Nisaidieni kwa hili!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidieni kwa hili!!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Pindima, Dec 8, 2011.

 1. Pindima

  Pindima JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 349
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Za saa hizi wana jamii wenzangu!!
  ni hivi nimeombwa ushauri nami naomba mnisaidie kuna mzee wangu anataka kununua roli la kusafirisha mafuta lakin mimi nimemshauri anunue roli la kubebea mizigo kwani nahisi linalipa zaidi!!sasa bado hatujafikia muafaka kwasababu wote hatuna uzoefu na hizo biashara nikaona nililete hapa jamvini kwa msaada na maono yenu ni lipi hapo inalipa zaidi!!asanten!!
   
 2. JJ Masselo

  JJ Masselo Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nitakupa ufafanuzi wa biashara hzo zote mbili, a) Lory la kubeba mafuta ni biashara ambayo hasara yake ni ndogo sana kwa maana once ukishalinunua utapata mkodishaji au litakodishwa na mfanyabiashara hiyo ya mafuta, kwa hiyo kukodishwa utalipwa kulingana na mkataba wa makubaliano kwamba ni dollar 4000 kila trip za inje au ni tz kiasi furani ndani ya nchi so utalipwa kama kodi ya nyumba na unaweza kulipwa kwa mkupuo au kwa kila trip chaguo lako.

  Lory la musafirisha mizigo si mara nyingi sana wenye nayo wanapendwa kuyakosidisha kwa mikataba ila wanapendwa wawe wanatafuta wasafirishaji mizigo au wenyewe wanaamua kufanya biashara hiyo ya usafirishaji so mpaka mzigo ujae kwenye lory na uwe unalipa ndo lory litasafiri vinginevyo hakuna safari na pasipokuwepo safari means hakupa income so you chose.

  Take a minuts and think about it
   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,128
  Trophy Points: 280
  Mkuu samahani lakini.

  - thread yako imenikumbusha mbali sana, imenikumbusha hotuba moja aliyo wahi kuitoa raisi msaatu wa awamu ya tatu, ben mkapa.

  - mkuu katika zote hizo si kushauri mnuue yeyote ile, na kama wewe ni muelewa kaa na baba ako jipangeni na tafuteni biashara ambayo ni sustainable mfanye.

  - au je katika hiyo business yenu nisaidie yafuatayo.
  1. Mmeisha andaa mchanganuo wa biashara ya hili roli?
  2. Je mnatageti nini hasa?
  3. Miaka mitano kumi ijayo mnataka kuwa wapi katika hiyo biashara yenu na hilo gari?
  4. Mna wateja wa uhakika?
  5. Au mnataka loli liwe linaishia kukaa kijiweni kusubiria wateja?
  6. Mnaweza kushindana na makampuni makubwa ya usafirishaji hapa tanzania?
  7. Na mnataka kuendesha vipi hiyo business yenu? As a company au

  - mkuu hii dunia tuliomo sio ile ya miaka ya 2000, kuna mabadiliko makubwa sana na unapoanzisha biashara kuwa na malengo na kuwa na mpango kazi wako.

  - biashara ya kwamba na nunua roli halafu kuna ndugu yangu atakuwa analiendasha yameisha pitwa na wakati.
  - je hamna bussiness aidia nyingine ya kufanya? Au hamtaki kuumiza vichwa? Make huku bongo kuna biashara zisizo umiza kichwa ambazo unaweza ziendsha ukiwa kitandani umelala.
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ktk haya magari mawili, ni bora tanker la mafuta. Kwa sababu muda mwingi linasafiri ktk barabara nzuri, hii itapunguza gari kuchoka,pili linakuwa na fixed route na hivyo ni rahisi kujua mapato kwa kadri ya route ilivyo. Hivi ndivyo nionavyo mimi.
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,128
  Trophy Points: 280
  - mkuu hili la mafuta nalo si rahisi kama unavyo zania.
  - haya makampuni mengi yao yana magari yao special ya kubeba mafuta yao.
  Mfano- bp wana magari yao
  - oilcom wanamagri yao
  - total wana magari yao
  - lake oil wanayo yakwao
  mkuu labda kwa zile shell bubu za mtaani ndo wanaweza pata tenda. Kwanza kwa makampuni ya mafuta ndo wana jukumu la ku supply mafuta kwenye shell za wateja wao, means oil kom wansambaza mafuta kwenye shell zao
  - ni kama ilivyo kwenye viwanda vya soda, kiwanda ndo chenye jukumu la kussuply soda kwa wateja na si wateja wakafuate soda kiwandani, hivyo hivyo kwa makampuni ya mafuta.
   
Loading...