Nisaidieni, upendo unapungua kwa mume wangu

Wapendwa poleni na majukumu ya kujenga taifa.Niende kwenye hoja yangu ,Mimi ni mdada/mama mwenye mtoto 1,nimeolewa na ndoa ya kanisani

Mume wangu alifiwa na wazazi wote wawili kitambo sana,sasa upendo kwangu haupo najitahidi sana nimletee vizawadi nikitoka kazini,amekuwa ni mtu wa kulalamika kuwa yeye upendo wake ulishaondoka na wazazi wake ,kiujumla anasema wazazi wake wangekuwepo angeishi maisha ya furaha sana,eti anaona maisha yote ni ubatili.

Kuna siku moja alinambia anashangaa wanaume wanaowanunulia wake zao nguo au kuwasomesha watakuwa wapumbafu na wajinga,anajali zaidi mtoto wake ,kwakweli ni mtu wa hasira nikikosea kidogo ni kipigo na akiongea kugomba nanyamaza kimya,but yeye anafanya makosa makubwa namsamehe ,kwasababu ukimwambia kwa kumshauri anakuja juu.

Pili ni mbinafsi sana kiasi inapelekea uchoyo wa hali ya juu.Nasema hivi nilivoolewa mimi nilikuwa nawasaidia ndugu zake,niliwachukulia km ndugu zangu but nikaona mwenzangu kwetu hajali babaangu mzazi alilazwa wiki mbili nilikuwa natuma hela,yeye hata senti tano kwamba anisupport hata kupiga cm kumjulia hali mgonjwa hakuweza ,nilivolalamika akanambia nichukulie jinsi nilivo univumilie ndivo nilivo.

Ila nami nachoka ,yeye ni mwajiriwa ana kipato kikubwa zaidi yang.Nisaidieni kwa mawazo naona maisha ya ndoa magumu sana.
Aiseee! Kaa chini utafakari mlipokutana mwanzo ilikuwaje na kadri mlivyoendelea uliendelea kuvifanya hivyo vitu, maana inawezekana kuna jambo ulilifanya na kumfanya apoteze upendo juu yako
 
Kwakweli nimeshangaa,mwanaume ni mchoyooo balaa,uwiiiii
Ila mi nigemfurahisha,hiyo samaki tungekula wote,na hela aliyonisonesha nisingempa!
Halafu ningempotezea
Ht mm nisingemlipa hiyo hela, yaan angedai mpk angekoma.
Kakutana na mwanamke mpole
 
kuna aina za abuse binadamu anaweza kuvumilia ila sio kupigwa. maneno hayaui ila ngumi zina athari kubwa. kuna mama na mtoto wake huku mtaani wapo kama watu wenye ulemavu wa akili kwa sababu baba alikua anawapiga kila kukicha. jamaa mtu mzima tu na smart kweli ila ukimwangalia unaona kabisa hayuko sawa.. physical violence ina madhara makubwa sana.
Abuse ina aina nyingi

Kuna mtu hapigi wala haongei ila hatoi emotional support yoyoote hio ni emotional abuse kwa kuwa we expect mume/mke ndiye wa kutoa msaada wa kihisia

Ipo verbal abuse hupigwi ila mtu anakusema maneno ya kushusha utu wako nk

Sema tu physical ndo mbaya zaidi ktk zote mana unajeruhiwa mwili kwa maumivu ya papo hapo na unaona nundu hioo inaumuka na bado unajeruhiwa nafsi ndani
 
Nimekerekwa hatari. Sema jamani kutoka kwenye ndoa ni ngumuuu unawaza macho ya watu mtaani,watoto n.k
Jamii inapenda kusema watu vibaya hasa wanawake
Akitoka kwny ndoa kosa..bila kujali nini kimemtoa
 
Wapendwa poleni na majukumu ya kujenga taifa.Niende kwenye hoja yangu ,Mimi ni mdada/mama mwenye mtoto 1,nimeolewa na ndoa ya kanisani

Mume wangu alifiwa na wazazi wote wawili kitambo sana,sasa upendo kwangu haupo najitahidi sana nimletee vizawadi nikitoka kazini,amekuwa ni mtu wa kulalamika kuwa yeye upendo wake ulishaondoka na wazazi wake ,kiujumla anasema wazazi wake wangekuwepo angeishi maisha ya furaha sana,eti anaona maisha yote ni ubatili.

Kuna siku moja alinambia anashangaa wanaume wanaowanunulia wake zao nguo au kuwasomesha watakuwa wapumbafu na wajinga,anajali zaidi mtoto wake ,kwakweli ni mtu wa hasira nikikosea kidogo ni kipigo na akiongea kugomba nanyamaza kimya,but yeye anafanya makosa makubwa namsamehe ,kwasababu ukimwambia kwa kumshauri anakuja juu.

Pili ni mbinafsi sana kiasi inapelekea uchoyo wa hali ya juu.Nasema hivi nilivoolewa mimi nilikuwa nawasaidia ndugu zake,niliwachukulia km ndugu zangu but nikaona mwenzangu kwetu hajali babaangu mzazi alilazwa wiki mbili nilikuwa natuma hela,yeye hata senti tano kwamba anisupport hata kupiga cm kumjulia hali mgonjwa hakuweza ,nilivolalamika akanambia nichukulie jinsi nilivo univumilie ndivo nilivo.

Ila nami nachoka ,yeye ni mwajiriwa ana kipato kikubwa zaidi yang.Nisaidieni kwa mawazo naona maisha ya ndoa magumu sana.

Pole sana mamy,hakika kuna wanaume wana mioyo kama ya simba Mwenyezi Mungu akutie nguvu na ambadilishe moyo wake
 
Kipindi nimefunga ndoa siku hiyo usiku ,alinambia nimekuoa but wasichana was nje siwezi waacha ,but kipindi cha a mwanzo nimepata Shida sana ,nikawaona wasimamuzi wangu wa ndoa wakamshauri akapunguza but nilimshakamata kalala na binti wa kazi ndani,nikamwambia naomba tuachane hapo mtoto akiwa na miaka 3 ,akanibembembeleza sana,akaomba msamaha yakaisha,but kuna kipindi akawa anatongoza mabinti ,nikasema sasa inabidi tuachane ,akalia sana akasema umeona coz wazazi wangu wamefariki ndo unataka kuniacha sawa,huruma ikaniingia tukayamaliza ,kwa sasa naona ametulia hata Kanisani anahudhuria vizuri tu

wew Aisee ningemjibu nitakuua bure alale na msichana wa kazi labda mimi sio mmachame aisee hapa ulimvumilia kwa kweli adhabu yake ambayo ningempa angechanganyikiwa kwa kweli ....
 
Wapendwa poleni na majukumu ya kujenga taifa.Niende kwenye hoja yangu ,Mimi ni mdada/mama mwenye mtoto 1,nimeolewa na ndoa ya kanisani

Mume wangu alifiwa na wazazi wote wawili kitambo sana,sasa upendo kwangu haupo najitahidi sana nimletee vizawadi nikitoka kazini,amekuwa ni mtu wa kulalamika kuwa yeye upendo wake ulishaondoka na wazazi wake ,kiujumla anasema wazazi wake wangekuwepo angeishi maisha ya furaha sana,eti anaona maisha yote ni ubatili.

Kuna siku moja alinambia anashangaa wanaume wanaowanunulia wake zao nguo au kuwasomesha watakuwa wapumbafu na wajinga,anajali zaidi mtoto wake ,kwakweli ni mtu wa hasira nikikosea kidogo ni kipigo na akiongea kugomba nanyamaza kimya,but yeye anafanya makosa makubwa namsamehe ,kwasababu ukimwambia kwa kumshauri anakuja juu.

Pili ni mbinafsi sana kiasi inapelekea uchoyo wa hali ya juu.Nasema hivi nilivoolewa mimi nilikuwa nawasaidia ndugu zake,niliwachukulia km ndugu zangu but nikaona mwenzangu kwetu hajali babaangu mzazi alilazwa wiki mbili nilikuwa natuma hela,yeye hata senti tano kwamba anisupport hata kupiga cm kumjulia hali mgonjwa hakuweza ,nilivolalamika akanambia nichukulie jinsi nilivo univumilie ndivo nilivo.

Ila nami nachoka ,yeye ni mwajiriwa ana kipato kikubwa zaidi yang.Nisaidieni kwa mawazo naona maisha ya ndoa magumu sana.
Anahitaji kupata ushauri kwa mwanasaikolojia
 
Amen Mpendwa barikiwa kwa ushauri ,nitaangalia namna ya kuufamyia kazi,but sikupenda kanisani wajue kwasababu mimi ni mwenyekiti wa akina mama kanisani ,kuna vitu sitaki wajue kabisa
Na saa nyingine baadhi ya makanisa huko ndo Kuna umbea utajikuta story zako wanazo waumini...... Mamiii mlilie Mungu kajiunge na prayer marathon kabla it's too late yaan uyo mume mbona utashangaa kajiunge embu Mimi nasubiri ushuhuda wako kabla huu mwaka haujaisha
 
Hiyo hali ya maneno machafu na matusi ndo mimi binafsi huwa yananiumiza nikikumbuka but kipigo kanipiga mpaka na kisu but maumivu yake siyafeel kama matusi mpaka anakutukania wazazi ,mfano nilimwambia kwa nini unatoka nje ya ndoa ,akanambia kamuulize mamaako kwanini babako ana...mba nje ,akikupa jibu uje unambie ,yaani roho inaniumaga sana,nikamwambia naomba uwe unanitukana mimi ,usiwaaingize wazazi wangu
Chiiiiisas..... Uyu mwanaume jamaniii
 
Pole sana ndg.
Kabla ya kuingia ndoani ni vyema kumchunguza mwenzio kipindi chote cha mahusiano, ukiona ana vijitabia vya ajabu ajabu afadhari kujiweka pembeni mapema kabla ya kujitwisha zigo la misumari..
Bila shaka kuna baadhi ya tabia zake uliziona mapema kabla ya ndoa ila ukajifariji kuwa atabadilika, tabia ni kama ngozi, kila siku utakuwa ni mtu wa kuombwa misamaha tu.
 
Endeleeeni kuishi kama kawaida.hivyo vizawadi unavyompa ndiyo vinamfanya aone anastahili zaidi yako.kwani nini umeanza kumpa zawadi baada ya kufiwa na wazazi?

Lea mtoto,mud yake itarudi tuu taratibu kabla ya umri unavyoenda.ila kama na wewe umeanza kulipiza visasi kwa kuacha kusapoti ndugu zake umekuwa tatizo.maana wote ni ndugu zenu.usifanye hivyo kwamba naye afanye hivyo kwa ndugu zako hapo unakosea.sababu moyo wa kusaidia ni wa mtu binafsi.inawezekana alikupebdea hilo pia.
 
Biblia inasema linda moyo wako kuliko unavyolinda vitu vingine kwa sababu huko ndiko zinatoka chembe chembe za uzima. We unalinda ndoa na heshima. Kazi kwako.
 
sorry kwa hili swali.....mkiwa faraghani anafurahia kwa kusisimka au??? nani huwa analianzisha kati yenu?? sbb naona kama mbweha na kondoo wanaishi pamoja....mbweha anamla kondo kwa style yake.....umesoma na kuelimika.....hiyo elimu waliyokupa wazazi wako ina faida gani ktk maisha yako...huna raha , huna amani na ni mjamzito....nikwambie mdogo wangu maisha yako ndio furaha yako......msalimie mmeo!!
 
Back
Top Bottom