Nipige booster kwenye shamba langu la mpunga?

Pastory Kimaryo

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
967
664
Habari wana JF,

Tangu nimwage mpunga wangu mbegu fupi Salu ya miezi minne, imepita miezi miwili ila nataka niupige booster ili ukue vizuri japo nilitupia urea kidogo wiki kama tatu zilizopita, naombeni ushauri wanamageuzi wenzangu wa kilimo.

Natanguliza shukrani!
 
Mkuu,km ulishaweka mbolea ya UREA sikushauri kupiga booster kwasababu ni kitu kilekile, mwisho wa siku mpunga utakua Sana bila kuweka punje za mchele, kutokana na kuzidi kwa kiwango cha Nitrogen.Hivyo hutapata mavuno stahiki.Utakuwa Sana na utakuwa kijani kibichi kizuri kabisa lkn mavuno hafifu au usipate kabisa.
 
Urea niliweka kidogo, imagine heka mbili niliweka kilo 13 yaan nilifanya kurushia tu, pia nauliza mpunga ukipendeza kwa mbolea unaathiri mapato?
 
Ok!!!,Hicho ni kiwango kidogo, mpunga kupendeza kutokana na mbolea haiwezi kuathiri mavuno,isipokuwa km kiwango cha Nitrogen kitazidi mpunga utarefuka sana na kuwa kijani kibichi kizuri Sana lkn hautazaa vizuri.Ushauri wangu tumia SA(Sulphate of Ammonium),au NPK.
 
Nashukuru kaka kwa ushauri!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom