Shukran kwa uzi murua na ubarikiwe kwa kujitoa kuhudumia jamii.
Binafsi napenda kujua reasons za missed abortion, na how to prevent it, na je kama mtu akipata missed abortion kwa mimba ya kwanza je kuna possibilit ya kujirudia tena??
Pole kwa uvumilivu. Sikuweza jibu swali lako kwa Wakati.
Kuhusu swali lako umeuliza reasons for missed abortion, Ila ntajaribu kuongelea abortion kwa ujumla has non elective abortion ambayo ufanyika pale kunapokua na grounds za ujauzito Kama utaachwa kuendelea basi afya ya Mama itakua matatani.
Missed abortion Mara nyingine huitwa missed miscarriage Ni hali ambayo kichanga au fetus ushindwa kuumbika au hufa Wakati nyumba ya uzazi inakua Bado iko intact.
Ila spontaneous abortion au miscarriage Ni ile hali ya ujauzito kutoka/kuharibu a kabla ya kutimiza wiki 20.
Kimsingi sababu zinazopelekea ujauzito kuharibika zaweza kuwekwa kwenye makundi makuu 2. Sabu za kinasaba / chromosome au sababu za kiafaya (medical reasons)
Ikiwa inasadikiwa 10-20% ya mimba uharibika. Takwimu zinaweza kuwa kubwa zaidi ya hizo kwani Mara nyingi mimba uharibika hata mwanamke hajajitambua kama ni mjamzito.
Sababu kubwa za mimba kuharibika utokana na titizo la kinasaba au chromosome linalotokea by chance kipindi kichanga kinapokua katika siku za mwanzo pale ujauzito unapotungwa. Ikiwa itilafu ya ukuaji itajitokeza ,mwili umejijenga kuhakikisha kisichosahii lazima kitolewe ,na hivyo ujauzito lazima utaharibika.
Sababu zingine zinaweza kuwa:
Maambukizi kipindi Cha ujauzito Kama magonjwa ya dhinaa, PID au UTI kali
Ugonjwa wa kisukari
Matatizo ya homoni
Magonjwa ya tezi joto- thyroid disease
Matatizo ya nyumba ya kizazi kama uwepo wa vivimbe- fibroids au shida ya mlango wa kizazi kama -cervical incompetence
Mambo mengine yanayoongeza risk for spontaneous abortion ni
Umri wa mwanamke anaposhika ujauzito. Mfano mama mwenye umri wa miaka 35 ana risk ya 20% ya mimba kuharibika Lakini yule mwenye umri wa miaka 40 na 45 risk zao Ni 40% na 80% respectively.
Viatarishi vingine ni kama
Historia ya mfuatano wa kuharibika kwa ujauzito
Utumiaji wa sigara, pombe kali na madawa ya kulevya
Au invasive procedures kipindi cha ujauzito.
Note: mazoezi , sex au kufanya kazi ofsini hakuna hatari ya kusababisha ujauzito kutoka.
Ni ngumu kuzuia ujauzito usitoke ikiwa sababu ni ile itokanayo na kasoro katika ukuaji wa kichanga-fetus. Upende usipende mwili lazima ukichomoe kiumbe hicho.
Ikiwa Sababu Ni zile za kiafaya, kuwahi clinic na kutunza ujauzito chini ya uangalizi wa wataalamu itakusaidia kubaini tatizo na kuchukua hatua stahiki.
Nadhani nimekusaidia, Ila usiache kuuliza swali mahala nilipokuacha.