Niruhusu nikusaidie kutatua changamoto yako kiafya

Niruhusu nikusaidie kutatua changamoto yako kiafya

Dr,nisaidie nina mwaka sasa na miezi miwili toka nitembee na binti positive wa VVU toka kipindi hicho nimekua napata dalili tofauti tofauti kama ulimi kuwa mweupe,,kichwa mwanzo kiliuma sana na presha ikapanda ila kwa sasa kimetulia,kuhisi kama mitoki,,sasa nina tatizo la vipele kuwasha sana nimetumia dawa za alegy lakini vinapoa vinaendelea kuwasha,,,nimepima Mara nyingi sana na Mara ya mwisho siku saba zimepita ila majibu ni Negative,,sorry Dr naweza nikawa na tatizo gani au bado nipo kwenye window period!??? asante
Nimesoma kwa umakini tatizo lako , Kama Daktari ninaweza hisi maumivu uliyonayo. Pole ndg .

Kuhusu VVU ondoa shaka , ikiwa hujashiriki ngono zembe hivi karibuni . Window period ni kipindi kisichozidi week 2-4. Kama vipimo vya HIV Ni negative basi waamini watoa huduma.

Umetaja dalili nyingi sana na hivyo inahitajika clear medical history nzuri ili kujua je dalili hizo ni ugonjwa mmoja au maladhi tofauti.

Kutoka mitoki mingi ni dalili ya systemic infection, ikiwemo maradhi ya kansa za damu au lymphoma.

Ulimi mweupe uenda ikawa ni dalili ya fungus za kinywa....ambazo mara nyingi hutokana na upungufu wa Kinga mwilini

Kupata vipele Mara kwa mara inaweza kuwa allergy au tatizo lingine.

Ntaomba tuwasiliane kwa mawasiliano niliyotoa hapo juu ili nikusaidie kwa ukaribu.
 
Maumivu ya korodani tatizo liaweza kuwa nini?
Pole ndg

Je ulianguka au kupigwa na kitu chochote?
Je ni maumivu tu au pia zinavimba ?
Je ukikojoa unasikia maumivu au kunatoka uchafu usio wa kawaida?
Dalili hii imekuwa kwa muda gani?

Ntaomba unijuze kuhusu maswali hayo hapo juu?

Ikiwa hayo yote huna ...inaweza kuwa ni infection tuiitayo orchatis . Tatizo hili linaweza kutoka na magonjwa ya zinaa.

Hivyo fika Hospitalini mapema utachunguzwa na kupewa dawa sahii
 
Mtoto wa miaka kumi na tatu kudindisha muda wote,nitatizo au ukuaji?kwani mimi ni mwanamke na cjawahi lea mtoto wa kiume.
Swali la pili,ni kwangu mimi binafsi,ninasumbuliwa na minyoo aina ya tegu nimetumia dawa kadhaa ila bado sipona.
Weulitaka awe hanithi
 
Pole ndg

Tatizo la maumivu kwenye joint ambalo linatokana na kupungua kwa ute kwenye joint ni very common kwa watu wengi hasa wazee.

Pia laweza kuwa ni matokeo ya magonjwa tuyaitayo autoimmune disease Kama Rheoumatoid disease s.

Maradhi haya ushambulia joint na kusababisha condition tuiitayo arthritis. Mara nyingi hali hii ikitokea inakua endelevu na sugu.

Chanzo na ukubwa wa tatizo ndo utoa mwanga wa aina ya matibabu yatakayohitajika Kama:
vidonge vya maumivu
Vidonge vyenye virutubisho vya joint na mifupa ( joint support)
Na Wakati mwingine upasuaji wa joint ufanyika.
Na mazoezi.

Kama maumivu ni makali sana nitaomba tuwasiliane kwa ushauri specific.
Sipati maumivu ila nikichuchumaa lazma yalie KWA nimdamrefusana ninasumbuliwa
 
Pole kwa changamoto hizo

Kuhusu shida ya mtoto huyo anayekaribia barehe kuwa na mdindisho muda mwingi sio kawaida. Japo inahitajika historia zaidi na kumchunguza mtoto ningependa kujua kama kipindi amedindisha je anapata maumivu?, Je Kuna dalili zingine Kama kuvimba kwa joints, maumivu ya kifua au tumbo, kupungukiwa na damu , homa za Mara kwa Mara?-.......ikiwa ndiyo mtoto anaweza kuwa na ugonjwa wa seli nundu sicle cell-disease (SC) kwenye condition tuiitayo priapism.

Ila ikiwa mtoto anadindisha ila hakuna maumivu basi inaweza kuwa tatizo la kihomoni. Uwenda amepata kitu tunachokiita premature puberty due male hormone over production. Hali hii uendana na dalili zingine za barehe Kama mtoto kukua zaidi, sauti kuwa na kibesi au kuota vinyweleo vingi Kama mavuzi na nyusi nyingi.

Please hakikishwa mtoto anaonwa na Daktari wa watoto for more evaluation.

Kuhusu tatizo lako la minyoo naomba kuuliza ulijuaje minyoo inajirudia na pia ulijuaje ni aina ya tegu? Kama Daktari alikuchunguza kwa details hizo hawezi shindwa kukutibu.
Asnt kwa maelezo haya,kuhusu mtoto ngoja tuu nimpeleke hosp,ila kuhusu mimi kua na minyoo ni kua hua natoa viyai vyeupe mdomoni,nimeenda hosp na kubadilishiwa dawa zaidi ya mara 3 inajirudia
 
Pole ndg
Je ulianguka au kupigwa na kitu chochote?
Je ni maumivu tu au pia zinavimba ?
Je ukikojoa unasikia maumivu au kunatoka uchafu usio wa kawaida?
Dalili hii imekuwa kwa muda gani?
Ntaomba unijuze kuhusu maswali hayo hapo juu?
Ikiwa hayo yote huna ...inaweza kuwa ni infection tuiitayo orchatis . Tatizo hili linaweza kutoka na magonjwa ya zinaa.
Hivyo fika Hospitalini mapema utachunguzwa na kupewa dawa sahii

Sijapigwa nakitu chochote maumivu wakati wa kukojoa hamna lakini kunamuda nawashwa chini ya penis
 
Habari ndugu.. Kuna ndugu yangu anasumbuliwa sana na kichefu chefu na kutapika na kinaanza asubuh tu akiamka akisha jisaidia hajakubwa mambo yanaharibika.. Amepima vipimo vingi vya damu hakuna kinachoonekana amefanya endoscopy majibu mazuri amefanya abdomen ct scan kilakitu kipo sawa.. Mwezi wa nane huu anatapika kila siku asubuh..na sasa hivi anasema anahisi kama kuna kitu kimekwama kooni.. Msaada tafadhali.
 
Sijapigwa nakitu chochote maumivu wakati wa kukojoa hamna lakini kunamuda nawashwa chini ya penis
Okay , wasiliana nami tuone tunasaidianaje kwa mawasiliano niliyotoa huko juu au njoo PM
 
Habari ndugu.. Kuna ndugu yangu anasumbuliwa sana na kichefu chefu na kutapika na kinaanza asubuh tu akiamka akisha jisaidia hajakubwa mambo yanaharibika.. Amepima vipimo vingi vya damu hakuna kinachoonekana amefanya endoscopy majibu mazuri amefanya abdomen ct scan kilakitu kipo sawa.. Mwezi wa nane huu anatapika kila siku asubuh..na sasa hivi anasema anahisi kama kuna kitu kimekwama kooni.. Msaada tafadhali.
Niwie radhi kwa kuchelewa kujibu

Mpe pole mgonjwa. Tatizo la kichefuchefu sio ugonjwa by itself ila ni dalili ya ugonjwa utakaokua mwilini.
Mara nyingi mgonjwa mwenye homa , mjamzito au anaetumia dawa hupatwa na kichefuchefu. Ila vitu hivyo vikitibiwa , tatizo uondoka.

Ukikuta kichefuchefu kinaendelea inakua inamaanisha tatizo la msingi halijatatuliwa.

Kwa ufupi ziko Sababu nyingi zinazosabisha kichefuchefu kwa muda mreefu, hasa matatizo za mfumo wa chakula, Kama vidonda vya tumbo, Kubeua asidi (GERD), tatizo la mmeng'enyo wa chakula na movement ya chakula-gastroparesis
Sababu zingine zinaweza kuwa tatizo kwenye eneo la ubongo linalocontrol mmeng'enyo wa chakula- automatic dysfunction), migraine headache.
Wakati mwingine laweza kuwa tatizo kubadirika kwa gafla mapigo ya moyo pale mtu anapoamka gafla - postural orthostatic tachycardia syndrome).

Pia mgonjwa mwenye panic atack and fear, anaweza kuwa na tatizo la kichefuchefu.

Kutokana na maelezo yako kuwa uyo ndg yako recently anekua akisikia kitu Kama kinamkwama akimeza chakula..... nahisi anaweza kuwa na tatizo la GERD yaani gastroesophageal reflux disease.

Ningependa kuwasiliana nae kwa ukaribu kabla sijapendekeza tiba .
 
Mwili kua na ganzi husababishwa na Nini? Mkuu
Ziko sababu nyingi zinazosababisha ganzi mwilini. Ila upatwapo ganzi tambua mfumo wa never hasa Central au peripheral never umepata shida.

Possible causes ni Kama:
Magonjwa sugu Kama kisukari, Ukimwi na kansa

Kuumia ubongo au uti wa mgongo au magonjwa yanayoasili maeneo hayo ikiwemo stroke

Ukosefu wa vitamin has B-12

Unywaji wa pombe kupitiliza

magonjwa ya zinaaa Kama sphilis

Wakati mwingine ganzi uletwa na side effects za madawa Kama baadhi madawa ya kufubaza VVU

Matibabu utokana na tatizo la msingi ila hata hivyo Kuna dawa zinasaidia wengi kuondoa ganzi.

Kwa matibabu tuwasiliane
 
Nina strabismus, ninasikia MUHIMBILI wanafanya surgery ya kuweka macho sawa.

Je, ni kweli? Na kuna madhara yoyote yale?
Pole ndg

Sina uhakika ila nitafanya mawasiliano kuthibitosha uwepo wa huduma hiyo.

Ila Kama upo karibu Basi fika Hospitalini pale ukahudumiwe.
 
Baada ya kudhohofu ghafla na kukimbizwa hospital nikagundulika nina kisukari, kijana mwenye under 30 ghafla nikaanza kuangaikia afya, hadi sasa sijajua njia sahihi za kuishi hili sukari i balance.
Msaada juu ya ugonjwa huu unaonitesa sukari.

Pole Sana. Kisukari kinatibika kwa kubadilisha kabisa mfumo/ aina ya vyakula unavyokula.
 
Naomba kujua sababu za vivimbe katika matumbo ya kinamama... Fibroids. Nini Tiba yake mbadala wa upasuaji kwa sababu huwa zinaota Tena baada ya miaka kadhaa. Asante
 
Ziko sababu nyingi zinazosababisha ganzi mwilini. Ila upatwapo ganzi tambua mfumo wa never hasa Central au peripheral never umepata shida.

Possible causes ni Kama:
Magonjwa sugu Kama kisukari, Ukimwi na kansa

Kuumia ubongo au uti wa mgongo au magonjwa yanayoasili maeneo hayo ikiwemo stroke

Ukosefu wa vitamin has B-12

Unywaji wa pombe kupitiliza

magonjwa ya zinaaa Kama sphilis

Wakati mwingine ganzi uletwa na side effects za madawa Kama baadhi madawa ya kufubaza VVU

Matibabu utokana na tatizo la msingi ila hata hivyo Kuna dawa zinasaidia wengi kuondoa ganzi.

Kwa matibabu tuwasiliane
Ahsante nitakutafuta.
 
Mimi natokwa sana na jasho kwapani kiasi hadi nikivaa nguo nyeusi inaacha alama ya chumvi, kwakweli nakosa raha kabisa, msaada wako tafadhali
 
Niwie radhi kwa kuchelewa kujibu

Mpe pole mgonjwa. Tatizo la kichefuchefu sio ugonjwa by itself ila ni dalili ya ugonjwa utakaokua mwilini.
Mara nyingi mgonjwa mwenye homa , mjamzito au anaetumia dawa hupatwa na kichefuchefu. Ila vitu hivyo vikitibiwa , tatizo uondoka.

Ukikuta kichefuchefu kinaendelea inakua inamaanisha tatizo la msingi halijatatuliwa.

Kwa ufupi ziko Sababu nyingi zinazosabisha kichefuchefu kwa muda mreefu, hasa matatizo za mfumo wa chakula, Kama vidonda vya tumbo, Kubeua asidi (GERD), tatizo la mmeng'enyo wa chakula na movement ya chakula-gastroparesis
Sababu zingine zinaweza kuwa tatizo kwenye eneo la ubongo linalocontrol mmeng'enyo wa chakula- automatic dysfunction), migraine headache.
Wakati mwingine laweza kuwa tatizo kubadirika kwa gafla mapigo ya moyo pale mtu anapoamka gafla - postural orthostatic tachycardia syndrome).

Pia mgonjwa mwenye panic atack and fear, anaweza kuwa na tatizo la kichefuchefu.

Kutokana na maelezo yako kuwa uyo ndg yako recently anekua akisikia kitu Kama kinamkwama akimeza chakula..... nahisi anaweza kuwa na tatizo la GERD yaani gastroesophageal reflux disease.

Ningependa kuwasiliana nae kwa ukaribu kabla sijapendekeza tiba .
Mawasiliano yako tafadhali. Ili kuweza kumsaidia
 
Shukran kwa uzi murua na ubarikiwe kwa kujitoa kuhudumia jamii.

Binafsi napenda kujua reasons za missed abortion, na how to prevent it, na je kama mtu akipata missed abortion kwa mimba ya kwanza je kuna possibilit ya kujirudia tena??
 
Back
Top Bottom