Hapo kwenye ukweli ndo wengi wetu tunapofeli,
Mimi binafsi kama ishu ipo nje ya uwezo wangu namwambia mteja au namwelekeza kwa mtu anayeiweza, maana huwezi jua kila kitu,
Na kama kazi itatumia muda mrefu huwa namwambia ukweli aiache au aiende nayo, sasa wengi wa wateja utakuta ananiletea kazi nampa bei na muda utakaotumika atahisi anataka kutapeliwa atawapelekea madalali (maana hawa wanajua kupiga saundi) cha ajabu dalali simu atairudisha tena kwangu (hii wengi wa wateja wetu hawajui) na akiirudisha nampa jibu lile lile la awali atakubaliana na dalali huko mwisho wa siku simu inaletwa kwangu na watu wanne tofauti tofauti na wote wanapata jibu moja tu, sasa huwa najiuliza, inamaana hawa wateja hawatuamini sisi ambao tupo makini na kazi mpaka wanaenda kuwaamini madalali?
Mwingine utakuta ana fremu kabisa lakini ana kazi zake anazoziweza sema kuwa mkweli ndo hataki ataamua kuidalalia tu ili na yeye apate cha juu
Binafsi kumpotezea muda mteja huwa sipendi ndo maana nakuwa muwazi tu, ikinishinda nasema kama siiwezi nakuelekeza kwa mtu anayeiweza
Pia kingine wateja wanapofeli ni kutafuta unafuu wa bei, kama unataka unafuu wa bei nenda moja kwa moja kwa fundi uongee nae bei ukiangukia kwa dalali kazi ambayo unapaswa kulipia 20k utalipia 45k mpaka 50k maana wengi ni vishoka
Bora uende kwa fundi anayekufanyia kazi yako ili hata kama kutakuwa na mabadiliko yoyote yale atakujulisha kuliko vishoka
Kifupi mambo yapo mengi sana ila wacha tu niishie hapa