- Thread starter
- #121
Thanks kwa kushukuruAsante Sana Mkuu kwa ufafanuzi na majibu makini toka kwako Daktari. Barikiwa.
Thanks kwa kushukuruAsante Sana Mkuu kwa ufafanuzi na majibu makini toka kwako Daktari. Barikiwa.
Ndg kwa uandishi wako unaonekana ni mtaalamu wa fani ya Afya.Mi nafikiria mtu anapoona ana mauvimbe, haraka saana akimbilie hospitali.
Benign kuja kuwa Malignant inawezekana kabisa.
Hivi Mkuu kama una mauvimbe katika matiti, mfano lilianza moja kisha likaja la pili. Je, nini kinapelekea kuwa hivi? Na inaweza ikawa ni dalili ya Malignant Neopalism?
Sometimez linakuwa na maumivu makali sana ila pia kuna muda maumivu yanakata.
Suruhisho ni kujua tatizo la why tinnitus is happening and then you address the cause if possible?Suluhisho ya tinnitus ni nini!?
nadindishaKujichua siyo issue...eleza umeathirikaje
Je haudindishi
Je unawahi fika kileleni
Je huna hamu ya tendo
Je je uwezi endelea zaid ya round moja?
Be specific tunone namna ya kukusaidia
Ndg hongera kwa kutosumbuliwa na magonjwa mbalimbali. Kifupi wewe ni miongoni mwa watu waliobarikiwa na Mungu kuwa na afya njema.
Kwa ufupi hali ya afya ya mtu ni matokeo ya factor mbalimbali zikiwemo:
Vinasaba vya mtu-genetic factors
Lishe
Mfumo wa Kinga (Body immune system)
Mfumo mzuri wa maisha (good health life style)
Mazingira Safi na yasiyo hatarishi
Chanjo
Na mwisho mfumo wa huduma za afya za eneo husika na urahisi wa upatikanaji wake.
Factor hizo zikiwa okay...watu huweza kuishi maisha bila kusumbuliwa na magonjwa.
Hivyo nakushauri keep praying for good health na usisahau ku-maintain mfumo bora wa maisha.
Nashukuru sana kwa ushauri mkuuNdg please kuwa serious na afya ya dogo.
Ni vigumu mm kukupa jibu kipi ni kifaa kizuri coz Sina specifications ya vifaa hivyo kama vinafanana au ni Orginal Vs fake -one.
Je hao waliokuambia utapata kifaa hicho kwa tsh 80,000 ni madaktari au wataalamu wa ENT ?
Unaweza kimbilia cheap Ila kisiwe msaada kwa kijana
Cha mhimu waamini madaktari wa Mhimbili, jichange nenda kawaone wataalamu.
Naelewa changamoto ya kifedha Ila linganisha hiyo laki 370,000 Na usumbufu na kero anazopitia kijana.
Please jipangeni muwahi hospitali
Sawa mkuu nashukuru nimekuelewa.Mkuu umenichekesha ila usijali
Tatizo la utofauti wa sauti ni la kimaumbile tu kama vile Kuna watu wafupi na warefu, weusi na weupe, wenye sauti ya Kwanza vs sauti ya 4 etc.
Tofauti zetu ziko kwenye organ mbili hizi , larnyx na vocal cords na mfumo wa hewa kwenye mapafu. Msukumo wa hewa kwenye koromeo(larynx) na mwitiko (vibration) wa kiwambo Cha sauti (vocal cord) ndo uleta tofauti hizo.
Wakati sababu kubwa ikiwa ni ya kimaumbile , kwenye organ zinazozalisha sauti, mambo mengine ambayo upelekea utofauti wa sauti ni pamoja na
Umri
Matumizi ya sigara na madawa ya kulevya
Personality ya mtu, Kuna watu huzungumza kwa nguvu kuliko wengine
Tamaduni za watu, kuna tamaduni zinamtaka mdada aongee kwa sauti ya chini na mwanaume akaze sauti
Mazingira ya makuzi. Kuna uhusiano wa mtu kukulia mazingira ya watu waongeaji sana na yenye makele na kuwa na sauti kubwa kuliko mtu aliyekua kwenye mazingira ya utulivu sana.
Asante ndgNashukuru sana kwa ushauri mkuu
Pamoja sana mkuuNashukuru sana kwa ushauri mkuu
Ok kakaMkuu nilikucheki pm,kama ukipata mda naomba upitie PM yako..
Soma coment # 72Miguu kufa ganzi inasababishwa na nini je kuna matibabu?
OkSoma coment # 72
Ziko sababu nyingi zinazosababisha ganzi mwilini. Ila upatwapo ganzi tambua mfumo wa never hasa Central au peripheral never umepata shida.
Possible causes ni Kama:
Magonjwa sugu Kama kisukari, Ukimwi na kansa
Kuumia ubongo au uti wa mgongo au magonjwa yanayoasili maeneo hayo ikiwemo stroke
Ukosefu wa vitamin has B-12
Unywaji wa pombe kupitiliza
magonjwa ya zinaaa Kama sphilis
Wakati mwingine ganzi uletwa na side effects za madawa Kama baadhi madawa ya kufubaza VVU
Matibabu utokana na tatizo la msingi ila hata hivyo Kuna dawa zinasaidia wengi kuondoa ganzi.
Kwa matibabu tuwasiliane
Mm nina O naugua kwa soeed ya 4g hasa amoeba haiishiAsante kwa swali zuri.
Nitajibu kwa upana kidogo ili swali lako liwasaidie na wengine wenye swali Kama hili.
Kitaalamu magroup ya damu yaweza kupangwa kwa namna mbalimbali, hata hivyo mfumo wa ABO na Rhesus (Rh) blood grouping ndo unatumiwa sana. Mfumo huu unatupa magroup ya damu kama
Group A
Group B
Group AB
Group O
Magroup haya ya damu hutokana na asili la vinasaba vya mtu ambavyo uvirithi toka kwa wazazi wake.
Jamii mbalimbali zinatofautiana kwa idadi ya asilimia ya watu wenye makundi mbalimbali ya damu. Mfano American watu wenye group O ni wengi zaidi. Denimark ni A na India ni B .
Nikijielekeza kwenye swali la msingi Kuhusu usiano wa kundi la damu na kinga juu ya maradhi . Nianze kwa kusema dhana hiyo ipo Kutokana na Tafiti zilizowahi fanyika katika nchi nyingi za ulaya na Amerika.
Kwa mfano kuna utafiti uliowahi kufanyika Marekani ulionyesha watu wenye group O walikua na kinga dhidi ya ugonjwa wa syphilis(ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ya zinaa).
Hata hivyo matokeo hayo sio universal na watafiti wanadhani findings hizo zilitokana na sehemu kubwa ya jamii hiyo iliwahi kushambuliwa na ugonjwa huo siku za nyuma. Na kwa kuzingatia kuwa population ya America idadi kubwa ni watu wenye Group O ,matokeo hayo hayakushangaza watafiti.
Ziko tafiti zingine ziliwahi onyesha watu wenye group AB walikua na kinga juu ya ugonjwa wa kipindupindu zaidi ya wale wenye group A and B.
Nikihitimisha hoja ya swali lako la msingi. Si kweli katika jamii zote watu wenye group O wana Kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa. Coz magonjwa ya zinaa yako mengi na hakuna uhusiano wa moja kwa moja na uwepo wa Kinga zidhi ya magonjwa hayo na mtu kuwa na damu kundi O.