hakutaka kumuamini alihisi labda alikuwa akimdanganya ili asiweze kumuacha lakini kitu cha kushangaza Monalisa alipoona Richard hamuamini aliamua kutoa cheti cha majibu ya dakatri ambayo yalikuwa yakimuonyesha kweli kuwa ni mjamzito. ****
Mapenzi yaligeuka kuwa mwiba wa maumivu kwa upande wa Evelyne, licha ya moyo wake kumpenda Richard lakini mwanaume huyo tayari alikuwa ameshamsaliti, hilo liliendelea kuwa tukio lililozidi kumuumiza sana, alikosa raha ya maisha, alishindwa kusoma, ulimwengu wa mapenzi alichukia.
Maumivu ya kimapenzi hayakuishia kwa kusalitiwa tu bali alizidi kuumia mara baada ya kusikia kuwa Monalisa alikuwa amebeba ujauzito wa Richard na ujauzito huo ndiyo ulizidi kumfanya azidi kumchukia mwanaume huyo.
“Sidhani kama nitakuja kupenda tena katika maisha yangu,” alisema Evelyne huku akijiapiza.
“Usiusemee moyo huwezi kujua nini kitakachotokea baadae,” alisema Happy.
“Sijui Happy kama nitapenda tena moyo wangu unakidonda na sijui kama kitapona na hata kama kikipona bado kitaniachia jeraha la maisha,” alisema Evelyne huku machozi yakianza kumdondoka.
Kipindi ambacho moyo wa Evelyne uliweza kupata maumivu ya kimapenzi, alijikuta akiwa ni mpenzi wa kuperuzi mtandao wa kijamii wa Instagram, aliuamini mtandao huo na ndiyo ambao uliweza kumsahaulisha maumivu yote ya kimapenzi ambayo moyo wake ulikuwa umeyapata.
More episodes please:Sehemu ya 40.
Fredrick alimpeleka Evelyne nyumbani kwake alipokuwa anaishi, siku hiyo Evelyne kila kitu alichokuwa akikiona kwa Fredrick kiliweza kumshangaza, licha ya umri mdogo aliyokuwa nao mwanaume huyo lakini alikuwa tayari ameshajipanga kimaisha.
“Hapa ni kwako?” aliuliza Evelyne alipoingia nyumbani kwa Fredrick.
“Hapana ni kwako pia,” alijibu Fredrick huku akimtazama Evelyne ambaye kwa muda huo alikuwa akitazama samani zilizokuwa ndani ya nyumba hiyo.
Fredrick hakutaka kumuacha Evelyne aendelee kumuuliza maswali mengi kwa wakati huo, alichoamua kukifanya ni kumuuliza aina ya kinywaji ambacho alikuwa anatumia baada ya kuketi katika sofa.
“Unatumia Juisi, maziwa au soda?” aliuliza Fredrick huku akimtazama Evelyne.
“Niletee chochote,” alijibu Evelyne kwa sauti ya aibu.
“Ndiyo maana nikakutajia inabidi uchague kimoja wapo hapo,” alisema Fredrick.
“Ok basi niletee juisi.”
“Unapenda ya tunda gani?”
“Lolote lile mimi natumia,” alijibu Evelyne kisha Fredrick akaenda kumletea.
Evelyne hakutaka kuamini kama kweli mwanaume huyo alikuwa peke yake siku zote hizo, huo ulikuwa ni wasiwasi uliyoanza kumuingia mara baada ya kuyaona mazingira ya nyumba hiyo jinsi yalivyokuwa mazuri.
“Karibu,” alisema Fredrick baada ya kurudi, mikononi alikuwa amebeba glass mbili, moja ilikuwa ni ya juisi na nyingine ilikuwa ni ya maziwa. Alipomkaribia Evelyne alimpatia ile glass ya juisi halafu na yeye akaketi pembeni yake, mkononi alikuwa amebakiwa na glass ya maziwa.
Wakaanza kunywa taratibu huku wakitazamana kwa macho ya kuibianaibiana.
“Nikuulize kitu?” aliuliza Evelyne.
“Ndiyo niulize,” alijibu Fredrick.
“Kwani unaishi na nani hapa?”
“Mwenyewe.”
“Una uhakika?”
“Ndiyo.”
“Hauna mwanamke mwingine kweli?”
*
*
Je, nini kitaendelea?