Mimi natokwa sana na jasho kwapani kiasi hadi nikivaa nguo nyeusi inaacha alama ya chumvi, kwakweli nakosa raha kabisa, msaada wako tafadhali
Pole ndg
Tatizo la kutokwa jasho lisilo la kawaida linawasumbua wengi. Mara nyingine humfanya mtu kupoteza ujasiri na unazifu wake coz y
jasho na harufu itokanayo na tatizo hili.
Nianze kwa kusema hivi, kutokwa jasho jingi Mara nyingi huwa ni harmless, ila ikitokea kuwa unatokwa jasho hadi inakua kero hapo nilazima kuchukuawa hatua za kukabiliana na tatizo hilo.
Kuna utokwaji wa jasho mwili mzima, kiasi kwamba mtu hata akifanya kazi nyepesi tu jasho linakua jingi na kumsumbua mhusika.
Ila Kuna aina nyingine jasho linakua maeneo maalumu tu Kama kwenye kwapa, shingoni, usoni , miongoni, au sehemu za siri na kwenye mapaja.
Kutokwa jasho kunaweza sababishwa na mambo mengi Kama stress and fear, homa, ujauzito, kitambi, ukomo wa hedhi yaani menopause, au mazoezi. Mara nyingi mambo haya yakiwa addressed maisha uendelea.
Sababu zingine zinafanya tatizo kuwa endelevu na pengine kuleta kero kubwa kwa mtu. Mfano watu wenye maradhi kama hyperthyroidism, parkinsonism, rheumatoid arthritis, Gout, au lymphoma. Watu wenye matatizo haya jasho liwatokalo mara nyingi huwa ni mwili mzima na uweza ambatana na homa .
Kitaalamu tunaweza kugawa tatizo la kutoka na jasho jingi Kama ifuatavyo.
1: primarily hyperhidrosis: ni pale sababu yake haitambulikani, watafiti wanazani tatizo hilo uanza toka utotoni, na wengi huusianisha na namana sweat glands-(tezi za jasho) zilivyo sensitive na uzaniwa Kuna elements za vinasaba.
2: Secondary hyperhidrosis: Ni pale tatizo la kutokwa jasho jingi linakua na kisababishi Kama maladhi ya mwili (Kama nilivyo yaorodhesha hapo juu) au mabadiriko ya kihomoni.
Kwa msingi huo niruhusu nijibu swali lako la msingi. Kutokwa na jasho jingi hasa kwapani inaweza kuwa linaangukia kwenye aina ya kwanza primary hyperhidrosis.
Ikiwa jasho linakua metabolize na bacteria, tatizo hili uambatana na harufu kali inayogeuka kero na kuondoa utanashati wa mtu.
Tiba yake Mara nyingi ni supportive kwa maana ya hatua za kupunguza jasho na kudhibiti harufu Kama:
Kuhakikisha mwili unakua safi
Unywaji wa maji mengi
Kuhepuka animal products foods
Matumizi ya antiperspirants
Matumizi ya deodorant
Unaweza tumia umeme hafifu kublock tezi za jasho -Iontophoresis
Matumizi ya botulinum toxins
Matumizi ya anticholinergic drugs
Na Kama njia hizo juu zitafeli basi upasuaji mdogo ufanyika kuziharibu tezi za jasho ...but this method is reserved for worth scenarios.
Namna ya matumizi ya vitu hivyo unaweza patiwa na dk hasa dematologist au physician.
Tumia mawasiliano yangu niliyoweka huko juu tuwasiliane kwa msaada zaidi