Baba mtakatifu91
JF-Expert Member
- Apr 25, 2026
- 3,674
- 7,633
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA
MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA (TMDA)
ISO 9001: 2015 IMETHIBITISHWA
TAARIFA KWA UMMA
23 Juni, 2026
KUPIGWA MARUFUKU KWA MATUMIZI YA DAWA ZENYE KIAMBATA HAI CHENYE JINA LEVAMISOLE
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) inafanya kazi ya ufuatiliaji wa bidhaa za tiba zilizosajiliwa nchini kwa kupokea na kupitia ripoti za kiusalama kutoka ndani na nje ya nchi ambapo taarifa husika hukusanywa, kuchambuliwa na kisha kuwasilishwa katika Kamati ya Kitaalamu ya Usalama wa Dawa (VTC) kwa ajili ya tathmini na ushauri.
Kupitia utaratibu huo, TMDA imebaini kuwa dawa za binadamu zenye kiambata hai cha Levamisole, zinazotumika kutibu maambukizi ya minyoo, zinaweza kusababisha ugonjwa katika mfumo wa fahamu unaojulikana kitaalamu kama Leukoencephalopathy. Usipotibiwa mapema, ugonjwa huu huleta madhara makubwa ya kiafya, ikiwa ni pamoja na vifo kwa watumiaji.
Kutokana na muktadha huo, TMDA inapenda kuujulisha umma kuwa dawa zote zenye kiambata hai cha Levamisole zimepigwa marufuku katika soko la Tanzania. Hivyo, dawa hizo hazitaruhusiwa kutengenezwa, kuingizwa, kusambazwa wala kuuzwa nchini kwa matumizi ya binadamu.
Vilevile, waagizaji na wasambazaji wote wa dawa hizo wanaelekezwa kusitisha shughuli husika mara moja kuanzia tarehe ya tangazo hili, na kuziondoa sokoni.
HABARI: TMDA ZUIA DAWA ZENYE KIAMBATA CHA LEVAMISOLE.