Niruhusu nikusaidie kutatua changamoto yako kiafya

Niruhusu nikusaidie kutatua changamoto yako kiafya

tatizo la kukosa hamu ya kula inasababishwa na nini?
Ndg tatizo la kukosa hamu ya kula ni tatizo linalowakabiri watu wengi duniani, watoto kwa wakubwa. Kwa sehemu kubwa inatokana na itilafu ya kiafya.
Zifuatazo zinaweza kuwa sababu ya kukosa hamu ya kula.

Maladhi ya mfumo wa chakula
Magonjwa ya kihomoni
Asthma
Diabetes
Magonjwa sugu ya figo na ini
Uongezeko la madini ya calcium
Magonjwa yatokanayo na tezi iitwayo thyroid.

Hata hivyo mgojwa yoyote ambaye ana homa kali hamu ya chakula hupotea.

Ni vizuri kuonana na Daktari mzungumze kwa ukaribu na akufanyie uchunguzi kabla ya mapendekezo ya tiba.
 
Tatizo la madaktari wa kitanzania wanajua kila tatizo la mgonjwa, yani hawaja specialize kwenye idara husika. Unaweza kuona daktar wa meno anamshaur mgonjwa wa ngozi
Ni kweli Hilo ni tatizo
Ila Kuna general knowledge inaweza kutolewa na mtaalamu aliyepata mafunuo hayo. Usiogope kuwashirikisha wanaweza kukusaidia wazo ambalo litakupa msaada zaidi.

I'm sure most doctors knows their limits
 
Inategemea unaonwa wapi na hao madr. Bongo kuna maspecialist wa kila aina
Tatizo la madaktari wa kitanzania wanajua kila tatizo la mgonjwa, yani hawaja specialize kwenye idara husika. Unaweza kuona daktar wa meno anamshaur mgonjwa wa ngozi
 
Nina mgojwa ana kidonda kina kama miaka mitano hakiponi kabisa,,,chanzo cha kidonda ni ajali,,hana sukari wala tatizo lolote.
Pole ndg
Kidonda ndgu ni kiashirio Cha tatizo kubwa. Viko visababishi vingi vya kidonda ndugu ikiwemo bacteria au fungus wenye usugu, tatizo la mishipa ya damu inayolisha eneo linye kidonda, au pengine ni kansa .

Ni vizuri kufika Hospitali inayoweza kufanya vipimo vya histology na biopsy. ( hapa wataalamu watachukua cells au kinyama kidogo toka kwenye kidonda na kukifanyia uchunguzi.)

Majibu ya vipimo hivyo yataongoza aina ya tiba utakayopewa. Pengine ulazimika hata kukata sehemu ya mwili wenye tatizo yaani amputation.

For more specific question ...usiache kuuliza.
 
Je punyeto inasababisha upungufu wa nguvu za kiume?
 
Nasumbuliwa na kifua kikavu,Nikipanda mlima hata mdogo nikifika juu mapigo ya moyo yanaenda kasi sana,mabega na magoti kuchoka na kujiona,mzito nikiwa natembea,nikikaa nje mda mrefu napata baridi na nikisema niogo lazima nitetemeke ila baada ya mda bila kutumia dawa hali hiyo inaondoka yenyewe tararibu kisha inarudi kwa fujo kiasi mda mwingine mapaja yanauma,nikichuchumaa nikiamka asubuhi nisipo Fanya zoezi ndogo LA kuruka kachura hata kwa dk5 ila nilitaka kupima TB ila nikaambiwa mpaka niwe na makohozi ikabidi nipige X-ray na majibu yaliporudi nikaambiwa moyo wangu unaonekana unatanuka ila sababu bado hawajajua kwa nini moyo unatanuka na shughuli zangu ni mfanyabiashara wa kutembea, sasa we kama mtaalam wanishauri ni au ni dalili ya nini
 
Bila kuhoji sana, hata kwa hapa tu ulipofika nikupongeze Dr. Kutumia muda wako kutoa majibu kwa wadau, sio kitu kidogo, inahitaji moyo.

Ila usihau kuwa makwazo hayana budi kuja. Kuna members humu watakuja kuharibu tu, kukejeli nk, ndio pale as a physician unabaki na ile kanuni ya "Big Heart" ili mambo yaende. Kazi njema.
 
Nasumbuliwa na kifua kikavu,Nikipanda mlima hata mdogo nikifika juu mapigo ya moyo yanaenda kasi sana,mabega na magoti kuchoka na kujiona,mzito nikiwa natembea,nikikaa nje mda mrefu napata baridi na nikisema niogo lazima nitetemeke ila baada ya mda bila kutumia dawa hali hiyo inaondoka yenyewe tararibu kisha inarudi kwa fujo kiasi mda mwingine mapaja yanauma,nikichuchumaa nikiamka asubuhi nisipo Fanya zoezi ndogo LA kuruka kachura hata kwa dk5 ila nilitaka kupima TB ila nikaambiwa mpaka niwe na makohozi ikabidi nipige X-ray na majibu yaliporudi nikaambiwa moyo wangu unaonekana unatanuka ila sababu bado hawajajua kwa nini moyo unatanuka na shughuli zangu ni mfanyabiashara wa kutembea, sasa we kama mtaalam wanishauri ni au ni dalili ya nini
Pole ndg

Nitajaribu kukusaidia Kama ifuatavyo. Kwa jinsi ulivyojieleza dalili za msingi ni kiwa una history ya kikohozi kikavu(dry coughing), mapigo ya moyo kwenda kasi hata unapofanya kazi kidogo(awareness of heart beat or palpitations), na mwili kuchoka (body malaise and fatigue).

Nikushukuru kwa kwenda kupima Chest x-ray ambayo wamekueleza kuwa moyo wako umeanza kupanuka.

Japo ningependa kujua your medical history in detail, hasa katika maeneo haya:
Hizo dalili zina muda gani ?
Je kifua kinauma?
Je unapata homa?
Je unatokwa na jasho jingi lisilo la kawaida?
Je usiku pumzi hukata gafla Kama vile umeota ndoto za jinamizi linalokuziba pumzi?
Je umewahi vimba miguu ikawa ukiigusa hasa maeneo ya ankle joint inakua Kama inabonyea Kama ndizi mbivu?
Je unafanya kazi maeneo ye vumbi Kama migodini ?
Je unavuta sigara au kufanya kazi maeneo yenye Moshi mwingi?
Je una high blood pressure (BP) au kisukari au tatizo la ini na Figo?

Majibu ya maswali hayo yatanisaidia hasa ku-stream line tatizo lako. Ila kwa kuzingatia dalili chache ulizozieleza Kuna uwezekano mkubwa tatizo lako kimsingi ni ugonjwa wa moyo yaani heart failure (HF).
HF kwa layman language (lugha isiyo ya kitaalamu) ni pale moyo unaposhindwa kusukuma damu kwenye maeneo mbalimbali ya mwili Kama inavyopaswa. Hali hii usababishwa na vitu vingi ikiwemo tatizo la kupanuka kwa misuli ya moyo, jinsi umeme unavyosafirishwa kwenye moyo, hitilafu kwenye valve za moyo, kuziba kwa mishipa ya damu inayolisha moyo, na Wakati mwingine inaweza kuletwa na sababu zingine nje ya moyo kama upungufu wa damu, magonjwa sugu ya mapafu (chronic lung diseases-COPD), mabadiriko ya kihomoni-hypo/hyper- thyroidism etc.

Kwa msingi huu ni vizuri kufanyiwa general body check up na vipimo kama ECG na ECHO ni mhimu sana.

Chanzo cha tatizo na ukubwa wa tatizo yaani severity ndo vitaongoza ni aina gani matibabu utapatiwa.

Usichoke kujibu maswali yangu nitakusaidia kupata ufumbuzi wa tatizo lako.
 
Maeneo makuu ya kufocus
Ni aina ya chakula na mpangilio wake,
Dose na idadi ya dawa unazomeza na
Jinsi unavyo control uzito na blood pressure yako.

Ntatamani kusaidiana na wewe kwenye maeneo hayo. Tuwasiliane kwenye namba 0752601418 whatsap
Asante mkuu
 
Salaam JF

Kama mtaalamu wa afya Mungu amenipa msukumo wa kukusaidia kiushauri juu ya changamoto ya kiafya inayokukabiri. Wataalamu tunaamini kutambua msingi wa tatizo ni hatua mhimu katika kulitatua. Natarajia kukusaidia wewe mwana JF na kama si wewe basi ndg yako au jamaa wako wa karibu.

Ki maadili ya kitaaluma sitakiwi kujitangaza nafanya kazi wapi ili isionekane najipigia upatu unaoweza kulenga kujinufaisha, ila ntaomba ushirikiano wako ili ku-maintain Doctor- patient relationship, utakaojengwa kwa msingi wa mutual respect.

Kimsingi , Mimi ni mtaalamu wa fani za afya. Ni mtumishi wa umma na ninauzoefu wa miaka isiyozidi kumi kwenye field hii. Hivyo mambo ya msingi kiutendaji na kimfumo ninayafahamu na kwa msingi huo ninao uwezo wa kukusaidia kitaalamu juu ya issue mbalimbali za kiafya japo kwa sehemu ili kufanikisha wewe au ndg yako kuwa na afya njema na ustawi

Context ambayo nataka uitumie ni kuuliza swali la kiafya linalokusibu either kwa kutaja dalili za hali ya kiafya inayokutatiza nami nitakusaidia kujua msingi wa tatizo na kukupa options za tiba kwa mkutadha wa conventional medicine yaani tiba ya kitaalamu na sio tiba asili.

Kwa kuzingatia unyeti wa suala la afya, nitakua huru kupokea maoni ya wataalamu wenzangu ili kuboresha na kuhakiki kile ntakachokua nakishauri ili ku-ensure safety ya watu wetu. Na kwa msingi huo ntajitahidi kushauri kile tu kinachokubarika as best practice kwenye fani yetu na si vinginevyo.

Kwa watakaojitokeza kupata msaada wangu ninaomba uvumilivu wao hata Kama nitachelewa kukupa msaada unaoutaka. Kumbuka ninashughuri zingine nyeti kwa ujenzi wa Taifa ila nimekusudia kutenga muda ili nitoe mchango wangu kwa jamii.

Idea hii nitaanza kuitekeleza kwa familia hii ya JF ila badae nakusudia kuipanua kwa jamii pana ya watanzania. Hivyo wale wadau wa afya ntaomba ushirikiano wao ili kusaidiana kufikia lengo la uzi huu.

Nakukaribisha ndg yangu ili unufaike na ushauri wa kitaalamu kwa tatizo lako la kiafya yaani medical consultation.
Huu uzi upo tayari.

Maxence Melo

Cookie

farid

Paw

unganisheni huu uzi.
 
Mkuu mimi hua nasikia baridi muda wote..na mwili wangu hasa viganja vyabaridi mno..
Mara nyingi navaa nguo mbili. Naambiwa eti nimemfuata babu wa jina langu maana toka mdogo mm nasikia baridi.
Kwenye baridi nateseka mno ila nikiwa dar joto hua nasikia marachache mno..Shida itakua nini?
 
Dokta hujanijibu? Nalo hilo ni tatizo kubwa.
Pole ndg
Kidonda ndgu ni kiashirio Cha tatizo kubwa. Viko visababishi vingi vya kidonda ndugu ikiwemo bacteria au fungus wenye usugu, tatizo la mishipa ya damu inayolisha eneo linye kidonda, au pengine ni kansa .

Ni vizuri kufika Hospitali inayoweza kufanya vipimo vya histology na biopsy. ( hapa wataalamu watachukua cells au kinyama kidogo toka kwenye kidonda na kukifanyia uchunguzi.)

Majibu ya vipimo hivyo yataongoza aina ya tiba utakayopewa. Pengine ulazimika hata kukata sehemu ya mwili wenye tatizo yaani amputation.

For more specific question ...usiache kuuliza.
 
Tatizo la madaktari wa kitanzania wanajua kila tatizo la mgonjwa, yani hawaja specialize kwenye idara husika. Unaweza kuona daktar wa meno anamshaur mgonjwa wa ngozi
Tuambue ulijuaje hilo. Usilete story za gheto au kwenye kahawa hapa.

Hapa watu wanajadili mambo muhimu ya afya ambayo ni nyeti.

Anzisha uzi wako wa ma dokta feki sio hapa.

Na usipokuja na jibu la kueleweka titakupa vpande vyako.ili kila unapochangia watu wakuelewe. Wajinga kama nyie ndio mnaharobu JF kila mahali una koment tu.
 
Je punyeto inasababisha upungufu wa nguvu za kiume?
Ndg naomba nijaribu kutoa maelezo kuhusu swali lako. Katika swali lako la msingi linataka kujua uhusiano wa punyeto na upungufu wa nguvu za kiume.

Nianze kwa kusema hivi neno "upungufu wa nguvu za kiume" ni dhana pana sana. Kitaalamu iko kwenye dhana inayoitwa "sexual dysfunction disorders" , syndrome hii ni mkusanyiko wa matatizo mbalimbali yanaoathiri kutamani, kutenda, kuwa na uwezo wa kutungisha mimba, au kutosheka kwa tendo la ndoa.

Hili ni tatizo kubwa kwa jinsia zote, inakadiriwa asilimia zaidi ya 30 ya wanaume wanakabiliwa na either aina moja au zaidi ya matatizo ya nguvu za kume.

Wapo wenye titizo la kukosa hamu ya tendo kabisa
Wapo wenye tatizo la kudindisha
Wapo wenye tatizo la kuwahi au kuchelewa kufika kileleni
Wapo wenye tatizo la mbegu za uzazi kutokua na nguvu ya kutungisha mimba
Wapo wenye tatizo la kusikia maumivu Wakati wa tendo

Sababu zinazopelekea upungufu wa nguvu za kiume ni nyingi zikiwemo matatizo ya kimaumbile yaani physical disorders e.g ulegevu wa misuli ya uume, medical conditions Kama kisukari, magonjwa ya moyo ini na figo, matatizo ya mishipa ya damu na nerve zinazolisha na kucontrol uume, matatizo ya kihomoni.

Pia matatizo ya kisaikolojia Kama stress zamaisha na mahusihano, sonona (depression), ukosefu wa kujiamini kuhusu body image yako n.k.

Sababu zingine zinaweza kuwa unywaji wa pombe, uvutaji sigara na tumbaku, madawa ya kulevya na hata side effects za madawa tunayotumia hasa kutibu magonjwa ya akili zinaweza pelekea tatizo la nguvu za kiume.

Nimalizie kwa kujibu swali lako la msingi ni kuwa punyeto inaathari kubwa mbili, kulegeza misuli ya uume na kuathiri saikoloji ya mtu. Haya mawili yanaweza pelekea tatizo la kukosa hamu ya tendo na hata kuimili tendo lenyewe kwa muda mrefu.

Usiache kuuliza ikiwa Kuna swali la nyongeza.
 
Back
Top Bottom