Niruhusu nikusaidie kutatua changamoto yako kiafya

pureman2

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
1,494
2,538
Salaam JF,

Kama mtaalamu wa afya Mungu amenipa msukumo wa kukusaidia kiushauri juu ya changamoto ya kiafya inayokukabiri. Wataalamu tunaamini kutambua msingi wa tatizo ni hatua mhimu katika kulitatua. Natarajia kukusaidia wewe mwana JF na kama si wewe basi ndg yako au jamaa wako wa karibu.

Kimaadili ya kitaaluma sitakiwi kujitangaza nafanya kazi wapi ili isionekane najipigia upatu unaoweza kulenga kujinufaisha, ila ntaomba ushirikiano wako ili ku-maintain doctor- patient relationship, utakaojengwa kwa msingi wa mutual respect.

Kimsingi, mimi ni mtaalamu wa fani za afya. Ni mtumishi wa umma na ninauzoefu wa miaka isiyozidi kumi kwenye field hii. Hivyo mambo ya msingi kiutendaji na kimfumo ninayafahamu na kwa msingi huo ninao uwezo wa kukusaidia kitaalamu juu ya issue mbalimbali za kiafya japo kwa sehemu ili kufanikisha wewe au ndugu yako kuwa na afya njema na ustawi

Context ambayo nataka uitumie ni kuuliza swali la kiafya linalokusibu either kwa kutaja dalili za hali ya kiafya inayokutatiza nami nitakusaidia kujua msingi wa tatizo na kukupa options za tiba kwa muktadha wa conventional medicine yaani tiba ya kitaalamu na sio tiba asili.

Kwa kuzingatia unyeti wa suala la afya, nitakuwa huru kupokea maoni ya wataalamu wenzangu ili kuboresha na kuhakiki kile ntakachokua nakishauri ili ku-ensure safety ya watu wetu. Na kwa msingi huo ntajitahidi kushauri kile tu kinachokubarika as best practice kwenye fani yetu na si vinginevyo.

Kwa watakaojitokeza kupata msaada wangu ninaomba uvumilivu wao hata Kama nitachelewa kukupa msaada unaoutaka. Kumbuka ninashughuri zingine nyeti kwa ujenzi wa Taifa ila nimekusudia kutenga muda ili nitoe mchango wangu kwa jamii.

Idea hii nitaanza kuitekeleza kwa familia hii ya JF ila baadaye na kusudia kuipanua kwa jamii pana ya Watanzania. Hivyo wale wadau wa afya ntaomba ushirikiano wao ili kusaidiana kufikia lengo la uzi huu.

Nakukaribisha ndg yangu ili unufaike na ushauri wa kitaalamu kwa tatizo lako la kiafya yaani medical consultation.
 
ni kweli wenye damu kundi 0 wana kinga ya magonjwa ya zinaa.?
Asante kwa swali zuri.

Nitajibu kwa upana kidogo ili swali lako liwasaidie na wengine wenye swali Kama hili.

Kitaalamu magroup ya damu yaweza kupangwa kwa namna mbalimbali, hata hivyo mfumo wa ABO na Rhesus (Rh) blood grouping ndo unatumiwa sana. Mfumo huu unatupa magroup ya damu kama
Group A
Group B
Group AB
Group O

Magroup haya ya damu hutokana na asili la vinasaba vya mtu ambavyo uvirithi toka kwa wazazi wake.

Jamii mbalimbali zinatofautiana kwa idadi ya asilimia ya watu wenye makundi mbalimbali ya damu. Mfano American watu wenye group O ni wengi zaidi. Denimark ni A na India ni B .

Nikijielekeza kwenye swali la msingi Kuhusu usiano wa kundi la damu na kinga juu ya maradhi . Nianze kwa kusema dhana hiyo ipo Kutokana na Tafiti zilizowahi fanyika katika nchi nyingi za ulaya na Amerika.

Kwa mfano kuna utafiti uliowahi kufanyika Marekani ulionyesha watu wenye group O walikua na kinga dhidi ya ugonjwa wa syphilis(ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ya zinaa).

Hata hivyo matokeo hayo sio universal na watafiti wanadhani findings hizo zilitokana na sehemu kubwa ya jamii hiyo iliwahi kushambuliwa na ugonjwa huo siku za nyuma. Na kwa kuzingatia kuwa population ya America idadi kubwa ni watu wenye Group O ,matokeo hayo hayakushangaza watafiti.

Ziko tafiti zingine ziliwahi onyesha watu wenye group AB walikua na kinga juu ya ugonjwa wa kipindupindu zaidi ya wale wenye group A and B.

Nikihitimisha hoja ya swali lako la msingi. Si kweli katika jamii zote watu wenye group O wana Kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa. Coz magonjwa ya zinaa yako mengi na hakuna uhusiano wa moja kwa moja na uwepo wa Kinga zidhi ya magonjwa hayo na mtu kuwa na damu kundi O.
 
Nina miaka 5 bila kuugua hata homa wala malaria au tumbo! Na siombi kuugua ila napenda kufahamu siri ya hii hali kwenye hiyo field yako ya udaktari?
Ndg hongera kwa kutosumbuliwa na magonjwa mbalimbali. Kifupi wewe ni miongoni mwa watu waliobarikiwa na Mungu kuwa na afya njema.

Kwa ufupi hali ya afya ya mtu ni matokeo ya factor mbalimbali zikiwemo:

Vinasaba vya mtu-genetic factors
Lishe
Mfumo wa Kinga (Body immune system)
Mfumo mzuri wa maisha (good health life style)
Mazingira Safi na yasiyo hatarishi
Chanjo
Na mwisho mfumo wa huduma za afya za eneo husika na urahisi wa upatikanaji wake.

Factor hizo zikiwa okay...watu huweza kuishi maisha bila kusumbuliwa na magonjwa.

Hivyo nakushauri keep praying for good health na usisahau ku-maintain mfumo bora wa maisha.
 
Baada ya kudhohofu ghafla na kukimbizwa hospital nikagundulika nina kisukari, kijana mwenye under 30 ghafla nikaanza kuangaikia afya, hadi sasa sijajua njia sahihi za kuishi hili sukari i balance.
Msaada juu ya ugonjwa huu unaonitesa sukari.
Pole ndg kwa madhira haya.

Kaa ukijua kuwa hauko peke yako. Tatizo ka kisukari ni kubwa duniani kote na linakua kwa kasi katika nchi zinazoendelea.

Inakadiriwa asiliamia 3.6,( sawa na watu 897000) kati ya watanzania wenye umri juu ya miaka 25 walikua na ugonjwa wa kisukari (Takwimu za 2017).

Kifupi kisukari ni ugonjwa unaotokana na tatizo la homoni iitwayo insulin inayokontrol kiwango cha sukari mwilini. Either mwili unashindwa kuizalisha homoni hii (Diabetic type 1) au mwili kushindwa kuitambua hormone hiyo mwilini (Diabetic type 2). Type 1 ni common kwa watoto na type 2 ni common kwa watu wazima wenye uzito uliokithiri.

Kwa msingi huu ni vizuri kutambua wewe una kisukari aina gani kabla ya kujua namna tiba yako itakavyokua.

Yafuatayo ni mambo ya msingi Kuhusu tiba ya kisukari.

Kisukari ni miongoni mwa magonjwa sugu na tiba yake ni ya maisha.

Ukiwa una kisukari type 1 wewe ni lazima utumie insulin Kama tiba .

Ukiwa na kisukari type 2 , balance ya lishe, na dawa za kumeza za sukari zinaweza kuwa sehemu ya maisha yako. Na Kama zitafeli basi insulin itakuhusu.

Ni mhimu kuhakikisha unapata tiba ili kubalance blood sugar, vinginevyo unajiweka kwenye hatari ya kupata complications za kisukari zikiwemo
Kupungua Kinga ya mwili
Kuharibu mfumo wa nerve
Kuharibu figo
Kuleta upofu
Kuleta vidonda visivyopona ambavyo upelekea kukatwa kwa viungo vya mwili n.k

Nimejibu kiujumla ila nategemea maswali more specific kutoka kwako. Karibu ndg tusaidiane.
 
ET ni tatizo au ni kawaida kwa korodani moja kuwa kubwa zaid na moja ya kawaida kwa mtoto mdogo wa miaka mitatu
Ndiyo ndg
It's common kuwa na utofauti wa korodani kwa watoto. Na Mara nyingi korodani ya kuria huwa kubwa ukilinganisha na ya kushoto. Na pia korodani ya kushoto huwa inaninginia chini zaidi ukilinganisha na ya upande wa kulia.
 
Back
Top Bottom