Nioe yupi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nioe yupi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mwiba, Jan 19, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kuna msichana ana miaka kuminatano(15) na mwengine ana miaka ishirininatatu(23) wote wapo ready au tayari ,mwenye umri wa miaka 15 amemaliza la saba na amepasi lakini atakuwa tayari kuolewa akishapitisha miezi sita na ni makubaliano ambayo hayana wasiwasi yameshakubalika kwa pande zote wazazi wazee na yeye mwenyewe ,huyu wa miaka 23 yeye anafundisha yaani ni mwalimu.

  Njemba inayotaka kuoa ina miaka 42 ila anaonekana ni mdogo kiumbo, wapo wanaoshauri bora huyu alie na miaka 15 eti ataweza kumlea na kumfundisha pia ana ladha na sauti zinazopishana kwa kuvutia na kusononeka kuliko wa miaka 23 na kumponda yule wa miaka 23 wakisema anaijua dunia vilivyo na hasa alivyokuwa msomi kutakuwepo na mbinde ilivyokuwa ni mtoto wa mjini na ameshapita hadi formsix na chuo cha ualimu ila wanaomtilia na kumuunga mkono huyu wa miaka 23 wanasema atakuwa ameshaijua dunia vilivyo na hivyo uamuzi wake wa kukubali kuolewa ni uamuzi mzuri unaofikiwa na wakike wanaotimiliza miaka hiyo(ukubwa) na kumponda yule wa miaka kumi na tano kwa kuwa huwa wanabadilika hasa watimiapo miaka 21 na wanakuwa rahisi kuanza kubishana na huwa hawakataziki.

  Wana JF nini ushauri ,mawazo na uchambuzi wenu ???
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Miaka 15?

  PEDOFILIA..
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hutakiwi kumaka au kuuliza yanahitajika maelezo na sababu zako ili tuweze kujadili.
   
 4. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #4
  Jan 19, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tuletee CV yako hapa
   
 5. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #5
  Jan 19, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  unataka mjadala upi? hata huo ni mmojawapo.
   
 6. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wote watatu (Njemba, Teacher na Teenager) wakapime kwanza AIDS, walete HIV status zao hapa ili tuendelee na ushauri. Vinginevyo unaweza kutoa ushauri kumbe unasaidia kusambaza.
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapana ndugu, ulichohitajiwa ni kutoa ushauri na nasaha zako ,inaonekana unapinga kwa wa miaka kumi na tano ,toa sababu au unaogopa kuaibika ,natumai umeona jinsi watu katika habari yenyewe walivyotetea na kupinga.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sass samahan bosi kama nimekukwaza..lakini si unasikia serikali kila siku inasisitiza watoto wa kike wapelekwe skuli wapewe darsa, iwasaidie maishani? Sasa haya mambo ya kukubali wakubali wazazi wake, kuolewa aolewe mwingine ni mambo ya karne hii?

  Halafu haiwezekani binti averaged 15yrs old Tanzanian CHILD amvutie mtu ambaye hana TAATHIRA YA U-PEDOFILIA, kiasi cha kutaka kumuoa..

  Hayo ni maoni yangu tu..
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  15 years girl is not a child anymore haswa siku hizi na hapa makwetu kama utatembelea sehemu zenye muziki nyakati ya jua linapozama utanifahamu vizuri kuwa hao wa kumi na tano huwa tayari wameshapevuka na ukielekea ukabilani ndio kabisa ,huachishwa hata shule.kuna mbegu zingine miaka kuminatano unaweza kufikiri ana miaka 25 hasa huko uzunguni na sehemu za bara ndani,kuna tofauti kubwa kati ya wasichana wa pwanipwani Tanga ,Dar ,Mtwara na wa mikoani.

  ila kutokana na hoja wapo wawili.
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kwakuwa kigezo hapo juu ni umri na elimu, nashauri aolewe mwenye miaka 'mwalimu' wa miaka 23. Hayo ya udogo wa umbo, kuielewa dunia na kufundishika yote yanasahihishika ndani ya ndoa.

  ...Binti wa miaka 15 madhali amefaulu, apewe nafasi ya kujiendeleza kimasomo, By the time akifikisha umri wa miaka 23 naye atakuwa ameelimika tosha kuja waelimisha wanawe pia.
   
 11. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  1) Miaka 15 bado ni mtoto kisheria na kisayansi
  a) Mambo ya sheria yatakuwa na utata niyaache
  b) Kisayansi umri huu ndio wanapata matatizo sana ya uzazi na husababisha hata kifo wakati mwingine kwa sababu bado wanakua.
  2) Mtoto pia amefaulu, mbona wanataka kumpoteza?
  3) Pia huyu mzee wa miaka 42 na mtoto wa miaka 15 mbona wamepishana sana? By the time anafikia miaka 60 "fimbo lugoda" haifanyi kazi vizuri "mtoto" ndio atakuwa na miaka 33 ndio kipindi anahitaji hasa "tendo" matokeo yake ni huyo mzee kuachwa solemba kwa kuwa hatamtosheleza, au ataletewa magonjwa n.k.
  4) Wote hawamfai, lakini kama ni lazima achague kati ya hao, amchukue wa miaka 23.
   
 12. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  Tatizo ni sheria ya Ndoa ya Tanzania ya 1973 ambayo inaleta utata. Sheria hiyo inasema kwamba binti wa miaka 15 anaweza kufunga ndoa kwa kupata ridhaa ya wazazi au mlezi wake.

  Hiki kifungu kinaenda kupingana na kile cha makosa ya kujaamiana(1998) ambayo inasema kwamba mtoto chini ya miaka 18 hawezi kukubali kufanya mapenzi na ukifanya naye mapenzi basi inachukuliwa kwama umembaka(statutory rape).

  Tukija kwenye suala la tafsiri za sheri hizi mbili, basi napenda kusema kwamba kulingana na sheria ya tafsiri ya sheria(tanzania) inabainisha kwamba sheria iliyopitishwa karibuni itaweza kuchukuliwa kama tafsiri sahihi ( subject to arguments).

  Huyo jamaa, anatakiwa ajiweke katika viatu vya mzazi huyo na kujiuliza kama angekuwa binti yake angeweza kuwmoza kwa jamaa wa miaka 42?

  Hitimisho langu ni kwamba jamaa ni mbakaji mtarajiwa na aangalie mkondo wa sheria unamfuata. Pili binti huyo kafaulu kwenda sekondari(kulingana na maelezo ya mtoa hoja) kwa hiyo ni kutaka kumwalibia maisha yake.
  Tatu, sote hapa barazani tunatakiwa kukemea vitendo kama hivi vya ubazazi kwa nguvu zote.
   
 13. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Asante kutuelewesha!
  Nadhani muoaji ambaye ndio mtoa hoja imemuingia hiyo. Kichwa cha habari kinajionyesha wazi mtoa hoja ataka ushauri!
   
 14. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bw. Mwiba hakuna cha kujadili hapo. Miaka kumi na tano-kwa sheria zozote zile dunia hii - huyo ni mtoto. Jee hivi kweli tunaowa watoto siku hizi? Lete mada yenye maana tujadili siyo hii.
   
 15. G

  Giroy Member

  #15
  Jan 19, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa mshikaji ulikuwa unasubiri nini mpaka umefikisha umri wa 42 hujaoa.au una mchezo wa kuacha,hayo tuyaachi hapo.samahani kama nimekukera.kwa kukujibu kwa maoni yangu achana na huyo wa miaka 15 akasome.nahata kama hasomi tofauti yenu nikubwa sana kwa umri,hilo ni jambo ambalo litakuletea usumbufu ktk maisha.Wasiwasi wangu mtakuwa mnapishana sana mawazo,wakati wewe unawaza kujenga,yeye anawaza kwenda disco,na vitu vingine vya ujana.ukimnyima utakuwa unamtesa,wakati mwingine ndoa inaweza kuvunjwa na mazingira kama hayo.MKE SI MTOTO,NI MWENZA,WENZA hubadilishana mawazo_Oa mtu ambaye hampishani sana itakusaidia.umeelewa ndg yangu?
   
 16. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mtoto chini ya miaka 18 hawezi kukubali kufanya mapenzi? au ni lugha tu mkuu hapo?
   
 17. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama katika karne hii kuna mtu anyeweza ku contemplate marriage kabla 'hajaonja'! Kuna kila indication hapa kuwa huyu anayetaka ushauri wa kuoa keshaonja kote (including hako ka 15!) na kaona kote kutamu ndo maana kachanganyikiwa hajui achukue kipi jumla! Hapo kwa miaka 15 ni suala la kisheria na kama tungekua nchi za watu nina hakika Mkuu Mwiba ungeupata ujio wa jamaa waliotinga gwanda dakika yoyote kuanzia sasa!
   
 18. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwiba nyinyi wazaramo nini mkuu???
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Amehusu Pemba
   
 20. b

  bAbiLoN Member

  #20
  Jan 20, 2009
  Joined: Jan 17, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  we we we, huyo kikongwe ujana wake ale na nani ubabu wake amalizie kwa watoto wa watu, ukiangalia hat interval ya umri almost wote wawili anawazaa
  Kaka wa shule aende shule, huyo babu wa miaka 42 anajifia muda sio mwingi sana.
  Hivi vitu na haya mambo yapo jamani sioni sababu ya ako kabinti kuolewa wakati
  hata future hakajatengeneza alafu sihisi kama anajitambua vya kutosha huyo teenager.
  Teacher jibu analo mwenyewe, she knows whats good for her!
   
Loading...