Nilipokutana na vibaka usiku nikiwa na girlfriend wangu

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,940
6,835
Arusha,

Ilikuwa ni mwezi wa saba kama huu, Mwaka 2017 nilikuwa Ndo nipo form four (Najua me bado nyokaa sana kwa wengi wenu humu ndani ila fresh sio kesi) Ilikuwa ni siku ya sikukuu Ya Eid sijui Maulid sijui kutofautisha hapo mtanisaidia.

As normal bado nilikuwa nategemea wazazi so, Mzee alinipatia kama 10k kwaajili ya kwenda ku-enjoy sikukuu yangu, Siku hiyo ratiba ilikuwa ni kuonana na girlfriend wangu ambae tulikubaliana tukutane ukumbi fulani wa kujidai uliojulikana kwa jina la Mile.... maeneo ya Sakina nafikiri, Nilifika fresh mida ya saa 10 jioni nimependeza fresh yaani nikaingia pale club nikawa nasikiliza mama la mama afike maeneo, Alinidis-appoint maana hakutokea wala kupatikana hadi kufika saa 12jioni ambapo niliamua kurudi zangu home nikiwa nimekwazika sana, Nilipofika Nyumbani ilikuwa kwenye saa 1 kasoro wakati naanza kubadili nguo ndipo nikaona simu yangu inaita (Tecno pop 1 lite ilikuwa ya kutoa betri) kucheki alikuwa Martha ambae ndo alikua Gf wangu nilipokea kwa jazba sana huku nikimuuliza kwanini alivunja appointment akajitetea kwamba home kwao walikuja wageni kuwatembelea hivyo alikuwa na kazi ya kuwahudumia kwanza hadi walipoondoka ndo akapata nafasi na kuhusu sim kutokupatikana alijitetea kuwa ilizima charge, Nilipomuuliza kwahiyo tufanyaje akanambia yeye ndo yupo kwa gari hivyotukutane round about jirani Sheli ya Gapco maana yeye anatokea Sinoni.

Basi kwa kuwa nilikuwa na mihemko mingi sana kukutana na Gf wangu niligahiri fasta zoezi la kubadili nguo na kuanza safari ya kutokea Kaloleni hadi Gapco tulipokubaliana, Basi tulionana fresh ikiwa ilikuwa sasa yapata saa 2 unusu usiku na tukaanza kujiongea ongea hadi katikati ya masoko, mitaa ya jirani na soko kuu tukatafuta restaurant fulani tukaagiza juice tukawa tunakunywa na stori mbili tatu, Before hiyo siku hatukuwahi kuwa na muda mzuri wa kuwa pamoja kama siku hiyo na wala hatukuwahi japo kupata japo busu kutoka kwetu wenyewe, That's why niliubless sana usiku ule.

Tulimaliza kupata kinywaji kile mida ya saa 4 usiku nafikiri ndipo nilipopata wazo kwamba tupate muda wa kutembea tembea kwa njia ya kuzunguka huku nikiwa kama namsindikiza yeye akachukue usafiri pale round about nilipompokea ili arudi kwao sinoni, Wazo likaja tupite barabara ya Sokoine mdogomdogo hadi tukutane na round about ya clock tower then tushuke na barabara ya mkabala na shule ya Arusha school kisha ndo tukutane na barabara ya Fire ambayo ingetufikisha hadi Round about ambayo ndo hiyo ya kuelekea sinoni kwao na hapo ndo palikuwa lengo langu ili achukue gari aondoke kwao.

Wahuni eeeh, Lengo langu kumzungusha vile lilikuwa sio baya bali ni ili japo nipate nafasi ya kum'busu tu (romance) mitaa ya town kule ilikuwa jau maana mitaataa ilikuwa mingi usiku ule, Nilijua kuwa nikifika pale jirani na Arusha school pale kumetulia na kumejificha hicho ningeliweza kuambulia busu kiurahisi na kwa uhakika zaidi. Kikweliii tulipofika nilifanikiwa na adhma yangu hiyo nilipata romance ya nguvu sana kwa yule mtoto (I can't forget the moment ) After pale sasa niliridhika ndipo tukaanza kutembea kwa haraka kidogo, Tukiwa barabara ile ya fire kuelekea tulipokusudia ndipo Gf wangu akaniuliza

Martha: "Hivi bby wewe hunaga hofu?"

Mimi: "Kwanini"

Martha: "We usiku huu wote saa tano sasa inaelekea saa sita na barabarani tupo peke yetu tu ujui ni hatari"

Mimi: Aaah jaman, bby sasa niogope nini wakati magari na bodaboda bado zinapita barabarani (Nilijibu kwa kujiamini na kama kumpuuzia kwamba aache uoga) Wakati huo simu yangu ilikuwa imeshazima charge pia (Tecno smart za mwanzoni zilikuwa miyeyusho sana zile za kutoa betri tofauti na simu za sasa simu hata siku mbili zinamaliza)

Tulitembea hadi tukafanikiwa kulivuka daraja fulani sijui ule mto unaitwaje tena, Nimesahau ila wanaoijua Arusha vizuri naamini wananipata vilivyo... Baada ya kama mwendo wa sec 10 hivi kutoka kwa lile daraja ndipo sasa tukio lililofanya nilete huu uzi lilianzia, Walitokea vijana watano kama sio sita (sikumbuki vizuri ila hawakuzidi 6) watatu walikuwa na mapanga na wawili Visu, Walitokea ghafla kwa mbele (Hawa nafikiri walitupangia kwa muda mrefu na walikaa tayari kutusubiri maana ile barabara ya fire ni nyoofu sana na ukizingatia ilikuwa usiku basi nafikiri walituona toka mbali sana)

"OOOYAAA NYIEE TULIENI KAMA MLIVYO, NYIE NDO TUNAWATAFUTAGA KMMAKE ZENU" (Ni sauti iliyonifanya nigundue kuwa sasa kimenuka) Mimi kikweli kabisa sikupata woga kwa wakati ule ila Gf wangu fasta tu aliwahi kukaa nyuma yangu akawa analialia na kunung'unika tu, Sikufikiria mara mbili me niliona kabisa wale tunawavuka bila shida hivyo sikusimama nikajiongea kuwafuata Note: Ningeweza kukimbia na kuwaepuka wale jamaa ila akili yangu ilikuwa kwa yule dem kwamba ningekimbia lazima yeye angedakwa na Kesho yangu angeniona dhaifu sana.

"Oya wazee vp kwani" Niliuliza kwa sauti ya kikakamavu nikijua kabisa kwamba kuwa leo hawa jamaa hawatuachi ila hofu yangu ilikuwa kwa yule dem tu, Majamaa wakawa wanakuja kwa kasi ya kutembea kitendo kilichofanya yule dem aogope na kuniachia kwa nyuma kisha kuanza kukimbia kama anaelekea fire (maamuzi yake yale ndo yalimponza) Majamaa wawili au watatu wakamfuata wakimkimbiza mimi kuona vile niliusoma mchezo kwamba waliobaki wanataka kubizubaisha ili wale wengine wamdhuru mtoto wa kike, ilibidi niachane na wale watatu waliobaki ambao nahisi lengo lao lilikuwa ni kudeal na mimi wakati wale wengine wakideal na dem kitambo nipige hatua moja nilishtukia nimepigwa na kitu kizito kwenye mbavu tendo lililofanya niachane na uamuzi wa kumfata dem alipo na kuaza kupambana na majamaa wale watatu, Walianza kutaka kunisachi bila hidhini yangu maana waliona simu imejichora kwa mfuko.

"Oyaa toa simu na hela zote kmmako tutakuua leo" ~In Chuga voice ni sauti nilizokuwa nazisikia huku nikiwa nakwepa mashambulizi ya visu kutoka kwa wale jamaa, Pia ndipo nilisikia sauti ya dem wangu akilia kuonesha wale jamaa wameshamkamata, Jambo hilo lilinipa hasira mno kiasi lilinifanya sasa nivurugwe zaidi mixer kurusha mingumi ya hapa na pale Ebwanaeeh, ile siku nasema kabisa ni Mungu tu Katika mashambulizi yale hakuna kisu wala panga lililonigusa ila Ngumi yangu nilikuwa nikirusha lazima mmoja aende chini tatizo lilikuwa alipoongezeka mmoja tena kuwapa nguvu wale watatu ili wanichukulie vitu vyangu, Biligundua kuwa wawili walitumika kumteka yule dem na kuanza kuingia nae porini mule, Kufuata ule mto kama unaelekea mitaa ya Daraja mbili kama sikosei pale kuna miti mingi sana sasa walikuwa wanamvutia kule yule mtoto wa kike fasta niligundua kuwa lengo halikuwa kumnyang'anya tu simu na vitu vyake bali na kum'baka pia.

Wale jamaa wanne hakika wangeniua maana sikuwa tayari wanichukulie chochote kile waliishia kunichania nguo zangu tu nilizovaa, mparangano haukuwa wa muda sana, Mjue ilikuwa usiku sana Magari na boda zinapita tuu ila watu hawatoi msaada japo tulikuwa tunapigana hadi wakati mwingine tunafikishana katikati ya barabara kabisa ila ndo kwanza bodaboda zinatanua njia tu zinapiata asee, Washukuriwe walinzi wa karibu na eneo lile nafikiri kuna soko lipo karibu na maeneo yale walitokea wakiwa na Marungu na mapanga wale vibaka kuona vile wakaniacha na kutokomea porini kule walipoelekea wenzao na Dem wangu.

Nikiwa Mtaroni nimevurugika sio kitoto wale walinzi walikuja fasta wakanikamata, "Nyie ndo wezi tunawatafuta" "Hapana wazee wangu me ndo wale walikuwa wananiibia"
Wazee wale kusikia vile wakaniachia maramoja nakuanza kuniuliza kama nimejeruhiwa "Hapana mi nipo fiti wazee ila hawa jamaa wamemchukua rafiki yangu wa kike" nilesema vile nikiwa nalia kwa uchungu na hasira sana ila wale wazee waliishia kuniambia "Nenda nyumbani kijana hayo ni makosa yako kwanini utembee usiku maeneo haya hujui kama ni hatari" Kauli zile zilifanya nichanganyikiwe kabisa nikajikuta nawatukana wale wazee huku najiongea kuingia kwenye lile pori "Nyie wazee ni wase** sana yaani mnaona kabisa binti anachukuliwa mnashindwa kunisaidia" Wale wazee hawakujali hata maneno yangu wakaniacha wakaelkea zao eneo lao la lindo.

Niliingia kwenye lile pori usiku ule huku uoga ukiwa umeniondoka kabisa, Nilikuwa naongea mwenyewe mithili ya mtu mwenye kuvurugwa "Kmmake hawa wasenge nikiwakamata watafurahi..." nilikuwa nakifuata kinjia kuelekea mabondeni mwa mto ule huku nikiita "Marthaaaaaaaa" Kinjia kile nilibahatika kukutana na mzee mmoja kimtazamo ni 26no: yaani muhuni sikumuona uzoni vizuri maana kulikuwa na giza yaani mbalamwezi ndo ilikuwa ndo angalau inaangaza mule porini na sauti ilikuwa ya ulevi, nikamsimamisha bila woga (muda huo nilikuwa tayari hata kwa lolote, Kwa hama hakika yule mzee mfano angejaribu kuni-attack kivyovyote basi ningeweza hata kumuulia mbali, Woga uliniondoka kabisa) "Vp mzee hujakutana na vijana wanamburuza msichana mbele" "Ndiyo kwanini ni nani ako"

Nilimuelekeza tukio zima akasema anaweza kunisaidia kunipeleka hadi walipo hao vijana ila ataishia kunionesha mlango wa maskani kwao tu kisha atasepa ila kwa makubaliano kuwa ntampa 5000, Kweli nikakubaliana na yule mzee na safari ikaanza kuelekea mtaa sijui ndo unaitwa matejoo ambapo Wahuni shazi ndo nasikiwa ndo mitaa yao na viunga vyake, Narudia tena kwamba sikuwa na hofu na safari yangu yote nilikuwa nawaza tu jambo nitakalofanya nikishakutanishwa na wale jamaa ni vita tuu, Mzee alikuwa tukitembea dk mbili anageuka kuniliza "Oyaaa 5000 yangu si unayo lakini?" "Ndiyo mzee usiwe na shaka" Kila dk mbili kuniuliza vile alikuwa ananikwaza sana na kunipa hasira hadi nikawaza kwamba huyu mzee lait angejua kwamba hasira niliyo nayo naweza nikamuulia porini mule nimtupie mtoni basi asikaa kuniuliza uliza maswali, (Si una simu? jaribu mpigie kama anapatikana) Maneno yale ya mzee yalinitoa kwenye dimbwi la mawazo kumuawazia binti wa watu ambae yupo hatarini, Nilitoa simu mfukoni (Simu majamaa walishindwa kuichukua kutokana na mpambano wangu)

"Dah mzee simu ninayo ila imezima charge" "Oooh kumbe majamaa hawajakuchukulia simuuu" mzee ni kama alishangazwa sana na mimi kutokuchukuliwa simu, Nadhani huyu mze ndo maana alikuwa akiniuliza kila wakati kama 5000 yake ninayo?, Nafikiri alikuwa anahisi labda niliporwa vitu vyangu vyote hivyo nisingekuwa na hela ya kumlipa.... Baada ya pale mzee akuongea tena chochote na mimi bali alikuwa akiniongoza tu njia hadi tukatokea kimtaa fulani, Nyumba za udogo zilikuwa Mob sana, Ile mitaa inaonekana wanauza sana pombe za kienyeji nadhani ndo unaitwa mtaa wa Matejoo.

Tutaendelea...
 
Dogo uko moto sana bado nafikiria ulivyosema "nilipata romance ya nguvu sana kwa yule mtoto (I can't forget the moment
emoji22.png
)"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom