Nimekata tamaa ya maisha nahitaji msaada

gbefa

JF-Expert Member
Jun 1, 2016
3,801
15,798
Mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 25, muhitimu wa shahada ya ugavi na usafirishaji mwaka 2019 (Bachelor of Logistics and Transport Management) mimi ni moja kati ya vijana ambao tumemaliza chuo na kuingia mtaani kupambana na maisha bila kurudi nyumbani na hii ni mwendelezo tu wa hustling ambazo zilizianza wakati nimeanza chuo, hali za nyumbani ni ngumu tangu tunasoma, nipo hapa kuelezea hali yangu ya maisha kwa sasa na nini kimesababisha nimekataa tamaa na kuomba msaada.

Wakati naanza chuo mama aliniambia wewe ndio mkubwa na wewe ndio Mwanga wa hawa ambao wako nyuma yako ukidondoka wewe basi uenda ukasababisha wewe udondoke "pambana" baada ya kuingia chuo kweli nilipambana kwenye masomo na kwenye utafutaji nilibahatika kufanya biashara ya mkaa, chips, biashara na biashara ya rasta mambo hayakuwa mabaya sana.

Baada ya chuo nikaanza mishe za nafaka yaani naenda sokoni naomba order ya wanachohitaji nawapelekea, nilikuwa napeleka mchele, choroko, maharage ya njano na mahindi ya njano, sometimes ufuta n.k nikaongeza mtaji nikaenda kulima mpunga maana asili yangu ni mbeya huko bonde la Usangu Mbarali, nililima kwa tabu kwa kuwa mtaji ulikuwa mdogo kiasi chake ila nilivuna na nikarudi kwenye biashara ya nafaka, hii round two haikuwa nzuri ndio hii inanifanya naandika huu uzi hapa ķwanza biashara iligeuka ikawa mbaya sana tena sana unaomba order unapewa unatafuta mzigo ukifila sokoni madarali wanakushusha bei mno mara wato maji bure n.k Mama akanishauri nipange nikamwambia nina mtaji tu akanikopea around 1 ili jipange na inayobaki niongeze mtaji, nikafanya hivyo nikatafuta chumba cha 25 moro nikapanga nikanunua kitanda na godoro na jiko la gesi vyombo kiasi n.k nikahamia maghetoni kwangu, nikaendelea na biashara baadae mambo yakawa ya madarali sokoni nikakata mtaji kama laki 2.2 nikakopa tena laki 5 ili nifidie pale niendelee dah nikawa ndio naaharibu nikakata tena hela laki 3 hapo bado sijala wala sijanywa na sijamunua vocha plus usafiri n.k.

Maisha yakawa yanaenda kinyume nyume nikajikuta nimebaki na laki 6 tu mwezi wa kodi huooo na maji na umeme nikatoka laki na 2 kodi ya miezi minne na maji na umeme hapo hapo nikanunua msosi nikaweka ndani na gesi nikajaza nikabaki na aroundi laki 4 sasa mwenye deni akawa nataka pesa yake ukizingatia ni ndugu yangu nikaona nisipolipa nitashindwa kudhaminika wakati mwingine ikabidi mpunga uuzwe wote na bei ya mpunga ilikuwa chini sana imeniumiza mno nikalipa deni nikabaki na laki 6+ laki 4 nikawa na milioni nikalipia shamba la mahindi laki 3 ili nilime, nikabakisha laki 7 ndio hiyo nimetumia yote shambani na bado imefeli.

wakuu, kuna ule usemi wanasema ukitaka mali kaifate shambani lakini hawajasema kama hauna mtaji usiende kabisa.. nimefirisika hela zote zimeishia shamba na bado halijaisha nimefanikiwa kupanda tu, nilikodi heka 6 jamaa akaniongezea 2 zikawa jumla 8 nikalima na kupanda 5 kwa hiyo 3 ndio bado, ubaya hizi tano zishaota sina hela ya palizi hizi tatu shamba limelimwa mbegu ipo hela ya kupandia nilikosa, kitu nilichobaki nacho ni hii simu tu nimeomba msaada hadi nimeshindwa hata nyumbani nimeshindwa kupata msaada ndoto zangu zinazama naziona nina mambo mengi nilitamani niandike hapa ila nashindwa sipendi niwachoshe wasomaji, kifupi nilipofikia ni kubaya hata hela ya kula imekuwa tabu ingekuwa kipindi cha kiangazi ningebeba hata mizigo, gesi imekata, chakula sina na hela nimezika shambani ambako sijui mstakabari wake sina kazi wala kibarua na maisha ni magumu balaa gesi ilikata last week nimekopa chakula week nzima hadi jana jioni imefikia deni 21000 naogopa hata kwenda hadi muda huu sijala.

MSAADA NINAOMBA
naomba mdhamini wa kunidhamini kiasi cha fedha ili nirudi kwenye mstari maana hali ya shamba sio zuri kabisa nimepanda heka tano bado 3 lakini hizi tano za awali zinahitaji palizi, tuandikishiane kwamba baada ya mavuno achukue hela yake na nisitoe mavuno shambani hadi alipwe maana ili shamba ni la shirika kila kitu kinafata utaratibu au naomba msaada wa kibarua au kazi yoyote halali nafanya iwe ya kutumia ngumu au akili, mahali naomba iwe mikoa ya Morogoro, Dsm au Dodoma maana ndio karibu na shamba ambapo nimekodi. nilijaribu hadi kwenda bank kuomba mkopo ila masharti nikashindwa na muda unayoyoma nisadieni wakuu

NACHOWEZA KUFANYA
company management, controling, and monitoring, au kumuendesha mtu au watoto maana nina leseni ya udereva, kazi za usisamizi wa store, biashara ya chakula, duka la nafaka au pembejeo za kilimo, Ushauri wa kampuni za chakula au mifugo, uandaaji wa business plan, project, kazi ugavi na usafirishaji, customer hospitality n.k nikipata sehemu ya part time, internship au kujitolea nitashukuru sana.

KAMA UNAHITAJI SOMETHING IN RETURN ILI UNIDHAMINI KARIBU PIA
Mfano, mtu mwingine awezi kutoa msaada kama jambo ana faida nalo, basi kama unahitaji kitu in return karibu mfano nikupe heka 2 au kama utaongeza napo ni jambo zuri hizi ulime hata alizeti mimi nitasimia physical maana nipo huku huku nitakusimamia kwa uadilifu mkubwa, natamani nitengeneze connection kwa uaminifu nataka ukinidhamini unitangaze vizuri ili niaminike

SKILLS
COMPUTER SKILLS:
1-Recording requisition (TMIS)
2-Microsoft office programs (Introduction to Ms Windows, Ms World, Ms Excel, Ms Access, Power point, Email and Internet).

PERSONAL SKILLS:
1-Strong communication skills in both oral and written including presentation skills, ability to work under pressure and willingly, team work and entrepreneurship skills, convincing power, fast in learning .
2-Strong communication skills in both oral and written including presentation skills, ability to work under pressure and willingly, team work and entrepreneurship skills, convincing power, fast in learning .

DRIVING SKILLS
With driving licence class A, B and D

MSAADA UNAWEZA KUWA FURSA
Hapa naweza nikawa nahitaji msaada ila napenda kutoa angalizo inaweza ikawa fulsa kwa vijana wenzangu kama mimi kwa maana kwamba ikitokea nisaidika basi naahadi itakuwa ndio mwanzo wa mimi kumvuta mtu mmoja au kijana mmoja ili baadae tuwe hata 10 tuendelee kuvutana kupitia nafasi ambayo tutaipata nataka niubadili huu mtazamo kwamba "Black people share cigarettes and beers but never opportunities".

N.B
uzi huu nimeandika nikiwa na mawazo kidogo hivyo unaweza usifurahishwe na aina ya uandishi wangu kama una swali au maoni na ushauri usisite kuniandikia hapa nitafarijika endapo ukinisaidia hata mawazo namna ya kufanya, nahitaji msaada waday uenda usiguswe na uandishi wangu maana uandishi ni kipaji ila nahitaji msaada mno kula yangu siijui kabisa

Mawasiliano;
Kama utahitaji maelezo ya ziada au CV, unaweza kuni-dm, kunipigia au
kunitumia ujumbe mfupi: 0625858406
Napatikana Morogoro kwa sasa ikitokea nafasi kati ya Dom au Dsm naweza kufanya pia.
 
Hadi nimefikia naandika humu tambua nimeshapambana sana, hii ya mitandaoni tunafanyaga as last option, nilikosa kaka ndio maana nimekuja humu, najua wapo waadilifu na ambao sio waadilifu nitajitahidi kuwavumilia hawa wa upande wa pili
Watu wa humu wengi huwaga hawana msaada wengine watakuponda na kukuongezea machungu nakupa angalizo usishtuke sana...
maoni yangu kwanini usitafute partnership na watu wenye mitaji
 
Mapambano mwanzo mwisho! Shamba halitaki ushalobalo, shamba halitaki uanze kuwaza matokeo kabla ya kuwaza process, shamba halitaki mkumbo baba, shamba ni biashara kuwa na malengo, hesabu, na adabu ya pesa.

IMG_20210208_144030.jpg
IMG_20210208_143929.jpg
 
Kwahiyo ungevaa gum boot ungekua sharo?
Ndiyo maana nasema shamba halitaki ushalobalo, hapo skuwa na safari ya shamba ratiba ilibadlika juukwajuu, hakuna muda wa kutafta excuse sjuwi gumboot sjabeba, sjuw nimetokea wapi, sjuw ntachafuka.

Usimamizi wa shamba unatakiwa uwe close, kama wanapanda ingia ushuhudie upandaji spacing ziko sawa? Mbegu wanatia na kufukia kwa usahihi? Kama ni mbolea tembea kuona kiwango kinachowekwa ni sawa? Siyo kulaza siti ya gari na kusklza muziki kisa unawalipa!
 
Siku nyingine dalali wakikuzingua, badilika wewe ndo uwe dalali, fanya legwork, tafuta namba za wale wanaonunua nafaka toka kwa wakulima katika area yako, hakikisha unapata ikiwezekana zote.

Rudi kijijini, wewe kazi yako unawatime wakulima wa vijijini kwa kuwapeleka lilipo soko, mfano wewe unepewa bei ya 1500 kilo ya maharage, mkulima mpe bei ya 1300,1350 ili ule hiyo 200 au 150.

Mtaji wako hapa ni vocha,mdomo wako na hela ya kuzungukia.
 
Ndiyo maana nasema shamba halitaki ushalobalo, hapo skuwa na safari ya shamba ratiba ilibadlika juukwajuu, hakuna muda wa kutafta excuse sjuwi gumboot sjabeba, sjuw nimetokea wapi, sjuw ntachafuka. Usimamizi wa shamba unatakiwa uwe close, kama wanapanda ingia ushuhudie upandaji spacing ziko sawa? Mbegu wanatia na kufukia kwa usahihi? Kama ni mbolea tembea kuona kiwango kinachowekwa ni sawa? Siyo kulaza siti ya gari na kusklza muziki kisa unawalipa!
Sawa sawa mkulima makini.
 
Back
Top Bottom