Royal Son
JF-Expert Member
- Dec 22, 2016
- 1,640
- 3,119
Habari za mchana. Nimekuwa nikikutana na video mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, hususan mtandao unaokua kwa kasi wa TikTok, zinazoonesha baadhi ya watu wakiogeshwa mkojo, wengine wakinywa, na wengine wakiosha miili yao kwa maji yenye chumvi ya mawe.
Naomba kufahamu, kiafya hali hii inachukuliwaje? Pia, kwa mtazamo wa kiimani au kiroho inaelewekaje, ilhali kwa uelewa wa kawaida mkojo huchukuliwa kuwa uchafu na unaweza kuwa na madhara kwa afya?
=======

JamiiCheck imepitia machapisho na tafiti za afya na kubaini kuwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kuwa kunywa mkojo wa binadamu una faida kiafya.
Tovuti ya UPMC health inabainisha kuwa hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha kuwa kunywa au kutumia mkojo kwa namna yoyote kuwa una manufaa kiafya.
Zaidi Soma SI KWELI - Kunywa ama kutumia mkojo kama tiba ni salama kiafya