Niruhusu nikusaidie kutatua changamoto yako kiafya

Niruhusu nikusaidie kutatua changamoto yako kiafya

Gesi inanisumbua zaidi ya miezi mitatu, nawezaje kupata tiba yake maana dawa za hospitalini zimeshachemka Bosi.@pureman2,
 
Mkuu mimi hua nasikia baridi muda wote..na mwili wangu hasa viganja vyabaridi mno..
Mara nyingi navaa nguo mbili. Naambiwa eti nimemfuata babu wa jina langu maana toka mdogo mm nasikia baridi.
Kwenye baridi nateseka mno ila nikiwa dar joto hua nasikia marachache mno..Shida itakua nini?
Pole mkuu na Asante kwa kutushirikisha.
Hili tatizo la kupata baridi Wakati huna homa sio common sana.

Na wengi walionalo tatizo Mara nyingi ni wanaume ukilinganisha na wanawake.
Zifuatazo zinaweza kuwa sababu ya mtu kusikia baridi sana:

Over sensitivity of cold receptors
Uzito mdogo na wembamba
Upungufu wa hormone ya thyroid- hypothyroidism
Upungufu wa madini ya chuma
Tatizo la mishipa ya damu kusafirisha damu kwenda kwenye lower extremities eg reynaud's disease
Ukosefu wa muda wa kutosha kusinzia
Upungufu wa maji mwilini
Upungufu wa vitamin B12
Ugonjwa wa kisukari

Specific question Kuhusu sababu hizi unaruhusiwa kuuliza.
 
Tuambue ulijuaje hilo. Usilete story za gheto au kwenye kahawa hapa.

Hapa watu wanajadili mambo muhimu ya afya ambayo ni nyeti.

Anzisha uzi wako wa ma dokta feki sio hapa.

Na usipokuja na jibu la kueleweka titakupa vpande vyako.ili kila unapochangia watu wakuelewe. Wajinga kama nyie ndio mnaharobu JF kila mahali una koment tu.
Barikiwa sana mkuu

JF inahitaji sana watu wenye uelewa Kama huu.
 
Pole ndg
Ningependa kujua ni tiba ipi umekua ukipewa ?
Nilipewa vidonge flani hivi rangi ya ukwaju, vyeupe na vidogo vidogo kama piliton na vingine vyeupe vikubwa muundo wa paracetamol zaidi ya siku 28 bila ya mabadiliko yoyote hadi nikapuuzia tena kurudi hospitalini.
 
Mtoto wa miaka kumi na tatu kudindisha muda wote, nitatizo au ukuaji? kwani mimi ni mwanamke na sijawahi lea mtoto wa kiume.
Swali la pili,ni kwangu mimi binafsi, ninasumbuliwa na minyoo aina ya tegu nimetumia dawa kadhaa ila bado siponi.
 
Dr. nisaidie nina mwaka sasa na miezi miwili toka nitembee na binti positive wa VVU toka kipindi hicho nimekua napata dalili tofauti tofauti kama ulimi kuwa mweupe, kichwa mwanzo kiliuma sana na presha ikapanda ila kwa sasa kimetulia, kuhisi kama mitoki.

sasa nina tatizo la vipele kuwasha sana nimetumia dawa za alegy lakini vinapoa vinaendelea kuwasha nimepima Mara nyingi sana na Mara ya mwisho siku saba zimepita ila majibu ni Negative.

sorry Dr naweza nikawa na tatizo gani au bado nipo kwenye window period!?

asante
 
Nina strabismus, ninasikia MUHIMBILI wanafanya surgery ya kuweka macho sawa.

Je, ni kweli? Na kuna madhara yoyote yale?
 
Ninatatizo lakuishiwa na ute kwenye magoti msaada
Pole ndg

Tatizo la maumivu kwenye joint ambalo linatokana na kupungua kwa ute kwenye joint ni very common kwa watu wengi hasa wazee.

Pia laweza kuwa ni matokeo ya magonjwa tuyaitayo autoimmune disease Kama Rheoumatoid disease s.

Maradhi haya ushambulia joint na kusababisha condition tuiitayo arthritis. Mara nyingi hali hii ikitokea inakua endelevu na sugu.

Chanzo na ukubwa wa tatizo ndo utoa mwanga wa aina ya matibabu yatakayohitajika Kama:
vidonge vya maumivu
Vidonge vyenye virutubisho vya joint na mifupa ( joint support)
Na Wakati mwingine upasuaji wa joint ufanyika.
Na mazoezi.

Kama maumivu ni makali sana nitaomba tuwasiliane kwa ushauri specific.
 
Nilipewa vidonge flani hivi rangi ya ukwaju, vyeupe na vidogo vidogo kama piliton na vingine vyeupe vikubwa muundo wa paracetamol zaidi ya siku 28 bila ya mabadiliko yoyote hadi nikapuuzia tena kurudi hospitalini.
Okay
Ni vigumu kuelewa description uliyoitoa.

Tatizo la gesi ni dalili ya maradhi ya tumbo Kama vidonda vya tumbo au shida za mmeng'enyo wa chakula au aina ya chakula Kama ulaji mwingi wa wanga au mafuta.

Taaluma yetu haitoniruhusu kukuandikia dawa hapa , hivyo nakuomba unacheck thru 0752601418- whatsap
 
Mtoto wa miaka kumi na tatu kudindisha muda wote,nitatizo au ukuaji?kwani mimi ni mwanamke na cjawahi lea mtoto wa kiume.
Swali la pili,ni kwangu mimi binafsi,ninasumbuliwa na minyoo aina ya tegu nimetumia dawa kadhaa ila bado sipona.
Pole kwa changamoto hizo

Kuhusu shida ya mtoto huyo anayekaribia barehe kuwa na mdindisho muda mwingi sio kawaida. Japo inahitajika historia zaidi na kumchunguza mtoto ningependa kujua kama kipindi amedindisha je anapata maumivu?, Je Kuna dalili zingine Kama kuvimba kwa joints, maumivu ya kifua au tumbo, kupungukiwa na damu , homa za Mara kwa Mara?-.......ikiwa ndiyo mtoto anaweza kuwa na ugonjwa wa seli nundu sicle cell-disease (SC) kwenye condition tuiitayo priapism.

Ila ikiwa mtoto anadindisha ila hakuna maumivu basi inaweza kuwa tatizo la kihomoni. Uwenda amepata kitu tunachokiita premature puberty due male hormone over production. Hali hii uendana na dalili zingine za barehe Kama mtoto kukua zaidi, sauti kuwa na kibesi au kuota vinyweleo vingi Kama mavuzi na nyusi nyingi.

Please hakikishwa mtoto anaonwa na Daktari wa watoto for more evaluation.

Kuhusu tatizo lako la minyoo naomba kuuliza ulijuaje minyoo inajirudia na pia ulijuaje ni aina ya tegu? Kama Daktari alikuchunguza kwa details hizo hawezi shindwa kukutibu.
 
Mwili kua na ganzi husababishwa na Nini? Mkuu
 
Back
Top Bottom