Nisaidieni, upendo unapungua kwa mume wangu

miss_mbeya

JF-Expert Member
Mar 24, 2015
1,020
2,000
Wapendwa poleni na majukumu ya kujenga taifa.Niende kwenye hoja yangu ,Mimi ni mdada/mama mwenye mtoto 1,nimeolewa na ndoa ya kanisani

Mume wangu alifiwa na wazazi wote wawili kitambo sana,sasa upendo kwangu haupo najitahidi sana nimletee vizawadi nikitoka kazini,amekuwa ni mtu wa kulalamika kuwa yeye upendo wake ulishaondoka na wazazi wake ,kiujumla anasema wazazi wake wangekuwepo angeishi maisha ya furaha sana,eti anaona maisha yote ni ubatili.

Kuna siku moja alinambia anashangaa wanaume wanaowanunulia wake zao nguo au kuwasomesha watakuwa wapumbafu na wajinga,anajali zaidi mtoto wake ,kwakweli ni mtu wa hasira nikikosea kidogo ni kipigo na akiongea kugomba nanyamaza kimya,but yeye anafanya makosa makubwa namsamehe ,kwasababu ukimwambia kwa kumshauri anakuja juu.

Pili ni mbinafsi sana kiasi inapelekea uchoyo wa hali ya juu.Nasema hivi nilivoolewa mimi nilikuwa nawasaidia ndugu zake,niliwachukulia km ndugu zangu but nikaona mwenzangu kwetu hajali babaangu mzazi alilazwa wiki mbili nilikuwa natuma hela,yeye hata senti tano kwamba anisupport hata kupiga cm kumjulia hali mgonjwa hakuweza ,nilivolalamika akanambia nichukulie jinsi nilivo univumilie ndivo nilivo.

Ila nami nachoka ,yeye ni mwajiriwa ana kipato kikubwa zaidi yang.Nisaidieni kwa mawazo naona maisha ya ndoa magumu sana.
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
13,852
2,000
Mumeo ni mmoja wa wale wanaume selfish,uamuzi ni wako kukaa nae au kuachana nae.....mie nakushauri uachane nae bado mapema ukiamua kubaki ujue unatoa sadaka furaha yako...na utabaki miserable for the rest of your life........................

Kuhusu wazazi,nahisi hakupata muda mzuri wa kukubali wamekufa(grieving period)...saa zote ana feel guilty and puzzled kuhusu kifo chao...au anaona wamekufa mapema kabla hajawahudumia kama zawadi ya kumlea......

Kwa kifupi ameyabeba mengi kifuani,ndio maana ukimuudhi kidogo ana snap,dada huyo ni bomu...ondoka kabla hujazaa mtoto wa pili na watatu halafu ushindwe ku move on.
 
interlacustrineregion

JF-Expert Member
Oct 28, 2018
7,144
2,000
Nakusihi waone wahenga wacha Mungu na waliobobea kwenye ndoa angalau zaidi ya miaka 20 au 15 7bu "jungu kuu halikosi ukoko"(wazoefu wa changamoto"

Pia miruzi mingi humpoteza mmbwa/nahodha wengi, chombo huenda mrama"(ushauri utaopewa na Watu wengi toka hapa JF unaweza kuwa mzuri lakini tokana na wingi wa mawazo tofauti tofauti unaweza kukuchanganya 7bu si kila atayechangia hapa JF atakuwa ana nia njema/mbaya na wewe.

Akili za kuambiwa changanya na zako, ushauri wangu siyo sheria hadi ulazimike kuufata.
 
miss_mbeya

JF-Expert Member
Mar 24, 2015
1,020
2,000
mumeo ni mmoja wa wale wanaume selfish,uamuzi ni wako kukaa nae au kuachana nae.....mie nakushauri uachane nae bado mapema ukiamua kubaki ujue unatoa sadaka furaha yako...na utabaki miserable for the rest of your life........................

Kuhusu wazazi,nahisi hakupata muda mzuri wa kukubali wamekufa(grieving period)...saa zote ana feel guilty and puzzled kuhusu kifo chao...au anaona wamekufa mapema kabla hajawahudumia kama zawadi ya kumlea......

Kwa kifupi ameyabeba mengi kifuani,ndio maana ukimuudhi kidogo ana snap,dada huyo ni bomu...ondoka kabla hujazaa mtoto wa pili na watatu halafu ushindwe ku move on.

Nashukuru dear kwa ushauri ingawa ni mama kijacho. Yaani kazini walikataa kunilipia masomo ya master ,ada ilikuwa milioni kama milioni kumi na tano hivi pamoja na research nililipa kama milioni 13,000,000 hivi sasa ikabaki milioni 3 nikamwomba akakataa kunipa ikabidi nikamkopa coz bank nilikuwa najua ana sh.ngapi akanipa baada ya miezi 3 alikuwa ananidai mpaka nikitoka kazini nakosa raha ya kurudi Nyumbani ,ikabidi niingie bank nikope nimrudishie ndo tukawa na amani but roho inaniuma coz kaenda kuweka bank.
 
miss_mbeya

JF-Expert Member
Mar 24, 2015
1,020
2,000
Nakusihi waone wahenga wacha Mungu na waliobobea kwenye ndoa angalau zaidi ya miaka 20 au 15 7bu "jungu kuu halikosi ukoko"(wazoefu wa changamoto"

Pia miruzi mingi humpoteza mmbwa/nahodha wengi, chombo huenda mrama"(ushauri utaopewa na Watu wengi toka hapa JF unaweza kuwa mzuri lakini tokana na wingi wa mawazo tofauti tofauti unaweza kukuchanganya 7bu si kila atayechangia hapa JF atakuwa ana nia njema/mbaya na wewe.

Akili za kuambiwa changanya na zako, ushauri wangu siyo sheria hadi ulazimike kuufata.
Ahsante Mpendwa kwa ushauri ubarikiwe
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
13,852
2,000
Nashukuru dear kwa ushauri ingawa ni mama kijacho ,yaani kazini walikataa kunilipia masomo ya master ,ada ilikuwa milioni kama milioni kumi na tano hivi pamoja na research nililipa kama milioni 13,000,000 hivi sasa ikabaki milioni 3 nikamwomba akakataa kunipa ikabidi nikamkopa coz bank nilikuwa najua ana sh.ngapi akanipa baada ya miezi 3 alikuwa ananidai mpaka nikitoka kazini nakosa raha ya kurudi Nyumbani ,ikabidi niingie bank nikope nimrudishie ndo tukawa na amani but roho inaniuma coz kaenda kuweka bank,

Hongera kwa mama kijacho,

Naona kwako huwezi kujiondoa kwenye huo uhusiano...

i guess mambo mengine ungemshirikisha ndugu yake anayemheshimu sana...

aongee nae...

Itakusaidia kuyatoa kifuani kwako ambayo itakusaidia kurelease tension...

Honestly sioni akibadilika,kwa hio inabidi umchukulie hivyo hivyo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom