Ninunue Range Rover sport au Land Cruiser VX?

Ninunue Range Rover sport au Land Cruiser VX?

E52

Member
Joined
Oct 31, 2010
Posts
81
Reaction score
14
Wadau poleni na majukumu...

Nimejaribu kufanya utafiti ili niweze kujua ubora wa haya magari mawili,,,

Ninaomba ambao wanayamiliki au wenye upeo nao wanisaidie nifanye uchaguzi sahihi....

Ninunue kati ya Range Rover Sport au Land Cruiser VX?

Natanguliza shukrani
 
...land cruiser ni nzuri na multipurpose,unaweza fanyia kazi za kawaida na oficial/kujirusha na consuption ya mafuta ni nzuri kuliko range. Ila range si rahisi kubadilika fasheni.

So kama mimi i'll go 4 made in UK kuliko mjapani...
 
Sijaendesha Range ila Land Cruiser hizi mjapani za Diesel zinakula mafuta vizuri sana kuliko hata gari ndogo hizi mnaita GX 110.

Kama unaenda for fuel consumption pengine Land cruiser itafaa. Kama unatafuta gari luxury bila kujali mafuta, spea na gharama zingine Range inapendeza zaidi.
 
Afadhali umesema hujaendesha Range Rover.....

Kuna TDV6 engine cc 2700, TDV6 cc 3000; hizi zina fuel consumption bora kuliko Land Cruiser...

BTW kama unaanza kuuliza range rover inakula mafuta vipi basi obviously thats not ur car!

TDV6 2700CC INAKUPA 10KM/L..........TDV6 CC3000 INAKUPA 8.5KM/L
 
Wadau poleni na majukumu...

Nimejaribu kufanya utafiti ili niweze kujua ubora wa haya magari mawili,,,

Ninaomba ambao wanayamiliki au wenye upeo nao wanisaidie nifanye uchaguzi sahihi....

Ninunue kati ya Range Rover Sport au Land Cruiser VX?

Natanguliza shukrani

Wengine bado tunasubiri bahati nasibu ya Bajaj na tiGO.....Labda ungeuliza kati ya Swift na Vitz angalao..
 
mleta mada hajazungumzia mafuta wala spea yeye anataka gari bora chukua range rover mkuu hutajutia pesa yako yani ukiwa una-drive iyo gari kama upo mbinguni vile!
 
Wengine bado tunasubiri bahati nasibu ya Bajaj na tiGO.....Labda ungeuliza kati ya Swift na Vitz angalao..

We Tedo wewe ndo nini sasa?? Watu tumezisubiria hizo bajaj only to find out zimeisha!! Mwe! Wakati wengine wanawaza kubahatisha bajaj na Tigo, wengine wanashindwa kuamua wanunue mtumba upi wa nguvu. Maisha haya ama kweli hayafanani. Wahenga walijisemea 'jikune mkono wako unapofikia' sijui ndo hivo walivosema....?
 
Back
Top Bottom